Asante sana mkuu. Na mimi nilifikiri kuwa kuna masharti ya ukaazi yanayoweza kumpa mtu wa bara Uzanzibari, lakini nikatukanwa kwamba sijui kitu hapa.
Zanzibar haina uraia, kwa sababu si nchi kamili. Uraia ni jambo la Muungano, kuna uraia wa Tanzania tu. Uraia wa Zanzibar ulikufa baada ya Muungano, kama uraia wa Tanganyika.
Kule kuna ukaazi tu.
Nafikiri ukaazi huu, angalau kinadharia tu, unafanya hii distinction ya "Mzanzibari" isiwe na maana kubwa.
Kwa sababu, in theory, kila Mtanzania anaweza kuwa Mzanzibari, sema kuna wengine wamezaliwa Zanzibar hawana masharti ya kukaa miaka hiyo inayotakiwa kabla ya kupata ukazi, na wengine wanatoka bara inawabidi wakae miaka hiyo.
Na hiyo miaka imewekwa hivyo, kwa sababu Zanzibar hawataki watu wa bara waende kwa wingi kupiga kura Zanzibar na kubadili matokeo ya uchaguzi bila kuwa wakazi, pamoja na kudhibiti watu wengi wa bara wasije kununua ardhi kwa sana na kuibadilisha Zanzibar.
Sasa, tukimkatalia Shaka kuwa Mkuu wa Wilaya bara, na Mndengereko atakayehamia Zanzibar naye akataliwe kuwa Mkuu wa Wilaya bara?
Wale kina Sepetu kina Wema baba yao alikuwa Zanzibar sana, kina Adam Mwakanjuki wamekaa sana Zanzibar mpaka SMZ walikuwepo.
Hawa nao wapigwe marufuku vyeo vya serikali ya Muungano kama vya ukuu wa Wilaya bara?
Ukianza siasa hizo maana yake nini? Utasema wakuu wa wilaya za Dar wote wawe Wazaramo? Wasije Wabondei kuwa wakuu wa Mkoa wala wilaya Dar?
Hapo hamuoni mnaanza dhambi ya ubaguzi aliyoisema Nyerere (probably akirejea mfano wa Simba walawatu wa Tsavo kutoka kitabu cha "The Man Eaters of Tsavo" cha John Henry Patterson) kuwa ni sawa na kula nyama ya mtu, ukianza huachi utabagua watu mpaka kwenye koo na familia?