Mdude CHADEMA: Hii katiba haifai, Wazanzibari wanakuwa wakuu wa wilaya Tanzania bara huku Watanganyika hawaruhusiwi kuwa wakuu wa wilaya Zanzibar

Kamwe tena wasahau Zanzibar kuwa mkoa !! Zanzibar ni Nchi kamili iliyoungana na Tanganyika hapo juzi juzi mwaka 1964 !! Zanzibar ilikuwepo kwa karne na karne kama Nchi ! Someni history yake !!
 
Ubaguzi ni Unyama !!
 
Kwa hiyo nchi imeamua kuajiri raia wa kigeni kwenye nafas za utawala? Usije kushangaa siku moja kuna mtendaji wa kata kutoka china!
 
Wenyeji na hawa Watanganyika waliokaribishwa vizuri wakaona Sasa ni wakati wa kuichukuwa nyumba. Wazanzibara
 
Tulia uandike vizuri basi, unapanic nini au Shaka!!?
 
dah kumbe ana mume? niliwahi sikia mengi mabaya kwa kweli
Hata mimi nilishasikia mabaya mengi sana kuhusu wewe lakini niliona hayana maana yoyote. Vivyo hivyo na ya Zena mwachie Zena mumewe.

Uzuri wa Zena aujua mume wake
 
Hakuna mtanzania Nusu. Kwanini watanganyika wanajimilikisha Tanzania?
Chako changu changu changu. A 20 years assimilation policy would have cleared this mess.

Nyerere alitupoteza hapa wadanganyika.
 
Aya ya kwanza hauko sawa hali hiyo ingeua utaifa ndiyo maana watu hawataki kusikia habari za machifu

Bila shaka kama tungelazimisha kuwa na serikali moja ili rais awe na mamlaka kamili na visiwa vya Zanzibar kwa sasa hali hii isingekuwepo.

Kuna ongezeko la manunguniko kwa Watanzania bara kuona Zanzibar ikichotewa pesa za misaada lukuki ilihali haichangii chochote kwenye kulipa, wazanzibar kuteuliwa hata kwenye wizara zisizohusu masuala ya Muungano, rais wa sasa ameenda beyond wizara anateua hata kwenye ofisi zingine za umma ambazo siyo sehemu ya masuala ya Muungano ilihali Zanzibar watanzania wanachukuliwa kama foreigners.

Zamani tuliona Nationalism ikikua Zanzibar katika mrengo wa secession lakini sasa kwa sababu wananufaika direct na Muungano ni kama wametulia hali hiyo imeibuka tena kwa watanzania bara ambao ni wazi tofauti na mambo ya kisiasa ni kama Muungano hauna maana kabisa kwao.
 
Ile one man show ya Nyerere ilikuwa kubwa sana kiasi kwamba iliharibu mengi kuliko kutengeneza.
 
Kamwe tena wasahau Zanzibar kuwa mkoa !! Zanzibar ni Nchi kamili iliyoungana na Tanganyika hapo juzi juzi mwaka 1964 !! Zanzibar ilikuwepo kwa karne na karne kama Nchi ! Someni history yake !!
Historia ni mkusanyiko wa matukio hivyo inaweza kutengenezwa tu.

South Sudan never existed before lakini sasa ni taifa linalojitegemea.
 
Historia ni mkusanyiko wa matukio hivyo inaweza kutengenezwa tu.

South Sudan never existed before lakini sasa ni taifa linalojitegemea.
Ni kweli kabisa historia inaweza ikatengenezwa ya uongo na ikapigiwa debe sana ili ionekane ni ya kweli ! Lakini kwa Zanzibar it’s another case !! Zanzibar ilikuwepo kama Nchi na baadaye ikaungana na Tanganyika !!
 
Basi waiondoe kama haiwez kuwa mkoa.
 
Kiukweli sioni maana ya muungano kwa hili
 
Na bado mmewakumbatia Zanzibar mda wote wamekuwa wakiukataa huu muungano kwa taarifa yako hakuna mzenji anaetaka hilo dubwashko linaloitwa muungano ni kiherehere chenu tu wabara.
CCM ni adui wa Watanganyika na Wazanzibari. Ni CCM ndiyo inang'ang'ania huu Muungano .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…