Mdude CHADEMA: Hii katiba haifai, Wazanzibari wanakuwa wakuu wa wilaya Tanzania bara huku Watanganyika hawaruhusiwi kuwa wakuu wa wilaya Zanzibar

Mdude CHADEMA: Hii katiba haifai, Wazanzibari wanakuwa wakuu wa wilaya Tanzania bara huku Watanganyika hawaruhusiwi kuwa wakuu wa wilaya Zanzibar

Natoa ushauri kwa CHADEMA watu kama mdude CHADEMA na wengine wenye aina yake ya siasa hawaisaidii CHADEMA Bali wanaiharibia kabisa.

Kwa mujibu wa katiba ,uteuzi wa wakuu wa wilaya unafanywa na Rais kama ulivyo kwa uteuzi mwingine wowote wa kikatiba.

Mfano, aliyekuwa katibu mkuu wizara ya nishati Tanzania bara mhandi Zena ,Rais Dkt. Mwinyi alipoingia tu madarakani alimteua kuwa katibu mkuu kiongozi na katibu wa mabaraza la Mapinduzi la Zanzibar, cheo cha juu kwa utumishi wa umma Zanzibar.

Sasa Kama mtanganyika amepewa cheo Cha juu kabisa Cha utumishi wa umma ,ni kweli
Mkuu wa wilaya hawezi kuteuliwa?

Acheni upotoshaji CHADEMA mtapoteana mtafute mchawi
Huyo dada ni Mpemba soma vizuri historia yake. acha kukurupuka
 
Aache roho mbaya, wote ni watanzani, kinachopaswa kufanywa ni kupeleka na wabara kwenye wilaya za Zanzibar. Tuache ubaguzi
Utawapeleka vipi wakati katiba za nchi zote mbili(kwa maana ya nchi ya Zanzibar na nchi ya Tanzania) haziruhusu jambo hilo, yupo sahihi kulalamikia katiba kwamba mambo hayapaswi kuwa hivyo hii katiba ni mbovu kwa sisi Watanganyika na haifai hata kidogo.
 
Wazanzibari tumeshawazoea. Wenyewe siku zote ni waumini wa ule msemo wa changu changu, chako changu.

Kiukweli hawa jamaa ifikie wakati wajitawale tu, ili na sisi Watanganyika tupumue.
Vipengele vya muungano ulishawahi viona!?
 
Charles Hillary mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Zanzibar.huyu ni mbara kabisa
 
Muungano wetu Tanganyika na Zanzibar ni wa asili. Hasa wazanzibara. Hivyo ili kuweka sawa kule ni mikoa 5 tu na serikali moja kwisha. Vinginevyo tuwe na federation . Lakini hii ya chetu cha wote lakini chao ni chao karne hii naona giza
 
Tumieni akili acheni uvivu, ile ni serikali ya Zanzibar, hii ni serikali ya muungano. Ndiyo maana mlishindwa hisabati mapema sana. This is simple logic.
Ndio mana tunataka katiba mpya, ili kipengele hiki kiwekwe sawa kwa faida ya wote
 
Msiwe wachawa. Jiridhisheni na mnayoleta humu. Mtanganyika haruhusuwi kumiliki hata ardhi Zanzibar maana siyo wa nchi ile kama ambavyo hapa kwetu Mkenya hatakiwi kumiliki ardhi. Kazi hawaruhusi isipokuwa ajira za sekta binafsi na sekta isiyo rasmi.
Kaisome vizuri sheria. Mimi ndiyo hufahamu. Kwanza katiba ya Zanzibar inasema ardhi yote ya serikali. La pili mtanzania akikaa znz miaka mitatu ana haki ya kumiliki ardhi. Nakupa homework wilaya ya kati wakazi wake asilimia na magharibi A zaidi ya 40% ya wakaazi wa wilaya hizo wana asili ya Tanganyika. Wanyamwezi, wamanyema, wandengereko, waruguru, wamakonde na wengine. Sasa wewe hizo data zilizotoa.mwanzo zinangalie kama.ni za uongo. Mnaropokwa na kuwapqta wajinga kama.nyinyi. Naibu Havana wa benki kuu kutoka Zanzibar ni mtanganyika na alipokuwa znz alishika nafasi kibao na kwa miaka mingi alikuwa katibu mkuu.
 
Hili ni Donda Ndugu. Nyerere na ujanja woote alikwama! Hawa wengine wanapapsa tu. Ngoja tuone samia! Ila ukweli labda katiba ije
 
Natoa ushauri kwa CHADEMA watu kama mdude CHADEMA na wengine wenye aina yake ya siasa hawaisaidii CHADEMA Bali wanaiharibia kabisa.

Kwa mujibu wa katiba ,uteuzi wa wakuu wa wilaya unafanywa na Rais kama ulivyo kwa uteuzi mwingine wowote wa kikatiba.

Mfano, aliyekuwa katibu mkuu wizara ya nishati Tanzania bara mhandi Zena ,Rais Dkt. Mwinyi alipoingia tu madarakani alimteua kuwa katibu mkuu kiongozi na katibu wa mabaraza la Mapinduzi la Zanzibar, cheo cha juu kwa utumishi wa umma Zanzibar.

Sasa Kama mtanganyika amepewa cheo Cha juu kabisa Cha utumishi wa umma ,ni kweli
Mkuu wa wilaya hawezi kuteuliwa?

Acheni upotoshaji CHADEMA mtapoteana mtafute mchawi
Ni kwamba hauna akili kabisa au umeamua tu kujitoa ufahamu.
 
Ni sahihi mtoa mada sisi wa bara hata ajira huko unguaja na pembe uwez pata bila ya kitambulisho cha mzanzibar

Wasiofk na kuish Zanzibar ndio wataipng hii hoja
 
Huyu n mjinga wa kupuuzwa. Mkuu wa wilqya magharibi A susaz kunambi, mkuu wa wilaya ya kati Medina Joel Thomas, Meneja mkurugenzi PBZ, Mkurugenzi ZBS na ZRA( ZRB) hao wote ni Watanganyika na hawana wazee znz. Zena katibu mkuu kiongozi. Babu yake ndiyo.alikimbia Pemba lakini yeye kazaliwa tanga na hajawahi kutumikia Seriki ya znz. Ali Hassan Mwinyi amekuja znz ana miaka 10 na amechauliwa kuwa raising wa Zanzibar, Aboud Kumbe Mwinyi kwao ni.mji mwema na amekuwa rais wa znz. Sasa huyo.mdude mpuuzi. Na ako wakurugenzi wa wa wizara wengi sana baba zao wana asili ya Tanganyika na hivi sasa viongozi. Kwani mnasema Zena siyo.mtanganyika kwa sababu babu zake wana asili ya kizanzibar. . Hayo.madai yenu yq katiba mpya yataonekana ni upuuzi wa sabau mnazozitoa. Eti chakuna kimepanda bei na suluhisho lake katoba mpya!!

Wewe ni kizibo,acha kujitia uchizi zenji kuna upuuzi mwingi.
 
Back
Top Bottom