PreGE2025 Mdude Nyagali adaiwa kukamatwa na kupigwa na watu waliojitambulisha Polisi

PreGE2025 Mdude Nyagali adaiwa kukamatwa na kupigwa na watu waliojitambulisha Polisi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kimya SIku ya 19 ,Si TLS Mwabukusi,Si Mwenyekiti wa kanda ,Si wanachadema wakimpambania Sumu ya nyigu....Wanaharakati ndiyo muone kwamba hakuna atakayekupigania sako kwa bako ,aliokuwa anawapambania wote wamekaa kimya sasa wanafanya mambo yao....inayoteseka kwasasa ni familia ya Mdude.
Inasikitisha sana.

Said Mpaluka Nyagali aka Sumu ya Nyingu ameenda kama Ben Saanane ,Soka n.k
 
Mwanachama wa JF na mdau mkubwa wa mitandao, Mdude_Nyagali amechukuliwa na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi usiku huu.

Walikuwa na silaha, wamevunja mlango.

Mdude amepigwa sana, alikuwa amelala nyumbani kwake Mbeya.

Watu hao wamevamia wakiwa na silaha, wakabomoa mlango, wakampiga sana na wakaondoka naye. Haijafahamika amepelekwa kituo gani cha polisi.

Inadaiwa walibomoa mlango wa nyumbani kwake na kuingia ndani wakiwa na silaha za moto. Watu hao wamempiga na kumvuta chini damu ikimwagika kuelekea pahali kusikojulikana.

Rais wa TLS naye amesema:

Nimepokea habari Usiku huu kwamba Jeshi la polisi Mbeya limefika nyumbani kwa Mdude Mpaluka Nyagali.

Baada ya kufika wamevunja mlango na kuingia ndani na kumpiga wa kitumia vitu mbalimbali na kumjeruhi na baadaye kuondoka naye.

Huu ni muendelezo wa kukithiri kwa vitendo vya wanao onekana wakosoaji wa Serikali kutendewa kinyume cha Sheria na Kuumizwa.

Tunalitaka Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kuhakikisha kuwa Ndugu Mdude Mpaluka Nyagali anakuwa salama na kuhakikisha wanampatia matibabu stahiki.

Tunakemea na kufuatilia jambo hili kwa ukaribu kuona haki ikitendeka.

Boniface A.K Mwabukusi
WAKILI.

View attachment 3322353

*****
MDUDE NYAGALI NI NANI HASA?

View attachment 3322349
​
Mdude_Nyagali , anayejulikana pia kama "Mdude Chadema," ni mwanaharakati wa kisiasa na kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) nchini.

Alizaliwa tarehe 25 Agosti 1987 katika kijiji cha Isongole, Wilaya ya Ileje, mkoa wa Mbeya (sasa Songwe). Tangu mwaka 2008, amekuwa mwanachama wa CHADEMA na amejihusisha na shughuli mbalimbali za kisiasa, ikiwa ni pamoja na kusimamia kampeni za wagombea wa chama hicho.

Mdude amejipatia umaarufu kwa kuwa mkosoaji wa wazi wa serikali kupitia mitandao ya kijamii na majukwaa ya kisiasa. Mara nyingi hujitambulisha kama mpiganiaji wa uhuru wa kujieleza, haki za kiraia na utawala bora.

Mnamo Mei 2019, Mdude alitekwa na watu wasiojulikana kutoka ofisini kwake katika Wilaya ya Mbozi, mkoa wa Songwe. Baada ya siku tano, alikutwa akiwa amejeruhiwa katika kijiji cha Inyala, Mbeya. Alidai kuwa alitekwa kwa sababu za kisiasa kutokana na ukosoaji wake dhidi ya serikali.

Katika maisha yake ya kisiasa, Mdude amekumbana na changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uchochezi na usafirishaji wa dawa za kulevya. Hata hivyo, ameshinda baadhi ya kesi hizo, na mnamo Juni 2021, Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya ilimuachia huru baada ya kumkuta hana hatia katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin.

Usiku wa Mei 2, 2025, taarifa za kukatamatwa kwake zimesambaa kupitia video inayoonekana mtandaoni. Hadi asubuhi hii, hakuna taarifa rasmi zinazoelezea ni wapi alipo pamoja na hali ya afya yake.

--- Jeshi la Polisi likichukua vielelezo eneo la tukio ---
View attachment 3322576View attachment 3322577
​
Pia soma
  1. Pre GE2025 - Martin Masese: Polisi wamefika nyumbani kwa Mdude kuchukua Sampuli ya damu ili waanze uchunguzi
  2. Sakata la kutekwa kwa Mdude, mzee afichua jinsi Polisi walivyomfuata kutaka awasaidie kumfanyia Ujasusi ili wampate
🥶
 
Ni mwaka umetimia , Mdude hajulikani alipo hakuna uchunguzi wala majibu kwa watu tunaoambiwa wanalipwa kulinda watu na mali zao.

Leo hii ni mwaka mmoja kamili kijana mwingine katekwa kwa mtindo ule ule kama walivyomteka .


View: https://x.com/i/status/2050566627079401869

Tiba ya kuzuia utekaji itapatikana siku wananchi wakianza kuchukua sheria mkononi hii ndio italazimisha polisi kutumia njia ya kisheria wanapoenda kumkamata mtu.
 
1 year has passed hii iwe fundisho kwa wanaharakati uchwara
 
1 year has passed hii iwe fundisho kwa wanaharakati uchwara
Mtekaji, baada ya kumuua Mdude ukosoaji umeisha?

Maana hadi ulikua unalilia PM ifunguliwe .

Baada ya kumuua Mdude , Soka , Chaula, Dioniz Kipanya , Polepole je wananchi milioni 70 wote wamegeuka kuwa CCM na kumsifia Samuya?

Baada ya kumuua Mdude ,bima ya afya na matibabu bure imewezekana kwa kila mtanganyika?


Baada ya kumuua Mdude , mfumuko wa bei, upatikanaji wa maji safi pamoja na umeme umefanikiwa kwa 100%

Baada ya kumuua Mdude mmeweza kuboresha elimu ya Tanzania walau ikawa na hadi ya juu kama shule wanazopeleka watoro wao akina Mwigulu?


Ukifanikiwa kujua utekaji na mauaji sio tiba ya matatizo ya Tanzania basi mkitumwa siku nyingine mtakataa.

Halafu nikukumbushe tu jinai haifi, rekodi huwa zipo wenzio kule Kenya walilia kwamba sisi tulitumwa tu , ila sheria haimtetei mtu kupokea amri haramu.

Watch out kuna siku yenu itakuja.
 
Mtekaji, baada ya kumuua Mdude ukosoaji umeisha?

Maana hadi ulikua unalilia PM ifunguliwe .

Baada ya kumuua Mdude , Soka , Chaula, Dioniz Kipanya , Polepole je wananchi milioni 70 wote wamegeuka kuwa CCM na kumsifia Samuya?

Baada ya kumuua Mdude ,bima ya afya na matibabu bure imewezekana kwa kila mtanganyika?


Baada ya kumuua Mdude , mfumuko wa bei, upatikanaji wa maji safi pamoja na umeme umefanikiwa kwa 100%

Baada ya kumuua Mdude mmeweza kuboresha elimu ya Tanzania walau ikawa na hadi ya juu kama shule wanazopeleka watoro wao akina Mwigulu?


Ukifanikiwa kujua utekaji na mauaji sio tiba ya matatizo ya Tanzania basi mkitumwa siku nyingine mtakataa.

Halafu nikukumbushe tu jinai haifi, rekodi huwa zipo wenzio kule Kenya walilia kwamba sisi tulitumwa tu , ila sheria haimtetei mtu kupokea amri haramu.

Watch out kuna siku yenu itakuja.
Leteni chokochoko tena tuwapoteze sasa hivi bado Heche
 
Chokochoko ni kama zipi chawa mtekaji?

Magufuli aliyeasisi "upotezaji " wa watu , yuko wapi saa hizi?
Chokochoko kama kuitisha maandamano nchi nzima kushinikiza mhalifu Lissu aachiwe bila masharti
 
Chokochoko kama kuitisha maandamano nchi nzima kushinikiza mhalifu Lissu aachiwe bila masharti
Wapi kwenye katiba wamezuia maandamano?

Hujui maandamo ni haki ya kikatiba .

The right to assemble and express opinions peacefully is a constitutional right guaranteed under Article 20(1) of the Constitution of the United Republic of Tanzania.

Kasome katiba chawa , katiba hii ina mapungufu mengi ila bado mmezidi kuikanyanga hadi mnaiita " KIJITABU"

Huyo Lissu unayesema ni mhalifu , mmeshindwa nini kuleta ushahiid hadi leo jamhuri inakimbia kuendelea na kesi bila kutaja tarehe na sababu ya kukwama, hujui hilo ila nikueleweshe tu ni ushahidi bandia unaotungwa unagonga mwamba haku a nchi itaendesha kesi ya uhaini taratibu maana uhaini halisi ni tishio kwa nchi hivyo hawatakua tayari kuchelewesha mambo ila kwa hii kesi ya kuchonga ya Lissu ushahidi wao ni video ya YouTube sasa uhaini gani mtu atangaze YouTube?
 
Back
Top Bottom