PreGE2025 Mdude Nyagali adaiwa kukamatwa na kupigwa na watu waliojitambulisha Polisi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mdude sio mkosoaji ni mjinga flan tu asiejielewam mwenyekiti wake maana huwa anaongea as if mdomo na ubongo vimetengana so lazima wamsynchronize. Unaona watu wana silaha na gwanda za polisi wamekuja kukukamata then unaanza kupambana nao. Wao wanaruhusiwaukugonga ukizubaa unavunjwa viungo. Anachokipata ni haki yake
Wewe ni hovyo sana!
 
Hawa watu wanaumiza watanzania wasio na hatia, ina maana usiseme ukiona mtu anaonewa? Huu woga utaendelea mpaka lini? Tuamke watanzania, hao polisi si wengi wa kutunyanyasa hivyo. Tuchukue hatua, tujilinde
Kauli za tishio la uasi kutoka hawa viongozi wa chadema hazipaswi kupuuzwa.
Kama wameamua taifa liingie kwenye machafuko ili mradi wao waingie madarakani,mimi siungi mkono kwani machafuko hayajawahi kuleta suluhu yoyote zaidi ya visasi visivyoisha vizazi na vizazi.
Ni sahihi watu wachache wanaohatarisha usalama wa taifa washughulikiwe kwa kadri ya uhatari wa kauli zao
 
Wewe ni ng'ombe
 
Kauli na vitendo ni vitu viwili tofauti,kama ni kauli uwe ndio vitendo wote tungesema na Kuwa tutakavyo!Acha akili mgando.
 
Mdude sio mkosoaji ni mjinga flan tu asiejielewam mwenyekiti wake maana huwa anaongea as if mdomo na ubongo vimetengana so lazima wamsynchronize. Unaona watu wana silaha na gwanda za polisi wamekuja kukukamata then unaanza kupambana nao. Wao wanaruhusiwaukugonga ukizubaa unavunjwa viungo. Anachokipata ni haki yake
Ovyoo
 
Na hata akili ya kukuongoza kuhisi chochote huna. Nikisema hao watu wanaopotea ni uongo hawapotei, bado utakuwa hujui kinachoelezwa. Sasa wewe ni mtu wa namna gani?
Ahaaa kumbe kweli Polisi wanateka na kupoteza raia.
Vp na kile kikundi cha utekaji alichosema Padri Slaa kuwa kiko ndani ya CDM hakiwezi kuwa kinahusika?
 
Mwanachama wa JF na mdau mkubwa wa mitandao, Mdude_Nyagali amechukuliwa na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi usiku huu.

Walikuwa na silaha, wamevunja mlango.

Mdude amepigwa sana, alikuwa amelala nyumbani kwake Mbeya.

Watu hao wamevamia wakiwa na silaha, wakabomoa mlango, wakampiga sana na wakaondoka naye. Haijafahamika amepelekwa kituo gani cha polisi.

Inadaiwa walibomoa mlango wa nyumbani kwake na kuingia ndani wakiwa na silaha za moto. Watu hao wamempiga na kumvuta chini damu ikimwagika kuelekea pahali kusikojulikana.

Rais wa TLS naye amesema:

Nimepokea habari Usiku huu kwamba Jeshi la polisi Mbeya limefika nyumbani kwa Mdude Mpaluka Nyagali.

Baada ya kufika wamevunja mlango na kuingia ndani na kumpiga wa kitumia vitu mbalimbali na kumjeruhi na baadaye kuondoka naye.

Huu ni muendelezo wa kukithiri kwa vitendo vya wanao onekana wakosoaji wa Serikali kutendewa kinyume cha Sheria na Kuumizwa.

Tunalitaka Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kuhakikisha kuwa Ndugu Mdude Mpaluka Nyagali anakuwa salama na kuhakikisha wanampatia matibabu stahiki.

Tunakemea na kufuatilia jambo hili kwa ukaribu kuona haki ikitendeka.

Boniface A.K Mwabukusi
WAKILI.

View attachment 3322353

*****
MDUDE NYAGALI NI NANI HASA?

View attachment 3322349
​
Mdude_Nyagali , anayejulikana pia kama "Mdude Chadema," ni mwanaharakati wa kisiasa na kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) nchini.

Alizaliwa tarehe 25 Agosti 1987 katika kijiji cha Isongole, Wilaya ya Ileje, mkoa wa Mbeya (sasa Songwe). Tangu mwaka 2008, amekuwa mwanachama wa CHADEMA na amejihusisha na shughuli mbalimbali za kisiasa, ikiwa ni pamoja na kusimamia kampeni za wagombea wa chama hicho.

Mdude amejipatia umaarufu kwa kuwa mkosoaji wa wazi wa serikali kupitia mitandao ya kijamii na majukwaa ya kisiasa. Mara nyingi hujitambulisha kama mpiganiaji wa uhuru wa kujieleza, haki za kiraia na utawala bora.

Mnamo Mei 2019, Mdude alitekwa na watu wasiojulikana kutoka ofisini kwake katika Wilaya ya Mbozi, mkoa wa Songwe. Baada ya siku tano, alikutwa akiwa amejeruhiwa katika kijiji cha Inyala, Mbeya. Alidai kuwa alitekwa kwa sababu za kisiasa kutokana na ukosoaji wake dhidi ya serikali.

Katika maisha yake ya kisiasa, Mdude amekumbana na changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uchochezi na usafirishaji wa dawa za kulevya. Hata hivyo, ameshinda baadhi ya kesi hizo, na mnamo Juni 2021, Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya ilimuachia huru baada ya kumkuta hana hatia katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin.

Usiku wa Mei 2, 2025, taarifa za kukatamatwa kwake zimesambaa kupitia video inayoonekana mtandaoni. Hadi asubuhi hii, hakuna taarifa rasmi zinazoelezea ni wapi alipo pamoja na hali ya afya yake.

--- Jeshi la Polisi likichukua vielelezo eneo la tukio ---
View attachment 3322576View attachment 3322577
​
Pia soma
  1. Pre GE2025 - Martin Masese: Polisi wamefika nyumbani kwa Mdude kuchukua Sampuli ya damu ili waanze uchunguzi
  2. Sakata la kutekwa kwa Mdude, mzee afichua jinsi Polisi walivyomfuata kutaka awasaidie kumfanyia Ujasusi ili wampate
Hivi yupo hai kweli kwa zile damu??
Mungu amsaidie sana kama bado yupo hai.
 
Mimi nitamkumbuka kwa matusi aliyotoa Tabata Baracuda June 01, 2021, siku 3 baada ya kutoka jela kwa msamaha wa Rais Samia. Clip hii hapa:-

Screenshot_20250503_105503_Chrome.jpg

Niliposikia hayo ndiyo nikajuwa kuwa sikio la kufa halisikii dawa. Sishangai kwa yaliyompata
 
Ahaaa kumbe kweli Polisi wanateka na kupoteza raia.
Vp na kile kikundi cha utekaji alichosema Padri Slaa kuwa kiko ndani ya CDM hakiwezi kuwa kinahusika?
Unapouliza swali la aina hiyo, inakuonyesha wazi kuwa upeo wako ni mdogo sana.CDM wawe na kikosi cha kuteka watu, na serikali ishindwe kudhibiti kikosi hicho, huoni kuwa ungekuwa na akili angalau kidogo tu ingekusaidia kutouliza swali la kijinga aina hiyo?
Halafu unamzungumzia Slaa, anashikilia wadhifa gani huko serikalini?
 
Angalau angekuwa hata na watu hapo nyumbani, si imeona mazingira yake lakini sio rafiki kwa Mpigania haki kama yeye. Anaishi mazingira sio salama kwa mtu wa kariba yake. Chadema wanatakiwa wakae waje na mkakati wa kiusalama kwa "Front line human rights defenders" wao angalau wawe na contingency evacuation security plan kwa watu wao.

This is definitely barbaric and uncouth way of dealing with our people.
Inabidi kujilinda kwa kila hali na mali.
 
Huwezi jua ,ila kuna utekaji na upigaji wa aina nasikia uliwahi kutokea huko siku za nyuma na mwisho wa siku wenyewe waliumbuana naona kuna haja kubwa ya Serikali kutumia uchunguzi wa hali ya juu badala ya kuridhika na viashiria tu.
Chadema wanaweza kuwatumia hawahawa polisi wanaweza kutumia hivihivi vyombo vya usalama ,wengine wakipiga makelele kuisakama serikali ,serikali inasahau ile methali ya kikulacho.

Nazani Polisi na vyombo vya uchunguzi vikifanikiwa kuwanasa hawa watekaji wasiojulikana basi wanaowatuma watajulikana na ukweli unaweza kuja juu. Kati ya Chadema na CCM wawili hawa hatakosa mmoja wao au wote kwa pamoja,nilimsikia msemaji wa Chadema hapa mjini Mbeya akisema na wao wanaweza kuwatumia polisi kwa namna wanavyojua wao. Kauli ya kiongozi huyu wa Chadema ilinifanya niunganishe vidoto.
 
Unajua ? Niliwahi kusikia ?

Yaan huna uhakika, mada ishakosa nguvu. Tafuta namna ya kuandika, or kama unaweza achana na ubashiri, tafuta ushahidi
 
Huwezi jua ,ila kuna utekaji na upigaji wa aina nasikia uliwahi kutokea huko siku za nyuma na mwisho wa siku wenyewe waliumbuana naona kuna haja kubwa ya Serikali kutumia uchunguzi wa hali ya juu badala ya kuridhika na viashiria tu.
Kama Chadema wanahusika basi wana watu ambao ni wazuri katika mambo ya intelijensia (ukanzu) kuliko Polisi na TISS. Chadema hawawezi kuwa wanahusika na siku zote hizi TISS au Polisi wasiwe wameukamata mtandao wao wa utekaji na uuaji, labda uniambie TISS na Polisi wa Tanzania ni wazembe wa kwanza duniani

Fanya tukio baya kwa siri uone Polisi watakavyokukamata haraka. Lakini umewahi kusikia wamemkamata hata mtekaji na muuaji mmoja? Unafikiri kwa nini?
 
Huwezi jua ,ila kuna utekaji na upigaji wa aina nasikia uliwahi kutokea huko siku za nyuma na mwisho wa siku wenyewe waliumbuana naona kuna haja kubwa ya Serikali kutumia uchunguzi wa hali ya juu badala ya kuridhika na viashiria tu.
Chadema wanaweza kuwatumia hawahawa polisi wanaweza kutumia hivihivi vyombo vya usalama ,wengine wakipiga makelele kuisakama serikali ,serikali inasahau ile methali ya kikulacho.

Nazani Polisi na vyombo vya uchunguzi vikifanikiwa kuwanasa hawa watekaji wasiojulikana basi wanaowatuma watajulikana na ukweli unaweza kuja juu. Kati ya Chadema na CCM wawili hawa hatakosa mmoja wao au wote kwa pamoja,nilimsikia msemaji wa Chadema hapa mjini Mbeya akisema na wao wanaweza kuwatumia polisi kwa namna wanavyojua wao. Kauli ya kiongozi huyu wa Chadema ilinifanya niunganishe vidoto.
Kama wanahusika nani kawahi kukamatwa na kutiwa hatiani kutoka Chadema kwa matukio hayo ya Utekaji?
 
Ni hoja dhaifu. Kwa jeshi la polisi na vyombo vya uchunguzi itakuwa ni aibu, kama chadema inafanya hivyo na hawakamatwi, itakuwaje akija PAKA?
 
Huwezi jua ,ila kuna utekaji na upigaji wa aina nasikia uliwahi kutokea huko siku za nyuma na mwisho wa siku wenyewe waliumbuana naona kuna haja kubwa ya Serikali kutumia uchunguzi wa hali ya juu badala ya kuridhika na viashiria tu.
Chadema wanaweza kuwatumia hawahawa polisi wanaweza kutumia hivihivi vyombo vya usalama ,wengine wakipiga makelele kuisakama serikali ,serikali inasahau ile methali ya kikulacho.

Nazani Polisi na vyombo vya uchunguzi vikifanikiwa kuwanasa hawa watekaji wasiojulikana basi wanaowatuma watajulikana na ukweli unaweza kuja juu. Kati ya Chadema na CCM wawili hawa hatakosa mmoja wao au wote kwa pamoja,nilimsikia msemaji wa Chadema hapa mjini Mbeya akisema na wao wanaweza kuwatumia polisi kwa namna wanavyojua wao. Kauli ya kiongozi huyu wa Chadema ilinifanya niunganishe vidoto.
Wewe ni mpumbavu.
Unadhani CHADEMA wangehusika wasingekuwa wamekamatwa na polisi wetu wenye intelijensia kubwa?!.
 
Kama wah8sika ni Chadema basibwapewe nchi,maana wana onyeligencia kali kuluko serikali,siku akotekwa mtoto wa kigogo mmoja akili zitakaa sawa
 
Back
Top Bottom