PreGE2025 Mdude Nyagali adaiwa kukamatwa na kupigwa na watu waliojitambulisha Polisi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mwanachama wa JF na mdau mkubwa wa mitandao, Mdude_Nyagali amechukuliwa na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi usiku huu.

Walikuwa na silaha, wamevunja mlango.

Mdude amepigwa sana, alikuwa amelala nyumbani kwake Mbeya.

Watu hao wamevamia wakiwa na silaha, wakabomoa mlango, wakampiga sana na wakaondoka naye. Haijafahamika amepelekwa kituo gani cha polisi.

Inadaiwa walibomoa mlango wa nyumbani kwake na kuingia ndani wakiwa na silaha za moto. Watu hao wamempiga na kumvuta chini damu ikimwagika kuelekea pahali kusikojulikana.

Rais wa TLS naye amesema:

Nimepokea habari Usiku huu kwamba Jeshi la polisi Mbeya limefika nyumbani kwa Mdude Mpaluka Nyagali.

Baada ya kufika wamevunja mlango na kuingia ndani na kumpiga wa kitumia vitu mbalimbali na kumjeruhi na baadaye kuondoka naye.

Huu ni muendelezo wa kukithiri kwa vitendo vya wanao onekana wakosoaji wa Serikali kutendewa kinyume cha Sheria na Kuumizwa.

Tunalitaka Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kuhakikisha kuwa Ndugu Mdude Mpaluka Nyagali anakuwa salama na kuhakikisha wanampatia matibabu stahiki.

Tunakemea na kufuatilia jambo hili kwa ukaribu kuona haki ikitendeka.

Boniface A.K Mwabukusi
WAKILI.

View attachment 3322353

*****
MDUDE NYAGALI NI NANI HASA?

View attachment 3322349
​
Mdude_Nyagali , anayejulikana pia kama "Mdude Chadema," ni mwanaharakati wa kisiasa na kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) nchini.

Alizaliwa tarehe 25 Agosti 1987 katika kijiji cha Isongole, Wilaya ya Ileje, mkoa wa Mbeya (sasa Songwe). Tangu mwaka 2008, amekuwa mwanachama wa CHADEMA na amejihusisha na shughuli mbalimbali za kisiasa, ikiwa ni pamoja na kusimamia kampeni za wagombea wa chama hicho.

Mdude amejipatia umaarufu kwa kuwa mkosoaji wa wazi wa serikali kupitia mitandao ya kijamii na majukwaa ya kisiasa. Mara nyingi hujitambulisha kama mpiganiaji wa uhuru wa kujieleza, haki za kiraia na utawala bora.

Mnamo Mei 2019, Mdude alitekwa na watu wasiojulikana kutoka ofisini kwake katika Wilaya ya Mbozi, mkoa wa Songwe. Baada ya siku tano, alikutwa akiwa amejeruhiwa katika kijiji cha Inyala, Mbeya. Alidai kuwa alitekwa kwa sababu za kisiasa kutokana na ukosoaji wake dhidi ya serikali.

Katika maisha yake ya kisiasa, Mdude amekumbana na changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uchochezi na usafirishaji wa dawa za kulevya. Hata hivyo, ameshinda baadhi ya kesi hizo, na mnamo Juni 2021, Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya ilimuachia huru baada ya kumkuta hana hatia katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin.

Usiku wa Mei 2, 2025, taarifa za kukatamatwa kwake zimesambaa kupitia video inayoonekana mtandaoni. Hadi asubuhi hii, hakuna taarifa rasmi zinazoelezea ni wapi alipo pamoja na hali ya afya yake.

--- Jeshi la Polisi likichukua vielelezo eneo la tukio ---
View attachment 3322576View attachment 3322577
​
Pia soma Pre GE2025 - Martin Masese: Polisi wamefika nyumbani kwa Mdude kuchukua Sampuli ya damu ili waanze uchunguzi
Aseh!!!
 
Mdude sio mkosoaji ni mjinga flan tu asiejielewam mwenyekiti wake maana huwa anaongea as if mdomo na ubongo vimetengana so lazima wamsynchronize. Unaona watu wana silaha na gwanda za polisi wamekuja kukukamata then unaanza kupambana nao. Wao wanaruhusiwaukugonga ukizubaa unavunjwa viungo. Anachokipata ni haki yake
Usimtendee mwenzako kile usichopenda kutendewa
 
Wapenda haki salam..!

Kitendo cha RPC Mbeya kusema hajui alipo MDUDE ni dhahiri wameshafanya yao. Ilitokea hivyo kwa Ben saa nane,Ilitokea hivyo pia kwa SOKA OCD TEMEKE BWANA MOHAMMED alimpigia simu SOKA akachukue pikipiki yake baada ya hapo RPC wa DAR ES SALAAM akakana kumshilia.Mpaka leo tunavyo zungumza MFWELE FAUSTINE AMESHAFANYA YAKE.

Nimeumia sana napanga kulipiza kisasi nikiwa nje ya nchii.
 
ambacho kinashirikiana na jeshi la polisi na kwa udhamini wa ccm
Yawezekana, japo Padri Slaa mwenyewe kama KM hakutaja washirika wa hicho kikundi cha utekaji cha CDM
Unjua Mafwele?
Unawajua Green guard????
Unayajua magari yasiyo na namba za TZ yanayobeba watu wasio na uniform rasmi ila wamebeba silaha za kijeshi??

Soma tena uzi wako alafu unijibu.
Nayajua yote hayo. Mi nlichosema ni kwamba Padri Slaa alitualert kuwa ndani ya CDM kuna kikosi cha utekaji
Wewe uliye na uhakika unajuwa ni akina nani waliomkamata?
Sijui na ndo mana sitaki uzushi. Nasubiri taarifa rasmi.
 
Nimeona video za mke wake akilia kwa uchungu, kwakweli inaumiza sana! Na kwa maelezo yale ni dhahiri walimmaliza hapo hapo sebleni Mungu atusaidie sana hali inatisha!.
 
LOoooh!
Mbona unaendelea kuhoji uhakika wangu wa ninacho andika, lakini wewe mwenyewe huna uhakika na chochote?
Siwezi kusema watekaji kina nani kwa sababu siwajui. Sasa wewe unayewajua tupe uhakika basi. Au na wewe ni mzushi tu
 
Na hata akili ya kukuongoza kuhisi chochote huna. Nikisema hao watu wanaopotea ni uongo hawapotei, bado utakuwa hujui kinachoelezwa. Sasa wewe ni mtu wa namna gani?
 
Mwanachama wa JF na mdau mkubwa wa mitandao, Mdude_Nyagali amechukuliwa na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi usiku huu.

Walikuwa na silaha, wamevunja mlango.

Mdude amepigwa sana, alikuwa amelala nyumbani kwake Mbeya.

Watu hao wamevamia wakiwa na silaha, wakabomoa mlango, wakampiga sana na wakaondoka naye. Haijafahamika amepelekwa kituo gani cha polisi.

Inadaiwa walibomoa mlango wa nyumbani kwake na kuingia ndani wakiwa na silaha za moto. Watu hao wamempiga na kumvuta chini damu ikimwagika kuelekea pahali kusikojulikana.

Rais wa TLS naye amesema:

Nimepokea habari Usiku huu kwamba Jeshi la polisi Mbeya limefika nyumbani kwa Mdude Mpaluka Nyagali.

Baada ya kufika wamevunja mlango na kuingia ndani na kumpiga wa kitumia vitu mbalimbali na kumjeruhi na baadaye kuondoka naye.

Huu ni muendelezo wa kukithiri kwa vitendo vya wanao onekana wakosoaji wa Serikali kutendewa kinyume cha Sheria na Kuumizwa.

Tunalitaka Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kuhakikisha kuwa Ndugu Mdude Mpaluka Nyagali anakuwa salama na kuhakikisha wanampatia matibabu stahiki.

Tunakemea na kufuatilia jambo hili kwa ukaribu kuona haki ikitendeka.

Boniface A.K Mwabukusi
WAKILI.

View attachment 3322353

*****
MDUDE NYAGALI NI NANI HASA?

View attachment 3322349
​
Mdude_Nyagali , anayejulikana pia kama "Mdude Chadema," ni mwanaharakati wa kisiasa na kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) nchini.

Alizaliwa tarehe 25 Agosti 1987 katika kijiji cha Isongole, Wilaya ya Ileje, mkoa wa Mbeya (sasa Songwe). Tangu mwaka 2008, amekuwa mwanachama wa CHADEMA na amejihusisha na shughuli mbalimbali za kisiasa, ikiwa ni pamoja na kusimamia kampeni za wagombea wa chama hicho.

Mdude amejipatia umaarufu kwa kuwa mkosoaji wa wazi wa serikali kupitia mitandao ya kijamii na majukwaa ya kisiasa. Mara nyingi hujitambulisha kama mpiganiaji wa uhuru wa kujieleza, haki za kiraia na utawala bora.

Mnamo Mei 2019, Mdude alitekwa na watu wasiojulikana kutoka ofisini kwake katika Wilaya ya Mbozi, mkoa wa Songwe. Baada ya siku tano, alikutwa akiwa amejeruhiwa katika kijiji cha Inyala, Mbeya. Alidai kuwa alitekwa kwa sababu za kisiasa kutokana na ukosoaji wake dhidi ya serikali.

Katika maisha yake ya kisiasa, Mdude amekumbana na changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uchochezi na usafirishaji wa dawa za kulevya. Hata hivyo, ameshinda baadhi ya kesi hizo, na mnamo Juni 2021, Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya ilimuachia huru baada ya kumkuta hana hatia katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin.

Usiku wa Mei 2, 2025, taarifa za kukatamatwa kwake zimesambaa kupitia video inayoonekana mtandaoni. Hadi asubuhi hii, hakuna taarifa rasmi zinazoelezea ni wapi alipo pamoja na hali ya afya yake.

--- Jeshi la Polisi likichukua vielelezo eneo la tukio ---
View attachment 3322576View attachment 3322577
​
Pia soma
  1. Pre GE2025 - Martin Masese: Polisi wamefika nyumbani kwa Mdude kuchukua Sampuli ya damu ili waanze uchunguzi
  2. Sakata la kutekwa kwa Mdude, mzee afichua jinsi Polisi walivyomfuata kutaka awasaidie kumfanyia Ujasusi ili wampate
Nchi inaumwa ....
 
Ukiunga dots ni kuwa mama ka-change gia angani anaupiga mwingi kwa wakosoaji.

Miaka 30 ijayo CCM ikiwa madaraki niitwe mbwa....kizazi cha CCM wapigania uhuru nikaenda kufa tunabaki hapo vijana tulizozaliwa 90 tunakuwa na miaka 50+ ukomboz upo karibu.

Watoto na wajukuu wa mafisadi mjipange.
 
Back
Top Bottom