PreGE2025 Mdude Nyagali adaiwa kukamatwa na kupigwa na watu waliojitambulisha Polisi

PreGE2025 Mdude Nyagali adaiwa kukamatwa na kupigwa na watu waliojitambulisha Polisi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kama wah8sika ni Chadema basibwapewe nchi,maana wana onyeligencia kali kuluko serikali,siku akotekwa mtoto wa kigogo mmoja akili zitakaa sawa
Inawezekana mpo hapa mmeganda na keyboard na hamfuatilii yaliyopo mjini, Jana msemaje wa Chadema alitamka wanaweza kuwatumia hawahawa polisi na wanaweza kutumia hivihivi vyombo vya usalama.

Sasa kauli hio inasehemu mbili , nionavyo CCM wanatekeleza utekaji (Nao waliwahi kutoa kauli wanaweza ya kuweza na polisi wasifanye lolote) kwa kutumia koti au kujivika upolisi ndio hapo mkuu wa Chadema inaonekana wanaweza kutumia njia hio hio, ....wanavunja na wanadai kuwa wao ni polisi....
 
Siku ya 7 bila Ndugu yetu Mtanzania mwenzetu kupatikana.
 
Kimya SIku ya 19 ,Si TLS Mwabukusi,Si Mwenyekiti wa kanda ,Si wanachadema wakimpambania Sumu ya nyigu....Wanaharakati ndiyo muone kwamba hakuna atakayekupigania sako kwa bako ,aliokuwa anawapambania wote wamekaa kimya sasa wanafanya mambo yao....inayoteseka kwasasa ni familia ya Mdude.
 
Kimya SIku ya 19 ,Si TLS Mwabukusi,Si Mwenyekiti wa kanda ,Si wanachadema wakimpambania Sumu ya nyigu....Wanaharakati ndiyo muone kwamba hakuna atakayekupigania sako kwa bako ,aliokuwa anawapambania wote wamekaa kimya sasa wanafanya mambo yao....inayoteseka kwasasa ni familia ya Mdude.
Wataenda kwa kila mtu na watakuja hadi kwangu... Lakini hayo yote hayana budi kutokea ili maandiko na tabiri za kitambo zitimie!
Wauao kwa upanga watauliwa kwa upanga!
 
Nimeumia sana baada ya kusoma hii post huko twitter
Screenshot_20250522-183016.jpg
 
Hatari Sana!! Tunasubiri kauli ya Mwabukusi.
Upo uku umejificha unasubili kauli ya mwabukusi..
Sasa mwambukusi afanye Nini na yeye ana watoto wanamuita dady,ana familia anapigania tumbo lake na maisha yake mdude anamuhusu Nini.
Achaneni na hizi siasa za uana harakati,kila mnaemuona na kamuamini kule anapambania maslahi yake na tumbo lake.
 
Daaaaaah So Sad aiseeeeee,😕😕

Mwamba hadi dakika hii hajulikani alipo na ni tokea mwezi wa 5 alivyonyakuliwa na ana familia iliyokua inamtegemea.

Ipo siku haya mambo yatajulikana tu waliofanya watatambulika na hata wakifa leo vizazi vyao vitateseka sana.
Rest Easy Bro Mdude!!!
 
Mwanachama wa JF na mdau mkubwa wa mitandao, Mdude_Nyagali amechukuliwa na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi usiku huu.

Walikuwa na silaha, wamevunja mlango.

Mdude amepigwa sana, alikuwa amelala nyumbani kwake Mbeya.

Watu hao wamevamia wakiwa na silaha, wakabomoa mlango, wakampiga sana na wakaondoka naye. Haijafahamika amepelekwa kituo gani cha polisi.

Inadaiwa walibomoa mlango wa nyumbani kwake na kuingia ndani wakiwa na silaha za moto. Watu hao wamempiga na kumvuta chini damu ikimwagika kuelekea pahali kusikojulikana.

Rais wa TLS naye amesema:

Nimepokea habari Usiku huu kwamba Jeshi la polisi Mbeya limefika nyumbani kwa Mdude Mpaluka Nyagali.

Baada ya kufika wamevunja mlango na kuingia ndani na kumpiga wa kitumia vitu mbalimbali na kumjeruhi na baadaye kuondoka naye.

Huu ni muendelezo wa kukithiri kwa vitendo vya wanao onekana wakosoaji wa Serikali kutendewa kinyume cha Sheria na Kuumizwa.

Tunalitaka Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kuhakikisha kuwa Ndugu Mdude Mpaluka Nyagali anakuwa salama na kuhakikisha wanampatia matibabu stahiki.

Tunakemea na kufuatilia jambo hili kwa ukaribu kuona haki ikitendeka.

Boniface A.K Mwabukusi
WAKILI.

View attachment 3322353

*****
MDUDE NYAGALI NI NANI HASA?

View attachment 3322349
​
Mdude_Nyagali , anayejulikana pia kama "Mdude Chadema," ni mwanaharakati wa kisiasa na kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) nchini.

Alizaliwa tarehe 25 Agosti 1987 katika kijiji cha Isongole, Wilaya ya Ileje, mkoa wa Mbeya (sasa Songwe). Tangu mwaka 2008, amekuwa mwanachama wa CHADEMA na amejihusisha na shughuli mbalimbali za kisiasa, ikiwa ni pamoja na kusimamia kampeni za wagombea wa chama hicho.

Mdude amejipatia umaarufu kwa kuwa mkosoaji wa wazi wa serikali kupitia mitandao ya kijamii na majukwaa ya kisiasa. Mara nyingi hujitambulisha kama mpiganiaji wa uhuru wa kujieleza, haki za kiraia na utawala bora.

Mnamo Mei 2019, Mdude alitekwa na watu wasiojulikana kutoka ofisini kwake katika Wilaya ya Mbozi, mkoa wa Songwe. Baada ya siku tano, alikutwa akiwa amejeruhiwa katika kijiji cha Inyala, Mbeya. Alidai kuwa alitekwa kwa sababu za kisiasa kutokana na ukosoaji wake dhidi ya serikali.

Katika maisha yake ya kisiasa, Mdude amekumbana na changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uchochezi na usafirishaji wa dawa za kulevya. Hata hivyo, ameshinda baadhi ya kesi hizo, na mnamo Juni 2021, Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya ilimuachia huru baada ya kumkuta hana hatia katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin.

Usiku wa Mei 2, 2025, taarifa za kukatamatwa kwake zimesambaa kupitia video inayoonekana mtandaoni. Hadi asubuhi hii, hakuna taarifa rasmi zinazoelezea ni wapi alipo pamoja na hali ya afya yake.

--- Jeshi la Polisi likichukua vielelezo eneo la tukio ---
View attachment 3322576View attachment 3322577
​
Pia soma
  1. Pre GE2025 - Martin Masese: Polisi wamefika nyumbani kwa Mdude kuchukua Sampuli ya damu ili waanze uchunguzi
  2. Sakata la kutekwa kwa Mdude, mzee afichua jinsi Polisi walivyomfuata kutaka awasaidie kumfanyia Ujasusi ili wampate
Damu ya huyo Mdude haitawaacha salama.
The fall of CCM 1995-2025.✍️📌
 
Back
Top Bottom