PreGE2025 Mdude Nyagali adaiwa kukamatwa na kupigwa na watu waliojitambulisha Polisi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Huyu jamaa KWA harakati zake hizi alitakiwa awe nje ya nchi kama wakina Kimambi
 
Rais wako amelaani hata kupigwa kwa Kitima? Sasa hapo anachafuliwa na nani kama sio kujichafua?
Aiseee! Nchimbi (mtanganyika) anajitahidi kukemea kauli za hovyo na kujali umoja wa watanganyika. Lakini yeye kimyaaaaa ni kama vile haoni chochote.
 
Mwanachama wa JF na mdau mkubwa wa mitandao, Mdude_Nyagali amechukuliwa na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi usiku huu.

Walikuwa na silaha, wamevunja mlango.

Mdude amepigwa sana, alikuwa amelala nyumbani kwake Mbeya.

Watu hao wamevamia wakiwa na silaha, wakabomoa mlango, wakampiga sana na wakaondoka naye. Haijafahamika amepelekwa kituo gani cha polisi.

Inadaiwa walibomoa mlango wa nyumbani kwake na kuingia ndani wakiwa na silaha za moto. Watu hao wamempiga na kumvuta chini damu ikimwagika kuelekea pahali kusikojulikana.

Rais wa TLS naye amesema:

Nimepokea habari Usiku huu kwamba Jeshi la polisi Mbeya limefika nyumbani kwa Mdude Mpaluka Nyagali.

Baada ya kufika wamevunja mlango na kuingia ndani na kumpiga wa kitumia vitu mbalimbali na kumjeruhi na baadaye kuondoka naye.

Huu ni muendelezo wa kukithiri kwa vitendo vya wanao onekana wakosoaji wa Serikali kutendewa kinyume cha Sheria na Kuumizwa.

Tunalitaka Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kuhakikisha kuwa Ndugu Mdude Mpaluka Nyagali anakuwa salama na kuhakikisha wanampatia matibabu stahiki.

Tunakemea na kufuatilia jambo hili kwa ukaribu kuona haki ikitendeka.

Boniface A.K Mwabukusi
WAKILI.

*****
MDUDE NYAGALI NI NANI HASA?

View attachment 3322349
​
Mdude Nyagali, anayejulikana pia kama "Mdude Chadema," ni mwanaharakati wa kisiasa na kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) nchini.

Alizaliwa tarehe 25 Agosti 1987 katika kijiji cha Isongole, Wilaya ya Ileje, mkoa wa Mbeya (sasa Songwe). Tangu mwaka 2008, amekuwa mwanachama wa CHADEMA na amejihusisha na shughuli mbalimbali za kisiasa, ikiwa ni pamoja na kusimamia kampeni za wagombea wa chama hicho.

Mdude amejipatia umaarufu kwa kuwa mkosoaji wa wazi wa serikali kupitia mitandao ya kijamii na majukwaa ya kisiasa. Mara nyingi hujitambulisha kama mpiganiaji wa uhuru wa kujieleza, haki za kiraia na utawala bora.

Mnamo Mei 2019, Mdude alitekwa na watu wasiojulikana kutoka ofisini kwake katika Wilaya ya Mbozi, mkoa wa Songwe. Baada ya siku tano, alikutwa akiwa amejeruhiwa katika kijiji cha Inyala, Mbeya. Alidai kuwa alitekwa kwa sababu za kisiasa kutokana na ukosoaji wake dhidi ya serikali.

Katika maisha yake ya kisiasa, Mdude amekumbana na changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uchochezi na usafirishaji wa dawa za kulevya. Hata hivyo, ameshinda baadhi ya kesi hizo, na mnamo Juni 2021, Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya ilimuachia huru baada ya kumkuta hana hatia katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin.

Usiku wa Mei 2, 2025, taarifa za kukatamatwa kwake zimesambaa kupitia video inayoonekana mtandaoni. Hadi asubuhi hii, hakuna taarifa rasmi zinazoelezea ni wapi alipo pamoja na hali ya afya yake.
Dah! Hivi Mungu aliumba binadamu wa aina mbili au ni sisi hawahawa😭😭😭😭
 
Mdude hakutakiwa kuishi namna hii, bila ulinzi, bila tahadhari yeyote na bila back-up. Mdude amekuwa target kwa siku nyingi na cold-blood murderers.
CHADEMA wanatakiwa waanzishe na kuimarisha mkakati wa kulinda watu wao, waandae mkakati wa tahadhari. Ukishakuwa mkosoaji kwa utawala kama wetu unakuwa haupo salama.
Kwasasa hilo sio swala la chadema. Ni swala la kila raia wa Tanzania
 
Mdude sio mkosoaji ni mjinga flan tu asiejielewam mwenyekiti wake maana huwa anaongea as if mdomo na ubongo vimetengana so lazima wamsynchronize. Unaona watu wana silaha na gwanda za polisi wamekuja kukukamata then unaanza kupambana nao. Wao wanaruhusiwaukugonga ukizubaa unavunjwa viungo. Anachokipata ni haki yake
Wewe ni mjinga na mpumbavu mkubwa.
Unayofurahia haya ipo siku yarakupata wewe au nugu yako.
Ndipo akili yako iliyojaa kinyesi itatengemaa.
 
Padri Slaa alishasema ndani ya CDM kuna kikosi cha utekaji
Unjua Mafwele?
Unawajua Green guard????
Unayajua magari yasiyo na namba za TZ yanayobeba watu wasio na uniform rasmi ila wamebeba silaha za kijeshi??

Soma tena uzi wako alafu unijibu.
 
Mwanachama wa JF na mdau mkubwa wa mitandao, Mdude_Nyagali amechukuliwa na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi usiku huu.

Walikuwa na silaha, wamevunja mlango.

Mdude amepigwa sana, alikuwa amelala nyumbani kwake Mbeya.

Watu hao wamevamia wakiwa na silaha, wakabomoa mlango, wakampiga sana na wakaondoka naye. Haijafahamika amepelekwa kituo gani cha polisi.

Inadaiwa walibomoa mlango wa nyumbani kwake na kuingia ndani wakiwa na silaha za moto. Watu hao wamempiga na kumvuta chini damu ikimwagika kuelekea pahali kusikojulikana.

Rais wa TLS naye amesema:

Nimepokea habari Usiku huu kwamba Jeshi la polisi Mbeya limefika nyumbani kwa Mdude Mpaluka Nyagali.

Baada ya kufika wamevunja mlango na kuingia ndani na kumpiga wa kitumia vitu mbalimbali na kumjeruhi na baadaye kuondoka naye.

Huu ni muendelezo wa kukithiri kwa vitendo vya wanao onekana wakosoaji wa Serikali kutendewa kinyume cha Sheria na Kuumizwa.

Tunalitaka Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kuhakikisha kuwa Ndugu Mdude Mpaluka Nyagali anakuwa salama na kuhakikisha wanampatia matibabu stahiki.

Tunakemea na kufuatilia jambo hili kwa ukaribu kuona haki ikitendeka.

Boniface A.K Mwabukusi
WAKILI.

View attachment 3322353

*****
MDUDE NYAGALI NI NANI HASA?

View attachment 3322349
​
Mdude_Nyagali , anayejulikana pia kama "Mdude Chadema," ni mwanaharakati wa kisiasa na kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) nchini.

Alizaliwa tarehe 25 Agosti 1987 katika kijiji cha Isongole, Wilaya ya Ileje, mkoa wa Mbeya (sasa Songwe). Tangu mwaka 2008, amekuwa mwanachama wa CHADEMA na amejihusisha na shughuli mbalimbali za kisiasa, ikiwa ni pamoja na kusimamia kampeni za wagombea wa chama hicho.

Mdude amejipatia umaarufu kwa kuwa mkosoaji wa wazi wa serikali kupitia mitandao ya kijamii na majukwaa ya kisiasa. Mara nyingi hujitambulisha kama mpiganiaji wa uhuru wa kujieleza, haki za kiraia na utawala bora.

Mnamo Mei 2019, Mdude alitekwa na watu wasiojulikana kutoka ofisini kwake katika Wilaya ya Mbozi, mkoa wa Songwe. Baada ya siku tano, alikutwa akiwa amejeruhiwa katika kijiji cha Inyala, Mbeya. Alidai kuwa alitekwa kwa sababu za kisiasa kutokana na ukosoaji wake dhidi ya serikali.

Katika maisha yake ya kisiasa, Mdude amekumbana na changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uchochezi na usafirishaji wa dawa za kulevya. Hata hivyo, ameshinda baadhi ya kesi hizo, na mnamo Juni 2021, Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya ilimuachia huru baada ya kumkuta hana hatia katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin.

Usiku wa Mei 2, 2025, taarifa za kukatamatwa kwake zimesambaa kupitia video inayoonekana mtandaoni. Hadi asubuhi hii, hakuna taarifa rasmi zinazoelezea ni wapi alipo pamoja na hali ya afya yake.
Hawa watu wameamua kuua
Sijui kama safari hii jamaa tutamuona tena .
Mungu atie mkono wake yaani mtu anachukuliwa na bunduki usiku
 
Mdude hakutakiwa kuishi namna hii, bila ulinzi, bila tahadhari yeyote na bila back-up. Mdude amekuwa target kwa siku nyingi na cold-blood murderers.
CHADEMA wanatakiwa waanzishe na kuimarisha mkakati wa kulinda watu wao, waandae mkakati wa tahadhari. Ukishakuwa mkosoaji kwa utawala kama wetu unakuwa haupo salama.
Sahihi kabisa.
 
Nguvu kubwa inayotumika kunyamazisha wakosoaji wa serikali wanaitia doa .Rpc Mbeya hakikisha mdude anakuwa salama.
 
Back
Top Bottom