Naumia sana nikimfikiria huyu kijana. Namna alivyochukuliwa na “kupotezwa” inanitia simanzi sana. Bahati mbaya/nzuri nimewahi kumfahamu japo kwa kiasi kidogo, kipindi akiishi Vwawa akiwa na ofisi pembeni ya mgahawa wa Mkulima pale Vwawa.
Kosa lake ni lipi hasa la kustahili aliyotendewa? Kuikosoa serikali? Serikali hii haitakiwi kukosolewa? Wengine watasema alikuwa “akiitukana serikali”. Nchi hii haina sheria? Haina mahakama? Kwanini tunaruhusu kama nchi kuingia kwenye laana ya “kuzima” watu bila hatia. Machozi ya mke wake, watoto wake, ndugu na jamaa wa karibu yanatuachia laana kubwa.
Nauliza, kwahiyo ndio Mdude Nyagali ndio amepotea hivyo? Yaani hivyo tu?