Mdude Nyangali, Wakili Mwabukusi na wenziwe wadaiwa kuundiwa mashtaka ya Uhaini

Mdude Nyangali, Wakili Mwabukusi na wenziwe wadaiwa kuundiwa mashtaka ya Uhaini

Ndio huo wameandika uhaini, lazima file liende kwa DPP ndiye anayetowa kibali cha kesi kwenda mahakamani.
Kwamba ni Uhaini au Uchochezi anayetafsiri ni DPP siyo Polisi

DCI anapeleka Taarifa ya Uchunguzi ikiwa imesheheni data zote zikiwa ghafi

DPP ndio anazitafsiri na kuandaa Hati ya Mashtaka pamoja na Ushahidi na Mashahidi atakaowahitaji mahakamani
 
Tena wachinjwe mchana kweupeeeee watu wakiona, ili iwe fundisho kwa wengine,
Yule mjomba aliwatia virobani walikuwa wapoleee kama maji ya mtungi, ila huyu aliwabembeleza sana, sasa sheria na ifanye kazi yake
Mhaini ni kumhaini tu full stop
Mkuu unaongea kama vile Rais ni Baba yako.
Hahaha
 
si walitaka kuigawa nchi kwa maneno ya uchochezi? kila mchuma janga hula na wa kwaoo
 
Kuna mtego upo hapa, kuwanyima dhamana ni ili kuwaondoa uraiani malengo ya muovu yatimie.
Wameshaona hao jamaa ni kikwazo. Kwamba hata kama ni kesi ya uongo itachukua muda kuisha na jambo lao litatimia.
 
Wameshaona hao jamaa ni kikwazo. Kwamba hata kama ni kesi ya uongo itachukua muda kuisha na jambo lao litatimia.
Hili jambo halitapoa, shetani atambue hilo, hajui kuwakamata hao ameamsha hasira mpaka za wale waliokuwa wamelala.
 
kuhoji ni kusema tutamtoa rais madarakani kwa maandamano yasiyo na mwisho? Hakuna anayewasupport wapumbavu km nyie, tunataka amani na maendeleo siyo watu wa kutuvuruia nchi yetu wakitumiwa na vibaraka vya nje.
😡
 
Hata iweje, hoja zijibiwe

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Swaaaaaafi kabisa! Watanzania hatuwezi kuvumilia treason!
 
Back
Top Bottom