Mechi ya Dar Young Africans vs Mamelodi Sundowns yapewa heshima ya siku ya Mudathir aka Muda Day

Mechi ya Dar Young Africans vs Mamelodi Sundowns yapewa heshima ya siku ya Mudathir aka Muda Day

Timu yenye uwezo wa kutengeneza nafasi nyingi ni ya kuiogopa, saa yoyote chochote kinatokea.
Hapana timu inayoweza kutumia nafasi chache ndio ya kuigopa hiyo, kutengeneza nafasi ni ishu moja na kutumia nafasi ni ishu nyingine. Hadi pale itakavyoweza kuitumia nafasi ipasavyo
 
Kwani kwa kawaida H2H inaanza kuhesabiwa tokea wapi hadi wapi?
Mimi nachojua H2H inaanza kuhesabiwa tokea mara ya mwisho kukutana kurudi chini. Ukitafuta head 2 head za Al Ahly vs Memolod utaona wanaanza kuhesabia game yao ya mwisho kisha ndipo wanarudi nyuma.
H2H huwa inahesabiwa mechi 5 za mwisho timu zilipokutana.

Sasa kwa case ya Mamelody na Ahly ni mechi 14

Wakati Ahly na Simba ni mechi 8

Sasa ukiambiwa katika h2h ya Ahly na Mamelody utoe mechi 6 ili upate ratio ya h2h ya Simba na Ahly, utatoa mechi gani kufanya Mamelody na Ahly wawe na mechi 8 ili kuwa na uwiano sawa na Simba?
 
H2H huwa inahesabiwa mechi 5 za mwisho timu zilipokutan

Sasa mbona unauliza swali ambalo jibu lake unalijua?
Chukua mechi 5 kati ya Al Ahly vs Simba. halafu chukua mechi 5 za mwisho za Al Ahly vs Mamelod fanya comparison ni yupi mbabe wa Al Ahly kwa hivi karibuni. Umeshasema kuwa H2H huwa inahesabiwa mechi 5 za mwisho zilipokutana sasa unazunguka zunguka nini? Jambo lipo wazi tuweke hapa mechi 5 za mwisho kwa kila upande
 
Yanga hatunaga dogo

Tarehe 30th March 2024 ni siku historia ya soka bongo inaenda kuandikwa upya

Mamelodi Sundowns wajipange,

Simu zitapigwa siku hiyo,wajiandae kupokea

Yanga huwa hatubeep,siye tunatwanga tu

Twende kazi
View attachment 2944467
Tatizo mkishahemka humu huwa mnatelekeza post zenu.

Utadhani mpira unachezwa humu Jf.
 
Hapana timu inayoweza kutumia nafasi chache ndio ya kuigopa hiyo, kutengeneza nafasi ni ishu moja na kutumia nafasi ni ishu nyingine. Hadi pale itakavyoweza kuitumia nafasi ipasavyo
Magoli yanatokana na nafasi. Timu kama inatengeneza nafasi chache inamaana mpinzani wake si dhaifu au yeye ni dhaifu.
 
Imagine unashangilia timu ambayo inakoswa koswa dk 90. Unakuwa kwenye hali gani?
Imagine unashangilia timu ambayo ina tengeneza nafasi 10 za magoli na big chances 5 lakini mwisho wa siku mpira unaisha imetoka suluhu je unajisikiaje?
 
Africa hii mbabe wa soka ni nani?

Na anacheza lini?

Afrika hii ni timu gani ambayo katika mechi zote za CAF champion league waliyocheza dhidi ya Al Ahly hajapatikana mbabe?

Simba na Al Ahly wamekutana mara 8

Simba kashinda mechi 3, Al Ahly kashinda mechi 3, mechi 2 zimeenda sare.

Huyo ndio bingwa wa Africa dhidi ya Simba.

Mamelody kakutana na Al Ahly mara 14, kafa mara 5 kasare mara 5 na hizo 4 ndio ushindi wake.

Sasa mpaka hapo ukiambiwa utaje Derby ya Afrika kwenye CAF champion league utataja Al Ahly na timu gani tofauti na Simba?
Hiyo al ahly na Simba ni mechi ya kiande na mbabe.
Kwa akili zako kwa performance ya Simba kwasasa unadhani utamfunga Al ahly??
Pole sana.
Game ya kibabe ni kati ya Mamelodi na Yanga wanakutana wote wajuzi wa mpira.
 
Imagine unashangilia timu ambayo ina tengeneza nafasi 10 za magoli na big chances 5 lakini mwisho wa siku mpira unaisha imetoka suluhu je unajisikiaje?
Kama ni lazima uchague suluhu ya kukoswa koswa na suluhu ya kukosa utachagua kuwa shabiki wa timu ipi?
 
Imagine unashangilia timu ambayo inakoswa koswa dk 90. Unakuwa kwenye hali gani?
Tufanye timu yako A halafu mimi timu B. Mimi timu nayoshangilia inakoswa koswa magoli dakika 90 ila nimeishia kukoswa koswa tu lakini mwenzio timu yangu umepata nafasi moja na hiyo hiyo imekuwa goli. Je yupi atakayeondoka anafuraha kati ya aliyekoswa koswa dakika zote 90 akapata chance moja kamba vs mkosaji kosaji dakika zote 90?
 
Sasa mbona unauliza swali ambalo jibu lake unalijua?
Chukua mechi 5 kati ya Al Ahly vs Simba. halafu chukua mechi 5 za mwisho za Al Ahly vs Mamelod fanya comparison ni yupi mbabe wa Al Ahly kwa hivi karibuni. Umeshasema kuwa H2H huwa inahesabiwa mechi 5 za mwisho zilipokutana sasa unazunguka zunguka nini? Jambo lipo wazi tuweke hapa mechi 5 za mwisho kwa kila upande
Umeelewa concept niliyokuwa naijenga?

Au unaandika kubishana?

Mimi sijakataa kuwa basic ya h2h haiiangalii mechi 5 za mwisho.

Mimi nimezungumzia overall

Ili kuweka balance ionekane Mamelodi kacheza mechi 8 sawa na Simba, ukaambiwa upunguze mechi za Mamelodi kufanya idadi ziwe 8 utapunguza mechi za mwisho au za mwanzoni?

Hili ndio swali
 
Tufanye timu yako A halafu mimi timu B. Mimi timu nayoshangilia inakoswa koswa magoli dakika 90 ila nimeishia kukoswa koswa tu lakini mwenzio timu yangu umepata nafasi moja na hiyo hiyo imekuwa goli. Je yupi atakayeondoka anafuraha kati ya aliyekoswa koswa dakika zote 90 akapata chance moja kamba vs mkosaji kosaji dakika zote 90?
Inakoswa koswa?

Timu yako imeruhusu mabao mangapi kwenye group stage?
 
Tufanye timu yako A halafu mimi timu B. Mimi timu nayoshangilia inakoswa koswa magoli dakika 90 ila nimeishia kukoswa koswa tu lakini mwenzio timu yangu umepata nafasi moja na hiyo hiyo imekuwa goli. Je yupi atakayeondoka anafuraha kati ya aliyekoswa koswa dakika zote 90 akapata chance moja kamba vs mkosaji kosaji dakika zote 90?
Kufungwa kwa aina yoyote hakuna furaha Ila hapa linakuja suala la ubora wa timu hata kama haina bahati. Timu bora ni timu bora saa yoyote inadhihirisha ubora wake.

Timu imecheza vizuri sana, imetengeneza nafasi sana, imekosa magoli sana ni bora kuliko Timu haitengenezi nafasi, imepata nafasi kibahati bahati ikaitumia kupata goli.

Umeshawahi sikia msemo "WAMESHINDA ILA HAWANA AMANI NA TIMU YAO" Mara nyingi huu msemo ni kwa timu inayoshinda kwa kubahatisha, huoni nafasi ikitengenezwa kwa mipango.
 
CAF yote inajua mechi yao bora ni ya Ijumaa.

Na ndio maana wameipa heshima kuwa siku hiyo kutakuwa na mechi moja tu.

Kwanini? Kwasababu ndio Derby ya Africa mpaka sasa.

Al Ahly na Simba hakuna mbabe katika mechi zote walizokutana.

Maana yake ulimwengu mzima kwa siku ya Ijumaa ukiwa unataka kuangalia mechi za CAF, utakuwa unatazama mechi moja tu ya Simba dhidi ya Al Ahly.

Baada ya hapo ndio watafuata wacheza makida kujirusha rusha nao kukamilisha ratiba.
Wacheza makida sio😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom