Yes, ni aibu kubwa mno Taifa limepata!
Hii mechi viongozi wa serikali waliipigia promo ya kununua tiketi, lakini Cha kushangaza uwanja haujafurika kama ilovyotarajiwa!
Cha ajabu na aibu ni mechi kusimamishwa eti kisa taa zimeshindwa kumulika ipasavyo na huku Waziri Mkuu na viongozi waandamizi wa serikali wakiwa uwanjani!
Ikumbukwe siku chache zilizopita Caf walitaka uwanja wa Mkapa irekebishwe ikiwemo taa na maeneo mengine!
Na Hili la taa wenye akili walishaliona mapema kwamba ipo siku kama ya Leo uwanja utakuwa Giza wakati mechi ikiendelea!
Hizi zile tiketi 2000 na hizi fedha za kununulia magoli zisingetosha kutuondolea hii fedheha?
Waziri Mkuu hebu tumbua mtu hapo sasa hivi!