Mechi ya Taifa Stars na Uganda yasimama kwa muda kutokana na taa za uwanjani kupungua mwanga. Taa ziliwaka ikaendelea

Mechi ya Taifa Stars na Uganda yasimama kwa muda kutokana na taa za uwanjani kupungua mwanga. Taa ziliwaka ikaendelea

Ni aibu aisee uko duniani mechi za usiku ni Tamuu kuangalia uwanja safi,mwanga wa kutosha unaweza sema ni mchana huku kwetu sasa TV haiwaki,Mataa yanasinzia sasa iyo VAR itaweza kuendeshwa kweli?

Uwanja upumue
Huu uwanja uko overused aisee.
Shida ni hakuna mwingine kama huo na mwingine kujengwa hadi aje yule mfalme Mohammed wa Morocco
 
Kuna lipaka nimeliona uwanjani pia a.k.a prime minister wa ile nchi😁😁😁
 
Hapo utakuta dokezo la kubadilisha hizo taa ilishaandikwa na kukumbushiwa mara nyingi sana ila wapi!!! Imekaliwa na wanaodhani kuwa taa hazina life span kisa zinawaka.
 
Yes, ni aibu kubwa mno Taifa limepata!

Hii mechi viongozi wa serikali waliipigia promo ya kununua tiketi, lakini Cha kushangaza uwanja haujafurika kama ilovyotarajiwa!

Cha ajabu na aibu ni mechi kusimamishwa eti kisa taa zimeshindwa kumulika ipasavyo na huku Waziri Mkuu na viongozi waandamizi wa serikali wakiwa uwanjani!

Ikumbukwe siku chache zilizopita Caf walitaka uwanja wa Mkapa irekebishwe ikiwemo taa na maeneo mengine!
Na Hili la taa wenye akili walishaliona mapema kwamba ipo siku kama ya Leo uwanja utakuwa Giza wakati mechi ikiendelea!

Hizi zile tiketi 2000 na hizi fedha za kununulia magoli zisingetosha kutuondolea hii fedheha?

Waziri Mkuu hebu tumbua mtu hapo sasa hivi!
 
Benchi la ufundi limevaa black na yellow wakati mwingine watafte jezi inginee
 
Katiba mpya itaondoa wahuni hawa wa galanos huwezi kuiba vyeti halafu uwe waziri wa nishati
 
Ingekuwa ni nchi za wenzetu waziri wa nishati anatakiwa kujiuzulu usiku huuhuu, ila kwa kuwa hakuna utamaduni wa kujiwajibisha poa tu, business as ussual
 
Tunachukuliana poa sana Waafrika. Tunataka standard zetu basi zivumiliwe na wengine, ujinga wetu ubebwe kikawaida na wengine.

Kwa hio ina maana hizo taa hazikuchekia once more, basi hata kuficha aibu katika mechi kubwa ya kihistoria. Yani hata hawakutaka kukagua kila kitu na vile vitu ambavyo walizembea angalau wavichangamkie.

Anyway tushazoeana. Maisha yataenda tu.
 
Back
Top Bottom