Hii tabia ya kusema zile hela zilizofanya hiki si zingefanya hiki muache ni upuuzi na umaskini. Kwani kuna kitu hakitakiwi kufanyika, vipaumbele vyote vinazingatiwa. Wangelipisha kiingilio watu wakakosa kabisa uwanjani bado ungesema kwanini serikali haikutoa hela kulipia kiingilio.
Ndio maana kuna kitu kinaitwa bajeti. Wizara, taasisi, idara, vyombo na kila kitu vina bajeti zao. Serikali ikitoa motisha ya milioni 5 asitokee mtu akaitaka ilipie dawa hospitalini kule Mpwayungu, afya nayo ina bajeti yake.
Huo uwanja ni chawote, mara kwaya mara kukimbia mara singeli sijui vuka kabla hujavuka. Matokeo yake unakuwa chandimu. Nyasi nazo zimeisha na vyoo vichafu siku zote