Mechi ya Yanga dhidi ya Simba, June 25 kuchezeshwa na Waamuzi kutoka Misri

Mechi ya Yanga dhidi ya Simba, June 25 kuchezeshwa na Waamuzi kutoka Misri

Inside10

Platinum Member
Joined
May 20, 2011
Posts
34,776
Reaction score
42,933
Mchezo wa Dabi ya Kariakoo kati ya Yanga SC na Simba SC utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Misri.

Mwamuzi wa kati atakuwa Amin Mohamed Amin Omar, msaidizi namba moja ni Mahmoud Ahmed Abo El Regal, huku msaidizi namba mbili akiwa Samir Gamal Saad Mohamed.

1750686317640.png
Dabi ya Kariakoo kati ya Yanga SC na Simba SC imeahirishwa mara mbili, kwani mchezo huo uliopangwa kufanyika Machi 8, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, na kuahirishwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).

Soma: POSTPONED (PP): Yanga SC VS Simba SC | Ligi Kuu NBC | Benjamin Mkapa Stadium | 08.03.2025

Mechi hiyo ikapangiwa tena kuchezwa tarehe Juni 15, 2025, ikiwa ni mabadiliko ya kwanza ya tarehe tangu kupangwa kwake awali.

Taarifa ya Bodi ya Ligi kuu yaahirisha Mechi ya Derby kati ya Yanga dhidi ya Simba

Baada ya mvutano kuendelea kuhusu Dabi ya Kariakoo, Rais Samia, alikutana na viongozi wa timu ya Simba na Yanga kwa mazungumzo maalum yaliyofanyika Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma.

Soma: Rais Samia akutana na Viongozi wa Simba na Yanga Ikulu, leo Juni 13, 2025

Mara baada ya kikao hicho, ratiba mpya ya mchezo huo ilipangwa rasmi, ambapo Dabi hiyo inayosubiriwa kwa hamu imepangiwa kuchezwa Jumatano, tarehe 25 Juni 2025.

1750685075860.png
 
Waamuzi wa mchezo wa dabi itayofanyika tarehe 25 watangazwa na wote wametokea nje ya nchi uku muamuzi wa kati akiwa kutokea nchini Misri. Orodha yao iyo chini.
Nafikiri hii itakuwa mwanzo mzuri wa kupata fair match isiyokuwa na makosa
 

Attachments

  • becb6bfb-3098-46d4-8606-8ef9b9854be9.jpeg
    becb6bfb-3098-46d4-8606-8ef9b9854be9.jpeg
    151.6 KB · Views: 53
Bado watakosolewa kuwa wanatoka Misri,
ingefaa watoke nchi tofauti ikiwa Mmoja anaongea Kiarabu, Kireno, Kizulu na Kifaransa yaaani iwe ngumu kuwasiliana na kupewa bahasha na wenyeji...
 
Back
Top Bottom