Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 13,417
- 23,310
Sasa hizo stendi ndiyo maendelo wakati watu huko Kazuramimba wanakunywa maji yenye matope. Mtwara watoto hawana madarasa lakusomea, Dar es Salaam hawana madarasa. Vituo vya afya na zahanati havina dawa. Wananchi wa Lindi na Mtwara hawawezi kuuza korosho zao.Wapinzani wa Tanzania wanakasumba mbaya sana. Wao kila jambo ni kukosoa tu.
Wakiona serikali inajenga shule,hospital, barabara au stendi ya mabasi wao ni kukosoa tu.
Nimeshuhudia mabadiliko makubwa sana kwenye miji yetu tangu JPM awe rais.Naweka baadhi ya mifano. Nilishuhudia mkoa wa Singida ukipata stendi mpya ya kisasa iliyogharaimu bil 12 +.
Pia tumeshuhudia stendi mpya ya kisasa jijini Dodoma na soko kubwa la kisasa la Ayubu Ndugai. Stendi mpya ya mabasi ya Magufuli ni ya kutiliwa mfano. Maana ni zaidi ya Johanesburg park station.
Wapinzani tokea JPM aingie madarakani mlikuwa mnakosoa na kumdhihaki kuw ni mzee wa kupenda Megastructures. Je, sasa hamuoni zilivyobadili taswira ya taifa letu? Hamuoni kuwa ni kaendeleo makubwa na miundo mbinu ya kisasa ambayo itaongeza mapato kwa taifa?
My take; Tusipende kukosoa kila kitu,hata mradi wa JNHPP ukikamilika itakuwa ni Megastructure inayotusaidia.
Yaani kujenga vituo vya mabasi na masoko ndiyo kigezo cha maenseleo. Hii ni akili ya KI- Pimbi sana