Mei 7, 1919 Vita ya Kwanza Duniani ilituharibia sana, Tanzania tungekuwa mbali sana

Mei 7, 1919 Vita ya Kwanza Duniani ilituharibia sana, Tanzania tungekuwa mbali sana

kwa ujumla Ujerumani ni watu wenye kufanya vitu kwa malengo ya muda mrefu.
Natumaini nchi au taifa lenye maendeleo makubwa pale ulaya Ujerumani haipungui kuwa ya 3.

Nina ushuhuda mimi binafsi kuna sehemu na fanya kazi, hapo Ujerumani wana uwekezaji wao kupitia jimbo la hamburg vitu wavyofanya, wanavyoleta si vya leo wala kesho bali ni vya kesho kutwa na kuendelea , wao hawana interest yoyote wanayo pata kwa uwekezaji huo bali charity tu.

Mtoa mada umeelezea kitu cha muhimu mno na chenye msingi wa aina yake, kuna tofauti kubwa mno kati ya Uingereza na Ujerumani kwenye swala la maendeleo ya moja kwa moja.
 
Mimi sio mtaalamu wa historia, ila kwa historia yangu ndogo niliyopata O-level ninaamini Tanganyika chini ya Ujerumani ingekuwa Taifa kubwa sana hapa Afrika zaidi ya hapa ilipo leo. Waliotuharibia walikuwa Waingereza waliokabidhiwa taifa leo. Hatukupaswa tuwe marafiki na waingereza. They were hopeless.

Nafikiria jinsi Ujerumani ilivyoendelea. Jinsi wajerumani wanavyofanya kazi kwa bidii. Nafikiria infrastructures walizojenga ambazo hadi sasa zinadumu. Hebu fikiria reli zetu. Hivi Tanganyika leo tungekuwa wapi tungeendelea kutawaliwa na waingereza. Naamini wangetunyorosha akili zetu - Tungekuwa mbali sana kifikra, kiuchumi na tusingekuwa wavivu kama sasa. Hofu yangu kubwa ni labda kukosa uwezo wa kumiliki ardhi. Lakini ardhi ya nini wakati mataifa yenye barafu kama Ukraine na Russia bado tunategemea toka kwao Chakula.

Tukumbuke tu kwamba kabla Ujerumani haijanyang'anywa eneo lake lililohusisha Tanganyika tarehe 7 Mei 1919, na kupewa Uingereza, eneo la maziwa makuu tulikuwa chini ya himaya iliyoitwa German East Africa (GEA) lilokuwa ni eneo linalohusisha nchi za sasa za Tanganyika, Burundi, Rwanda, na sehemu ndogo ya Msumbiji huku makao yake yakiwa Bagamoyo (1885–1890) kisha yakahamia Dar es Salaam (1890–1916) na kwa muda mfupi yakaenda Tabora (1916).

Mwingereza alituharibia sana.
1919 hata Tanzania haikuwepo.mgewezaje kuwa mbali?
 
Huijui Ujerumani wewe. Kaulize kule Namibia na nchi zote ambazo Ujerumani ilitawala, ukimaliza hapo linganisha na nchi zilizotawaliwa na Uingereza tangu mwanzo. Bora Mfaransa kuliko Mjerumani, bora Mwingereza kuliko Mfaransa, kamwe usitawalike na Mbelgiji
 
Nyerere ndie aliyetuharibia Nchi na ndie aliyepanda mbegu za uharibifu.
 
Walitengeneza miundombinu kwa maslahi yao ili kiwarahisishia huduma na sio kwa kutupenda tupate maisha kwa urahisi

Haya leo ni miaka 100 na ushee bado mnawaza maendeleo toka kwao au sisi ndio wajinga tusiojiweza?

Yaani kuna watu wanaamini wameondoka na nyota zetu [emoji1]
Na tujiliwaze kuwa tumerogwa na wazungu
 
kwa ujumla Ujerumani ni watu wenye kufanya vitu kwa malengo ya muda mrefu.
Natumaini nchi au taifa lenye maendeleo makubwa pale ulaya Ujerumani haipungui kuwa ya 3.

Nina ushuhuda mimi binafsi kuna sehemu na fanya kazi, hapo Ujerumani wana uwekezaji wao kupitia jimbo la hamburg vitu wavyofanya, wanavyoleta si vya leo wala kesho bali ni vya kesho kutwa na kuendelea , wao hawana interest yoyote wanayo pata kwa uwekezaji huo bali charity tu.

Mtoa mada umeelezea kitu cha muhimu mno na chenye msingi wa aina yake, kuna tofauti kubwa mno kati ya Uingereza na Ujerumani kwenye swala la maendeleo ya moja kwa moja.
Waingereza sio watu
 
hakuna mkoloni mwenye unafuu wote walikuja Kwa ajili ya Mali ghafi na si kukuboreshea maisha.
Mashule / vyuo , barabara , hospital na mahuduma yote yalianzishwa na mkoloni na hadi leo zinatumika

Mi naona kungekuwa na ufadhali wa maisha ktk nchi za Afrika Kama mkoloni angebaki kutawala
 
Mashule / vyuo , barabara , hospital na mahuduma yote yalianzishwa na mkoloni na hadi leo zinatumika

Mi naona kungekuwa na ufadhali wa maisha ktk nchi za Afrika Kama mkoloni angebaki kutawala
Unapenda sana ukoloni na utumwa ?
 
Habari Yakuwa Wameacha Vito vya Thamani Kubwa Na Kuvificha Sijui uko Mapangoni Na mazindiko Makali Yana Ukweli Wowote?
 
Unapenda sana ukoloni na utumwa ?
Kama itatufanya usiwe jobless , upate huduma za kijamii na kutokua na rushwa bora uwepo

Pale Kilimanjaro Kuna shamba la kahawa la mzungu linalowapa kazi watu zaidi 7000 ,tokea miaka ya utumwa Hadi leo. Najiuliza Kama nikutegemea serikali kungeweka fursa Kama hizi au kuicha jamii ifie mbali
 
Mashule / vyuo , barabara , hospital na mahuduma yote yalianzishwa na mkoloni na hadi leo zinatumika

Mi naona kungekuwa na ufadhali wa maisha ktk nchi za Afrika Kama mkoloni angebaki kutawala
Kiwango cha watu kutokujua kusoma kilikuwaje Tanzania pindi wakoloni walivyoondoka? Na uwiano WA mgawanyo WA huduma za afya ulikuwaje wakati WA ukoloni na baada ya Sisi kujitawala wenyewe.

Tumekuwa kwenye ukoloni Kwa miaka karibu miaka karibu 70, nchi ina miaka 61 tangu uhuru, fananisha maendeleo ya vitu ulivyovitaja Kati ya miaka 70 ya ukoloni, na miaka 61 ya kujitawala.

Fikiria miaka 70 ya ukoloni Tanzania/Tanganyika haikuwahi kuwa na chuo kikuu, hawa watu walikuwa wapo maendeleo yenu au Yao?

Wakoloni kama wangebaki jamii ya wazawa ingekuwa maskini halafu mazalia ya wajerumani au uingereza ndio wangekuwa wanaimiliki ardhi karibia yote kama inavyotokea Afrika kusini, Zimbabwe na Botswana.
 
Kama itatufanya usiwe jobless , upate huduma za kijamii na kutokua na rushwa bora uwepo

Pale Kilimanjaro Kuna shamba la kahawa la mzungu linalowapa kazi watu zaidi 7000 ,tokea miaka ya utumwa Hadi leo. Najiuliza Kama nikutegemea serikali kungeweka fursa Kama hizi au kuicha jamii ifie mbali
Jibu swali unapenda ukoloni na utumwa ?
(a) Ndio 
(b)  Hapana
 
Back
Top Bottom