Japan, South Korea, Philippines wangechagua upande wa China.
Haya mataifa ya Asia kama China, S.K, Japan, N.K, India n.k halafu imagine na Russia nayo iwe upande wao
Yangekuwa kitu kimoja Marekani hasingekuwa na influence eneo la Indo-Pacific na kungekuwa na balance of power kwenye huo ukanda.
Kukiwa na balance of power inachangia sana amani na utulivu duniani
Na Marekani anajua kuwa hayo mataifa kiuchumi, kiteknolojia, kijeshi yakiungana ushawishi wake upande wa Indo-Pacific lazima upotee
Ndio maana anafanya juu chini kupandikiza uadui hasa kati ya mataifa hayo na China na anataka kuyatumia to containing China's influence in Indo-Pacific region
Kabla ya influence ya Marekani hapo Indo-Pacific kulitokea haya:
1. Urusi na Japan zilipigana mwaka 1904 na mpaka sasa bado zinagombea Kuril Islands. Muda wowote zitapigana bila influence ya US, ndio akisuruhisha vita iishe.
2. Japan iliiteka Manchuria ya China, ikaipiga Ufilipino na kufanya mauaji na ubakaji Korea. Wote hao hawaipendi na hawawezi ungana nayo.
3. China iligombea na mpaka sasa inabishana mipaka na kila jirani. Inabishana bahari na Japan na Ufilipino. Hao wote hawawezi ungana nayo. China inaidai Urusi eneo lake, hadi huu mji wa Vladivostok ni eneo la China lile. Muda wowote Wachina wakiamua Warusi watakiona cha mtemakuni. Watu ambacho hawajui ni kuwa ni rahisi China kupigana na Urusi kuliko kupigana na Marekani, kwanza walipigana mwaka 1969.
Mwaka 1964 Wachina waliamua kufanya review ya mipaka yao na kulitaka eneo lao la Urusi, mazungumzo kwa miaka mitano yakafeli wakapigana kimyakimya mipakani. Sasa imagine China wanafanya review tena. Kwa upande wa Marekani, China hawadaiani chochote hivyo wanaweza wasiingiliane maslahi na wasipigane.
4. China inagombana na India eneo la Ladakh. Hao nao unataka eti waungane dhidi ya Marekani. Wakati China inaungana na Pakistan kwenye ugomvi na India.
************
Huyo Australia ni mshirika wa Uingereza na Marekani. Hawezi achana na watu anaojua na waliotoka mbali wakisaidiana eti ashirikiane na Wachina wanaogombana na kila jirani yao.
Hata China yenyewe ilipokea misaada ya Marekani kwa airlift kupitia milima ya Himalaya. Airlift ngumu ya jeshi la anga la Marekani kuwahi kutokea hadi leo, ndege zaidi ya 500 za Marekani zilidondoka milimani kwa tufani, ukungu, kugonga safu za milima, mvua kali, dhoruba na usumbufu wote wa ile milima. US ilipoteza marubani na wanaanga zaidi ya 1,000 kwa ajili ya China kujikomboa dhidi ya Japan.
Hapo Korea ni Marekani iliingilia kati Warusi wasiiteke nchi nzima. Hatimaye zikatokea nchi mbili, iliyowahi tekwa na Urusi unaiona hadi sasa ilivyo.
********
Kwahiyo hao Asians usidhani ni wapumbavu hawajui kuchagua, hakuna mwendawazimu atachagua kushirikiana na China kijeshi wakati lengo la China ni expansionism na kudaiana maeneo na kila jirani.