Muda mfupi uliopita kiongozi wa wanamgambo wa Houth wa nchini Yemen wameteka meli yenye bendera ya Israel kusini mwa bahari nyekundu iliyokuwa ikielekea bahari ya mediteranean.
Kiongozi wa Houth amethibitisha hilo na kusema ni katika juhudi zao za kupambana na Israel inayoua watoto na akinamama huko Gaza,
Kabla ya leo wanamgambo hao wamewahi kurusha makombora kuelekea kusini ya Israel kwa lengo hilo hilo.
Hilo lemetokea leo wakati makombora kadhaa yamerushwa kwa mara nyengine katikati ya Israel kutoka Gaza na ambako mapigano makali yameripotiwa huko kaskazini ya eneo la Gaza.
Chanzo ni mtandao wa Aljazeera.
Habari zaidi tutawaletea baadae.