Tetesi: Membe awakatalia Kardinali Pengo na Askofu Malasusa kumsamehe Musiba

Mm mkatoliki ila huyo Pengo ni mnafiki sana kipindi Cha Magufuri alikuwa anarambishwa asali na alikuwa kimya tu Leo anataka kumuokoa mtu waliyekuwa wanaramba asali wote.

Membe shikilia hapo hapo mpaka nyani ateme bungo.
 
Askofu Pengo na Malasusa walikuwa karibu sana na JPM hivyo kujiingiza kwao kumuombea msamaha huyu mhalifu Musiba kunadhihirisha dhahiri kuwa Musiba alikuwa anatumwa na rafiki yao JPM na walikuwa wanajua.
Hii ni aibu kubwa kwao na wanaliaibisha kanisa kwa kushirikiana na uovu
 
Musiba ni mtu mwenye kiburi kupindukia.

Kupigwa mbada mali zake zote ni jambo jema kabisa kwa nia ya kuwafunza watu wengine wenye tabua kama zake au wale ambao wangekuja kuwa na tabia kama za kwake.

Madam adhabu haijahusisha kuundoa uhai wake, ni jambo jema.

Viongozi wa dini, nao wasitumie nafasi zao kuulinda uovu. Wakati Musiba akitukana watu na kuhamasisha baadhi ya watu wauawe, Askofu Mkuu Pengo na Askofu Malasusa walikuwa wapi? Walitoa kauli gani?

Wakati watu wanauawa, wanapotezwa, wanatekwa na kudhulumiwa mali zao, Maaskofu wa Kanisa Katoliki waliandika waraka kulaani matukio hayo, lakini jambo la ajabu Kadinali Pengo aliukana waraka ule na kudai yeye si sehemu ya azimio lile, na wala sahihi kwenye waraka ule siyo ya kwake. Yote hayo ilikuwa kwaajili ya kutomkera mtawala aliyekuwa akiufadhili uovu.

Hayo ya nyuma yaliishapita, tuliishayasamehe. Kadili Pengo ni vema akapumzika, asijiingize katika mambo haya. Nchi hii inahitajika kujengwa upya, japo ujenzi wake unaenda taratibu mno. Upatikanaji wa Katiba ulkohitajika kuwa kipaumbele cha kwanza, unapelekwa kwa danadana na hadithi nyingi bila vitendo.
 
Membe itakua kafulia anataka hela hakuna kingine hapo nimemshtukia.
Hizo mali ziwekwe wazi mahali zilipo. Hilo shamba kama lipo maeneo ya karibu na mjini, ninalihitaji. Nikilinunua nitaligawa kwa kwa taasisi za dini wajenge sehemu ya kuabudia, au kwa wanaotaka kujenga kituo cha kulelea watoto yatima, au eneo la wazi kwa vijana wasio na ajira wafanyie shughuli zao hapo.
 
Hahaaa..... wapambe mmeshindwa kumchangua shujaa wenu msiba?

Yuko mwingine alisingizia watu madawa ya kulevya.

Kesi zake zitafunguliwa hata baada ya miak 30 mbele. Ajiandae tu.
Kila siku watu wanarekebisha miandiko kwenye documents tu. Siku miandiko ikikaa sawa hatoboi
 
Kwa nini haku appeal mpaka case ifike mahama za EAC, yaani yeye angeenda na mwendo wa ku apeal tu!
Sidhani kama hii case ilifika kwenye Mahakama ya Rufaa!
Well I’m just curious [emoji3166]
Hakuwa na sababu ya ku-appeal akiamini wale maafisa wa TISS ambao marehemu aliwapa ujaji wangetoa hukumu ya kumlinda kama ilivyokuwa inafanyika wakati marehemu akiwa hai.
 
Umeandika utumbo tu.
 
Huyo mzee kafulia mpaka anasikitisha.

Sasa kuuza mali za musiba ndio kutamtoa kwenye ukata.
Kamchangie Musiba. Kumsema vibaya mwenye haki hakuzuii haki yake. Njia mojawapo ya kumchangia, wakati wanapiga mnada apartments zake, unanunua mojawapo. Halafu unamrudishia Musiba ila ibakie kwenye jina lako, la sivyo pesa isupokamilika, ndani ya miaka 10 kunaweza kufanyika mnada mwingine wa vitu vingine alivyo chuma tena.
 
Kuuliza Sio ujinga, hizo mali zote zinazotangazwa kupigwa mnada zina hati? Kama zina hati je zote zimeandika Majina yake au kuna zenye Majina ya mke na Watoto?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…