Uchaguzi 2020 Membe: Kamati Kuu haina mamlaka ya kunifukuza Uanachama wa CCM bali Halmashauri Kuu ya Taifa. Asema kati ya Juni na Oktoba chochote kinaweza tokea

Why now? Kwa nini disturbing the piece now? Utaratibu wa zamani wa chama ulikuwaje? Mkapa walichukua form? Kikwete walichukua form? Membe nae anajua utaratibu wa sisiemu hii, na kubadilihwa kwa huo utaratibu sio muda huu....
Unaweza ukawa ndo mwanzo na ikaendelea hivyo. Ndo kukua kwa demokrasia. Hata walivyoanza vyama vingi wangeuliza why now ?Leo kusingekuwa na vyama vingi. Jambo lolote linaloleta kukua kwa demokrasia ni jambo zuri. Na kama Magu anakubalika why mnaogopa ?Si atamshinda Membe asubuhi tu ?
 
Kwa ndani ya sisiemu hamna hofu yoyote ya Membe sababu hatoteuliwa kuwa mgombea kupitia sisiemu, suala ni why disturbing the piece sasa wakati kuna stability tayari? Hata huko wanakosema ndio baba wa demokrasi kwa kina trump na uk ktk second term mara nyingi nao wanakwepa vitu kama hivi, wa term ya kwanza anadunda automatic selection kuwa mgombea term ya pili, term ya pili sio ishu ya demokrasi ni ishu ya maintaining stability of the status quo...
 
Membe achukue,kura zipigwe. Stability itakuwepo.Tanzania ipo stable hata Magu akishindwa.
 
Huyu barafuyamoto ni mtu ambae siku zote mimi na yeye huwa tunakinzani kimawazo na kimisimamo hapa JF yeye aikionekana kuwa ni mtu anaeunga mkono CCM na mimi nikiwa ni mtu naeunga mkono upinzani.

Hata hivyo,kwa mshangao mkubwa leo hii mimi na yeye tumewaza kitu kile kile kwa asilimia 100 jambo ambalo linenifanya nijiulize kama hii imetokea tu kwa bahati au vinginevyo ila nimekuja ku-conlude kuwa haya yatakuwa maono na hiki huenda ndio kinaweza kuja kutokea hapo baadae kabla ya Oktoba mwaka huu.

Ni hivi:Baada ya kuisikiliza clip ya Membe,ndani ya muda mfupi tu nikapata wazo kuwa Membe atahamia ACT-Wazalendo na atateuliwa kuwa mgombea na watachofanya CHADEMA ni kutosimamisha mgombe(watacheza mchezo wa kisiasa) alafu waje wamuunge mkono Membe na lengo ni wao kukwepa kurudia kosa kama lile la kumsimamisha Lowassa(hawatataka kuonekana wanachakuwa tena wagombea kutoka CCM hasa kwa ngazi ya uraisi).

Hivyo ndivyo nilivyowaza, ila kwa mshangao mkubwa, nimekuta na huyu member barafuyamoto nae kawaza kama mimi kwa asilimia 100 ingawa mimi nilienda mbali zaidi kwa kuwaza/kuamini watachofanya CHADEMA ni kumsimamisha Lissu alafu baadae Lissu atajitoa kwa kuhofia usalama wake na hatarudi nchini na mchezo huo wa kisiasa utakuwa umekamilika na CHADEMA wataamunga mkono Membe.

Najua yako yanayosemwa kuhusu Lissu kufanyiwa mizengwe kwenye uteuzi ila hizi zote zinaweza kuwa ni siasa tu zenye malengo fulani.

Tusubiri.

Maoni yangu:
Mimi kama mwananchi wa kawaida,nawashauri wapinzani wasirudie kosa la kumsimamisha mgombe yoyote aliekataliwa,kufukuzwa au kujiondoa CCM katika uchaguzi huu, hasa kwa nafasi ya uraisi, kwani wananchi teyari wana majereha katika mioyo yao hivyo kurudia kosa kama hili kupitia chama chochote cha upinzani ni kutonesha vidonda hivi na zaidi ni kukaribisha hatari ya vyama vya upinzani kudharauliwa, kupuuzwa na hata kukataliwa na wapiga kura na madhara mengine ni hali hii kuwakatisha tamaa wananchi wengi na kuwafanya wasijitokeze kwenye kupiga kura.

Hata Nyalandu nawashauri msimpitishe kuwa mgombea kwasababu hizi hizi nilizozitaja.
 
Membe bana ....furahisha baraza hii [emoji41]
 
Pumbavu sana. Basi mruhusu demokrasia achukue fomu ili akajipime na Mtukufu na KUNOGESHA uchaguzi, shida ni nini wana CCM wenzangu?
Inajulikana pote, Membe ndiye Mgombea Urais kupitia CCM, ni suala la muda tu.
Hata Mh. Lowasa wafuasi wake aliwaaminisha hivyo hivyo ila kwa sasa wewe mwenyewe anajua
 
Vita za kijasusi hazitabiriki. Ila inategemea nani yupo smart na anauwezo kiasi gani. Up to this moment hii ni vita mbaya sana kutokea ndani ya ccm na itatikisa chama as I told ye on last thread ccm kutikisika. Japo iman yetu kuna ushindi
Mgawanyiko mkubwa ulikuwa enzi za JK sio sasa. Hii furahisha baraza na tutarudi hapa baada ya Oct na stori za malalamiko ya kushindwa.
 
Siyo utaratibu rasmi, ndo maana John Shibuda alichukua fomu kuchuana na Kikwete kwenye muhula wake wa pili..
 
Membe akagombee Cuf au Nccr sisi chadema atutaki wapuuzi.


Kwanini unasema hivyo?

Jamaa siyo wa kumpuuza kihivyo.

Chama atakachoshiriki kitapata faida kuliko kumkosa.

Kwanza atakuja na wanachama wapya wengi

Pili itapelekea nguvu ktk kuchagua wabunge na madiwani wa chama husika cha upinzani.

N.k

Chama chochote atakachogombea kitapeleka value addition nakuambia.

Tafakari
 



Chadema inajitosheleza kila kitu
 
Kwa nini huja coment kwenye thread au post yake hiyo?

Au ndo mpaka uanzishe thread yako ili uonekane!
Huu mgongano wa kimawazo wa kiwango hiki ndio umenishitua na kunipa nguvu ya kuanzisha huu uzi ingawa nilitaka kuanzisha tangu mwanzo ila nikaamua kupotezea ila sasa ndio nimepata nguvu ya ku-share hii idea baada ya kuona kuna mtu mwingine kawaza kama mimi kwa asilimia 100.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…