Huyu
barafuyamoto ni mtu ambae siku zote mimi na yeye huwa tunakinzani kimawazo na kimisimamo hapa JF yeye aikionekana kuwa ni mtu anaeunga mkono CCM na mimi nikiwa ni mtu naeunga mkono upinzani.
Hata hivyo,kwa mshangao mkubwa leo hii mimi na yeye tumewaza kitu kile kile kwa asilimia 100 jambo ambalo linenifanya nijiulize kama hii imetokea tu kwa bahati au vinginevyo ila nimekuja ku-conlude kuwa haya yatakuwa maono na hiki huenda ndio kinaweza kuja kutokea hapo baadae kabla ya Oktoba mwaka huu.
Ni hivi:Baada ya kuisikiliza clip ya Membe,ndani ya muda mfupi tu nikapata wazo kuwa Membe atahamia ACT-Wazalendo na atateuliwa kuwa mgombea na watachofanya CHADEMA ni kutosimamisha mgombe(watacheza mchezo wa kisiasa) alafu waje wamuunge mkono Membe na lengo ni wao kukwepa kurudia kosa kama lile la kumsimamisha Lowassa(hawatataka kuonekana wanachakuwa tena wagombea kutoka CCM hasa kwa ngazi ya uraisi).
Hivyo ndivyo nilivyowaza, ila kwa mshangao mkubwa, nimekuta na huyu member
barafuyamoto nae kawaza kama mimi kwa asilimia 100 ingawa mimi nilienda mbali zaidi kwa kuwaza/kuamini watachofanya CHADEMA ni kumsimamisha Lissu alafu baadae Lissu atajitoa kwa kuhofia usalama wake na hatarudi nchini na mchezo huo wa kisiasa utakuwa umekamilika na CHADEMA wataamunga mkono Membe.
Najua yako yanayosemwa kuhusu Lissu kufanyiwa mizengwe kwenye uteuzi ila hizi zote zinaweza kuwa ni siasa tu zenye malengo fulani.
Tusubiri.
Maoni yangu:
Mimi kama mwananchi wa kawaida,nawashauri wapinzani wasirudie kosa la kumsimamisha mgombe yoyote aliekataliwa,kufukuzwa au kujiondoa CCM katika uchaguzi huu, hasa kwa nafasi ya uraisi, kwani wananchi teyari wana majereha katika mioyo yao hivyo kurudia kosa kama hili kupitia chama chochote cha upinzani ni kutonesha vidonda hivi na zaidi ni kukaribisha hatari ya vyama vya upinzani kudharauliwa, kupuuzwa na hata kukataliwa na wapiga kura na madhara mengine ni hali hii kuwakatisha tamaa wananchi wengi na kuwafanya wasijitokeze kwenye kupiga kura.
Hata Nyalandu nawashauri msimpitishe kuwa mgombea kwasababu hizi hizi nilizozitaja.