Uchaguzi 2020 Membe: Kamati Kuu haina mamlaka ya kunifukuza Uanachama wa CCM bali Halmashauri Kuu ya Taifa. Asema kati ya Juni na Oktoba chochote kinaweza tokea

Uchaguzi 2020 Membe: Kamati Kuu haina mamlaka ya kunifukuza Uanachama wa CCM bali Halmashauri Kuu ya Taifa. Asema kati ya Juni na Oktoba chochote kinaweza tokea

Wanasiasa hawana msimamo,Membe alipokuwa kwenye awamu iliyopita alikuwa hazungumzii tume huru ,sasa yupo nje ya mchezo anadai tume huru
 
Labda anaenda kuchukua copy lakin najiuliza Copy yenyewe ataipata wapi? Maana nahisi iliyochukuliwa tayari ilishajazwa baadhi ya vipengele. Hahahaha!! Kazi kweli kweli!!!
 
Wewe unafikiri inawezekana mkuu?
Vita za kijasusi hazitabiriki. Ila inategemea nani yupo smart na anauwezo kiasi gani. Up to this moment hii ni vita mbaya sana kutokea ndani ya ccm na itatikisa chama as I told ye on last thread ccm kutikisika. Japo iman yetu kuna ushindi
 
Anaweza kuitwa kwa mashauriano au kutekwa wakati wowote licha ya ukweli kuwa hata hiyo form hawezi kupewa kwa maagizo ya Jiwe.
Lazima utambue kuwa huyo Membe ana "backup" nzito sana nyuma yake.......

Wewe jiulize anaewezaje kujiamini kiasi kikubwa hivyo hadi atamke maneno hayo?

Vile vile tusisahau kuwa yeye Membe mini jasusi mbobezi, inayompa confidence ya kutamka maneno hayo bila kuogopa chochote!
 
“Reporters think they control the story, but always the story control the reporters” (George Edwoods)
 
Vita za kijasusi hazitabiriki. Ila inategemea nani yupo smart na anauwezo kiasi gani. Up to this moment hii ni vita mbaya sana kutokea ndani ya ccm na itatikisa chama as I told ye on last thread ccm kutikisika. Japo iman yetu kuna ushindi
Mkuu that will never happen kwa CCM. CCM ni mfumo, ina think tank kubwa sana. Mpaka sasa walishafanya analysis ya threat ya Membe na wanajua mwisho wake ambao ni kuomba msamaha. Sema anachokifanya kwa sasa ni kutengeneza vuguvugu ili 2025 asisahaurike, wenye akili wala hawahangaiki naye.
 
Watu wengi wanaichukulia CCM poa, lakini hawafahamu wamekuwepo hapo tangu uhuru wa Tanzania na sio tu wapo wapo kama wengi wanavyofikiria Wanatekeleza yale ambayo wanasema na kuamua. Kwa yanayotokea kwenye vyama vingine itachukua muda mrefu sana kupata ridhaa ya Watanzania. Mfano mzuri ni utekelezaji wa sera zao chini ya JPM. Hata mataifa ambayo yanaipinga Tanzania yanaona aibu kwa yale ambayo yametelekezwa katika kipindi hiki cha miaka 5.

Ikumbukwe Kamelius Membe ni moja kati ya mawaziri wa mambo ya nje aliyepwaya sana pamoja na Jakaya, ni watu ambao hadithi zilikuwa nyingi bila utekelezaji. Hivi Membe alifanya nini cha maana alipokuwa Waziri? Najaribu kukumbuka tu lakini sioni lolote zaidi ya maloloso. Labda aje hapa atwambie, Watanzania waliteleza tu baada ya Alhaji Mwinyi na Che-Nkapa. I hope it will never happen again.
 
Huo urais aende akagombee chadema au ACT lakini sio CCM na haita kuja itokee membe awe rais wa tanzania ,hana vigezo wala hata nusu ya kumfikia Dr. Magufuli hakuna wa kumpinga magufuli ndani ya CCM. Over.
Kwanini hakuna wa kumpinga Magufuli ndani ya CCM? Je! Ni urais alionao sasa au uenyekiti wa CCM?
 
Membe kwa sasa hana ujasusi huo,na majasusi wengi wapo kwenye system ya sasa atapata support wapi
Vita za kijasusi hazitabiriki. Ila inategemea nani yupo smart na anauwezo kiasi gani. Up to this moment hii ni vita mbaya sana kutokea ndani ya ccm na itatikisa chama as I told ye on last thread ccm kutikisika. Japo iman yetu kuna ushindi
 
Kwanini asifukuzwe kama anasumbua,wameshindwa kumfukuza
Mkuu that will never happen kwa CCM. CCM ni mfumo, ina think tank kubwa sana. Mpaka sasa walishafanya analysis ya threat ya Membe na wanajua mwisho wake ambao ni kuomba msamaha. Sema anachokifanya kwa sasa ni kutengeneza vuguvugu ili 2025 asisahaurike, wenye akili wala hawahangaiki naye.
 
Naona Role model ameamua kufafanua kidogo..
20200621_104624.jpeg
 
Membe anasema:

Nimetafakari wito wa Watanzania. Mchakato wa Uchaguzi ulipoanza sikuamini tungefanya uchaguzi kutokana na hali ya Corona. Nilitarajia ungefanywa uchambuzi mkubwa sana kabla ya kuamua kuingia kwenye uchaguzi katika mazingira haya.

Nilihoji, tunaweza kwenda kwenye Uchaguzi bila Tume Huru ya Uchaguzi? Jibu likawa – tuwe na Tume Huru. Lakini, safari hii Waangalizi wa Uchaguzi wa Kimataifa hawatakuwepo. Je, tuko tayari kuwa na Uchaguzi usio na waangalizi wa Kimataifa?

Kuhusu kugombea ndani ya CCM:

Tumefikia uamuzi kuwa sisi hatujamkosea mtu, hatujawa wahalifu, na hatuna uoga na tunajiamini. Tunayo haki kabisa ya kugombea Urais kwakuwa tunalindwa na Katiba na si utamaduni. Tunamheshimu Mwenyekiti na tunaiheshimu Kamati Kuu. Walichokisema kilikuwa ni mapendekezo na yatafanyiwa kazi na Halmashauri Kuu ya Taifa ambayo itafanyika mwezi Julai. Chombo kinachotoa adhabu ndani ya CCM ni Halmashauri Kuu ya Taifa; bahati mbaya Kamati Kuu wao walitamka kuwa “Membe tumemfukuza” na hawana mamlaka hayo.

Kamati Kuu ya CCM inaweza ikakataa, ikasema tulichoamua – tumeamua… Inaweza kabisa ikakataa! Ikikataa, sitoweza kwenda Dodoma kuchukua fomu. Kunikataa mimi kugombea ndani ya CCM, Uchaguzi haunogi. Mimi sitakwenda Dodoma mpaka Kamati Kuu itakaponiambia kuwa nipo huru kufanya hivyo, siko tayari kuingia kwenye mtego. Lazima tupate ridhaa!

Nisipopata ridhaa, tunakitakia chama chetu kila la heri. Uchaguzi ni Oktoba, sasa ni Juni… Chochote kinaweza kutokea hapa katikati. Nawaomba vijana tulieni, msilete ghasia zozote. Hatujui Mungu alichotupangia, tusitoe hukumu mapema! Tuwe na imani, yote tumwachie Mwenyezi Mungu.

Video hii hapa:


View attachment 1484912
Nimeisikiliza speech yake kimsingi hana jipya wala la maana naona anajifariji tu na watoto wake walio mzunguka kumpigia makofi
 
Wanabodi,

Benard Membe amesema bado anajishauri kama agombee kumpinga Magufuli sio ili ashinde uchaguzi bali kuunogesha tuu uchaguzi.

Trend hii imepatikana kwa kumsikiliza Membe kwa kutumia analytical listening in between the words, na kubaini kitu kilicho moyoni kwa msemaji japo hajakizungumza expressly but impliedly kupitia matamshi yake.

Time will tell.

Nawatakia Jumapili Njema.

P
Labda kama kuna video nyingine,ila kwa hii uliyoisikiliza wewe mhh.

Anaiheshimu kamati kuu,anaisubiri itoe tamko ama hata kiongozi mmoja wa hiyo kamati kuu..akisema yupo huru basi ataenda kuchukua fomu.

Vinginevyo kamati kuu/kiongozi wake wakikaa kimya Membe hachukui fomu. Huo ni mtego.

Uchaguzi unanoga panapokuwa na ushindani,uwepo wake utafanya unoge zaidi..si unakumbuka ulipoweka kambi kwa Lowassa. Zile raha za mshikemshike..ndo kunogesha kwenyewe.

Ila huyu jamaa pengine anavitu ambavyo wengi hatuvijui.

Hotuba yake hii inahitaji kufanyiwa critical analysis hasa na vyombo vya usalama.

Inanikumbusha hotuba za Osama Bin Laden,ikulu ya marekani haikuwahi kuzipuuza. Zilichambuliwa in detailed.

Membe sio wa kumpuuza hata kidogo.

June-Oct lolote lile litatokea,tuwe wapole.
 
Back
Top Bottom