Membe anasema:
Nimetafakari wito wa Watanzania. Mchakato wa Uchaguzi ulipoanza sikuamini tungefanya uchaguzi kutokana na hali ya Corona. Nilitarajia ungefanywa uchambuzi mkubwa sana kabla ya kuamua kuingia kwenye uchaguzi katika mazingira haya.
Nilihoji, tunaweza kwenda kwenye Uchaguzi bila Tume Huru ya Uchaguzi? Jibu likawa – tuwe na Tume Huru. Lakini, safari hii Waangalizi wa Uchaguzi wa Kimataifa hawatakuwepo. Je, tuko tayari kuwa na Uchaguzi usio na waangalizi wa Kimataifa?
Kuhusu kugombea ndani ya CCM:
Tumefikia uamuzi kuwa sisi hatujamkosea mtu, hatujawa wahalifu, na hatuna uoga na tunajiamini. Tunayo haki kabisa ya kugombea Urais kwakuwa tunalindwa na Katiba na si utamaduni. Tunamheshimu Mwenyekiti na tunaiheshimu Kamati Kuu. Walichokisema kilikuwa ni mapendekezo na yatafanyiwa kazi na Halmashauri Kuu ya Taifa ambayo itafanyika mwezi Julai. Chombo kinachotoa adhabu ndani ya CCM ni Halmashauri Kuu ya Taifa; bahati mbaya Kamati Kuu wao walitamka kuwa “Membe tumemfukuza” na hawana mamlaka hayo.
Kamati Kuu ya CCM inaweza ikakataa, ikasema tulichoamua – tumeamua… Inaweza kabisa ikakataa! Ikikataa, sitoweza kwenda Dodoma kuchukua fomu. Kunikataa mimi kugombea ndani ya CCM, Uchaguzi haunogi. Mimi sitakwenda Dodoma mpaka Kamati Kuu itakaponiambia kuwa nipo huru kufanya hivyo, siko tayari kuingia kwenye mtego. Lazima tupate ridhaa!
Nisipopata ridhaa, tunakitakia chama chetu kila la heri. Uchaguzi ni Oktoba, sasa ni Juni… Chochote kinaweza kutokea hapa katikati. Nawaomba vijana tulieni, msilete ghasia zozote. Hatujui Mungu alichotupangia, tusitoe hukumu mapema! Tuwe na imani, yote tumwachie Mwenyezi Mungu.
Video hii hapa:
View attachment 1484912