Uchaguzi 2020 Membe: Kamati Kuu haina mamlaka ya kunifukuza Uanachama wa CCM bali Halmashauri Kuu ya Taifa. Asema kati ya Juni na Oktoba chochote kinaweza tokea

Uchaguzi 2020 Membe: Kamati Kuu haina mamlaka ya kunifukuza Uanachama wa CCM bali Halmashauri Kuu ya Taifa. Asema kati ya Juni na Oktoba chochote kinaweza tokea

Mkuu hongereni kwa hayo maono yenu. Hivi kweli tatizo la sasa ni aina ya mgombea wa upinzani au kutokuwepo kwa tume huru ya uchaguzi? Nisiwe mnafiki, kumchukua Membe kuwa mgombea wa upinzani, ni kosa kubwa kuliko lile kosa walilofanya wapinzani la kumchukua Lowassa 2015.

Ni wapi tunakwama, mbona tatizo la msingi lipo wazi kuwa tume kutokuwa huru ndio tatizo la msingi lilipo? Bila tume huru ya uchaguzi, ni wendawazimu wapinzani kushiriki huo utapeli uitwao uchaguzi.
 
Ubunge viti maalum pia hutegemea wingi wa kura za Rais, chadema wako tayari viti maalum upande wao vipungue kwa kutosimamisha mgombea urais?
 
Huo urais aende akagombee chadema au ACT lakini sio CCM na haita kuja itokee membe awe rais wa tanzania ,hana vigezo wala hata nusu ya kumfikia Dr. Magufuli hakuna wa kumpinga magufuli ndani ya CCM. Over.
Amesema lkn kuwa hakuna ajuae Mungu kapanga nn juu yake na Magu pia. Oct. mbali tutegemee lolote hapa katikati.
 
Chadema watamsimamisha mgombea urais. Ila inavyoonekana Membe atakuwa na jambo moja na ndiyo maana anasema hapa katikati lazima kitokee kitu.

Jambo litakalotokea ni usaliti mkubwa ndani ya CCM na huo usaliti utaitikisa sana CCM tofauti na 2015 kutokana na hulka mbovu ya Rais Magufuli.
 
Pale tu watu walipoanza kufananishana na Yesu, ili kupeana sifa na utukufu wa kiungu, kwa kupitia jicho la tatu wengine tukaiona hiyo ni kufuru kubwa sana mbele ya mbingu. Kwa zama zile za taifa la Israeli, kufuru kama hii ikifanya ilimpasa mfalme kufunga kwa kutokula wala kunywa kwa sikuu kadhaa, na hata pia kuvaa nguo za magunia ili apate kuikwepa hukumu ya Mungu juu yake.

Viongozi hawapaswi kushupaza shingo zao, pale wasikiapo viongozi wa kiroho wakikosoa kufuru zitolewapo kwa kuhusisha utukufu na sifa za Mungu na viumbe vitakatifu vya kimbingu. Vinginevyo utabiri kama ule wa..
Mene, Mene, Tekeli & Peresi...
Tunaweza kupata kuuona ukitimia ndani ya chama tawala katika kipindi kati Julai hadi Oktoba.

Yeye aliye na masikio na alisikie neno hili.
 
Chadema inajitosheleza kila kitu


Sizani kama ni kwa kiasi hicho !

Msidanganyike!

Mtake mkubali Awamu hii inayoisha idadi ya wanachama, wabunge na madiwani iliongezeka
sababu ya mzee mamvi kuja CDM wakati ule !

Sasa mamvi karudi alikotoka.

Unajuaje status ilivyo majimboni?

Je ni ile ile au imeshuka? Au kuongezeka?

Jamaa akija huko atawafaa sana na kuwapa assurance kubwa ya kuboost idadi ya wanachama. Wabunge na madiwani.

Tafakarini
 
Mkuu hongereni kwa hayo maono yenu. Hivi kweli tatizo la sasa ni aina ya mgombea wa upinzani au kutokuwepo kwa tume huru ya uchaguzi? Nisiwe mnafiki, kumchukua Membe kuwa mgombea wa upinzani, ni kosa kubwa kuliko lile kosa walilofanya wapinzani la kumchukua Lowassa 2015. Ni wapi tunakwama, mbona tatizo la msingi lipo wazi kuwa tume kutokuwa huru ndio tatizo la msingi lilipo? Bila tume huru ya uchaguzi, ni wendawazimu wapinzani kushiriki huo utapeli uitwao uchaguzi.
Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100 kuwa bila tume huru hakuna uchaguzi unaostahili kuitwa uchaguzi ila tatizo ni kukosekana kwa msimamo wa pamoja wa wapinzani kuhusu jambo hili hivyo najua watashiriki tu mradi kunadi vyama vyao na kuonyesha nguvu ya watu walio nyuma yao kupitia mikutano ya kampeni lakini sio kutangazwa washindi pale watakaposhinda unless wana mipango ya siri ambao labda sisi hatuijui.
 
Mbona km umepanic Mkuu

Fomu achukue tu ila akubaliane na matokeo
kama hakubali aende ACT ajipime uzito na Magufuli
Sijaona dalili ya Membe kupanic. Ni kweli kwa katiba yenu, kwamba maamuzi ya kamati kuu ni mapendekezo? Kwamba anayefukuza mi Halmashauri Kuu?
 
Hata Mh. Lowasa wafuasi wake aliwaaminisha hivyo hivyo ila kwa sasa wewe mwenyewe anajua
Mrembo unajisikiaje kuanzia mwaka 2015 kila mwaka wa uchaguzi CCM kunakuwa na mvurugano? Halafu wa kipindi hiki ni mvurugano haswaa maana Jiwe kaivunjavunja CCM. Halafu hivi na urembo wote unahangaika na Jiwe!
 
Amesema lkn kuwa hakuna ajuae Mungu kapanga nn juu yake na Magu pia. Oct. mbali tutegemee lolote hapa katikati.
Kama umeona clip kwa umakini, aliposema kati ya juni na octoba aliongeza usiriaz na aliangalia kwenye deski na kuangalia tena watu. Body language, anajua kabisa anagombea urais bali kupitia chama kingine.
 
Back
Top Bottom