Uchaguzi 2020 Membe: Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala, nitajitosa na nitashinda

Uchaguzi 2020 Membe: Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala, nitajitosa na nitashinda

Hivi kuna mtu humu anayeweza kuleta kumbukizi zake, juu ya ile gari ya mhindi iliyonaswa na maburungutu ya minoti 'cash' makao makuu ya chama Dodoma kwenye kinyang'anyiro cha urais mwaka '15, zilikuwa ni za nani kwa jina na hilo saga liliishia wapi?
 
Hivi kuna mtu humu anayeweza kuleta kumbukizi zake, juu ya ile gari ya mhindi iliyonaswa na maburungutu ya minoti 'cash' makao makuu ya chama Dodoma kwenye kinyang'anyiro cha urais mwaka '15, zilikuwa ni za nani kwa jina na hilo saga liliishia wapi?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] membe bhana
 
Nishawahi sema...CDM wanaandaliwa mgombea wa urais toka ccm.
Na nawaona watapelekewa mgombea sio muda mrefu Kama walivyopelekewa 2015 na wanaandaliwa kumpigia Makofi.
Upinzani ukitumia akili Kidogo tu mambo yanakua mazuri Huyu akitoka CCM asipewe kugombea hata uenyekiti wa mtaa awe mwanachama Wa kawaida.
Lakini utashangaa kuna Chama 2020 mgombea wake atakua Membe.
 
Kwa anaeona sawasawa Membe hatakua mgombea wa CCM bali wa anajiandaa kugombea chama kingine.
No chama kipi? Tutajua tu CCM wamemtuma kudhoofisha wapi
 
Kati ya wanasiasa Nassary naye unamhesabu, kuhusu Mbowe kasome katiba ya Chadema
Niwekee wewe hicho kifungu,sijui nisome ya mwaka gani,mana chadema kuna katiba tatu na zote zinatumika kutegemea na mazingira
 
Goood!, Safi sana, yaani hapa sasa nina furaha isiyopimika
Sasa Watanzania, nafasi hiyo ya kuling'oa Jiwe mwaka 2020 imewadia, yaani tushindwe wenyewe!
Tusikubali kulishwa propaganda za #MATAGA wakati kwa miaka hii 4 ilikuwa ni machozi na damu
Miaka hii minne imekuwa ni ya mateso makubwa Kisiasa, kiuchumi kwa wananchi wetu

2020 Twende na Membe
NO RETREAT NO SURRENDER, JIWE MUST GO!
 
Kwanza anatakiwa kuchukuliwa hatua na Chama chake baadae ile sauti yake iliyodukuliwa kusambaa. Hii ya kugombea anasema ili wakimfukuza apate agenda ya kisiasa eti baada ya kuonesha nia ya kugombea urais 2020 ndo amefukuzwa chamani.

Membe anatakiwa kufukuzwa fasta CCM ili akastaafie siasa akiwa opposition.
Afukuzwe kwa kosa la kuwa na nia ya kugombea uraisi? Hapa akili unakuwa umeziweka wapi?
 
Makatibu wamekuja na waraka kwa nia njema tu, tumeona walivyoshambuliwa kwa matusi sijui ndiyo demokrasia unayoisema.
Walikuja na waraka baada ya kumtukana Mkuu wa Nchi wakidhani wapo gizani kumbe ni kama Mbuni wameficha kichwa makalio yapo nje nje! Huo waraka haukuwa na nia njema kwa kuwa walikuwa wamepanga hujuma
 
Niwekee wewe hicho kifungu,sijui nisome ya mwaka gani,mana chadema kuna katiba tatu na zote zinatumika kutegemea na mazingira
Huu ni mwaka wa 10 mnazungumzia uenyekiti wa Chadema, wenye chama wala hawana habari nanyi wanaendelea tu na chaguzi zao, na mwaka huu wanamchagua tena ili kibarua chenu kiendelee.

Chukueni ushauri wa Bashiru kuwa kila chama kinataratibu zake, kama CCM ilivyo na utaratibu wa kuwanyima haki wanachama wake kugombea urais kwa miaka 10.
 
Walikuja na waraka baada ya kumtukana Mkuu wa Nchi wakidhani wapo gizani kumbe ni kama Mbuni wameficha kichwa makalio yapo nje nje! Huo waraka haukuwa na nia njema kwa kuwa walikuwa wamepanga hujuma
Kwahiyo badala ya kutumia vikao kuwasikiliza demokrasia ikawatuma muwatukane.
 
Hivi nyinyi moods wa humu jf hii habari si niliileta Jana Uzi mkaufuta ,ina maana haukuwa wa kweli au mna watu wenu mnaowataka waandike wengine tuwe wasomaji tu na wachangiaji ?
Wanaumia sana lln hawana jinsi
 
Maskini hata mm hii iliniumaa.... Imagine kama ingekuwa mm.... Ila mzee hana makuuu... Alikuja chuoni kwetu.. Akatusalimia msafara wake tu kama vile bado ni president..... Alisema see you torrow morning guys... Nilimshika mkono asee
Naiona CCM iliyopasuka.
Kikwete alikuwepo Dar ila hakukaribishwa kwenye ufunguzi wa Uwanja.
Jina lake lilitajwa kama aliyetoa wazo na si mwanzilishi wa ujenzi.
Kikwete akawa kaenda zake kuhani msiba kwao Mbowe
 
Membe for presidency
2020
tapatalk_1564907492289.jpeg
 
Alishashindwa 2015,huyu atakuja Chadema kuwazungusha vichwa badala ya mikono

Kushindwa siyo hoja, Imran Khan waziri mkuu wa Paksitan amewahi kushindwa zaidi ya mara nne lakini leo ndiyo bosi huko Pakistan. mwaka Membe kushindwa siyo hoja, mwaka 2020 anaweza kushinda maana sasa huenda kajifunza kilichomkwamisha na pia huyu aliyekalia madaraka watu walidhani mtu makini kumbe yeye ndiye mharibuji wa mambo namba 1. Anatumia nguvu nyingi sana for nothing!

Hata Magufuli alivyogombea Ubunge mara ya kwanza ndani ya CCM alipigwa na Kabuye, ni mpaka uchaguzi uliofuata alipopenya kibahati ndani ya CCM na kugombea!
 
Membe alikuwa na nafasi kubwa sana by 2015 kuliko aliyonayo 2020.

Namuona Membe akienda kujaribu bahati yake huko upinzani
 
Back
Top Bottom