Uchaguzi 2020 Membe: Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala, nitajitosa na nitashinda

Duh!
JF ya siku hizi hata kujibu comment za wachangiaji inahitaji moyo sana!

Wewe kwa uzoefu wako hapa ulipaswa angalau ujitofautishe na kundi la instagram lililovamia JF lakini umeshindwa!

Samahani kama nimekukwaza!
Concept yake ni kwamba kama Magufuli kafanya mazuri mengi kwanini anaogopa kushindana na wengine ndani ya chama.
 

Sawa...kujitosa kwake ni sawa kabisa...ila jina lake litaishia kwenye kamati ya maadili...Kamati Kuu itabariki uamuzi wa kamati hiyo na kuamua jina moja tu nalo ni la JPM liende kwenye NEC...Nayo NEC itakubaliana na maamuzi ya Kamati KUU na kuamua kulipeleka kjina moja tu kwenye Mkutano Mkuu..huo ndio utamaduni wa CCM...
 
Ikumbukwe ya kwamba "Tabia haina dawa" mkuu
Membe kuwa Rais!! Hapana kwa kweli. Heri ya Magufuli wetu. Tumwombee Magu,aache hofu ajiamini;awe na hekima na busara,aache kiburi.
 
Kwahiyo maamuzi ya vikao vyote vya chama tayari yanajulikana, kumbe CCM ni predictable.
 
Umeandika poa na kila kitu lakini sioni mantiki ya yeye kusema hivyo halafu Mwanahalisi ndiyo liwe lenye stori husika.
 
Membe kwa urais hapana. Ila nasema hivi . kwa vile hata Magu ameonesha kuto faa . wakipambanishwa tu Magu atakaa . ni bora Membe azuiwe kwa namna yoyote kumuepushia aibu the incumbent
 
Na atafukuzwa tu hakuna namna hata akisema anagombea Urais hawezi kunusurika na kufukuzwa. Atafukuzwa yeye na wenzake wote kama vipi akaanzishe Chama chake ama aungane na vyama vingine
Atafukuzwa kwa kosa gani.
 
Amesema, "Katika hili siwezi kurudi nyuma na hayupo anayeweza kunishawishi kurudi nyuma. Nitagombea, nitajitosa katika kinyang'anyiro hicho kwa kuwa nina kila sababu ya kufanya hivyo."
Labda urais wa YANGA
Kams alishindwa lowassa,alikua na NEC yote,na asilimia 90 ya wajumbe wa mkutano mkuu itakua kikaragosi membe?
Membe ni sawa na joka la mdimuni
 
Ombwe lililopo magogoni ni dhahiri lahitaji kuzibwa. Kinyago tulichokichonga tukiogope vipi? Akalime nyanya chato na kwa vile uwanja wa ndege kajijengea kama maandalizi awe mjasilia mali tu.Nchi hii si sehemu ya Gitarama!
 
Kamilius Membe...! ananikumbusha miaka ya elf 2 kuelekea uchaguzi mkuu wa 2005 kuna Mbunge alikuwa wa jimbo fulani mkoa wa Lindi akiwa mbuge mfululizo zaidi ya miaka 30 na waziri mwandamizi ktk serikali ya Benjamin. Akajitokeza mshindani ktk jimbo hilo ambaye alikuwa timu Membe. Mbunge aliyekuwepo hakukubali kusalenda kwa huyo ndugu ingawa alijua promo ya huyo mshindani wake mtaani. Timu Membe ikamwambia Mbunge Waziri lazima 'tukung'oe tu'. Mbunge akapanic kwamba hawezi kung'olewa km muhogo, alijitahidi kututumia mbinu zake zote abaki lkn wapi mwisho wa siku ilipokaribia mchakato wa kumpata mgombea ndani ya chama akatangaza kutogombea. Wakati wa mchakato ndani ya chama akaja na mbinu ya kumbemba X-DC mmoja ili mshindani wake timu Membe naye akose ubunge lkn alishindwa. Mgombea timu Membe akapeta ndani ya chama na uchaguzi wa 2005 akshinda ubunge na Jakaya akampa uwaziri. Huyo ndo Membe.
 
Ahhhh wapi , fisiem wajinga sana! Hapa wanataka kutuaminisha wagombea Urais 2020 ni kati ya Jiwe Vs Membe , mwisho wa siku Membe anajitoa Jiwe anapita bila kupingwa.

Na msitegemee Membe kufukuzwa Uanachama wa Ccm kwa kumpinga Jiwe , haya ni maigizo. Membe akifukuzwa uanachama wa ccm hapo kweli nitaamini kweli alikuwa anampinga jiwe siyo vinginevyo.


Mark my words.
 
Na atafukuzwa tu hakuna namna hata akisema anagombea Urais hawezi kunusurika na kufukuzwa. Atafukuzwa yeye na wenzake wote kama vipi akaanzishe Chama chake ama aungane na vyama vingine

Wakimfukuza ndio itakuwa vizuri ili mkose pa kujifichia pale mnaposema ccm kuna demokrasia, na mkimuacha mmemuogopa.
 
Hahahaha yaani hakuna anayeongelea kina Mbowe, yaani ni CCM tu. 2020 twende na Magufuli ndiyo mpango mzima!
Inategemea wanakiongelea chama kwa mazuri au mabaya.
 
November 2020 baada ya uchaguzi utuletee feedback please.

Ashinde yeye,asishinde ila moto atakua ameupata na aameungua mpaka matak0!

Atakua ametambua demokrasia ni demokrasia na wananchi ndio maboss wa everything!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…