- Thread starter
- #121
Alijenga airport terminal III.Aliyekuwepo huko nyuma alijenga miundo mbinu IPI?? Huyo hawezi kuwa rais hata kwa mtutu was bunduki!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alijenga airport terminal III.Aliyekuwepo huko nyuma alijenga miundo mbinu IPI?? Huyo hawezi kuwa rais hata kwa mtutu was bunduki!!
Concept yake ni kwamba kama Magufuli kafanya mazuri mengi kwanini anaogopa kushindana na wengine ndani ya chama.Duh!
JF ya siku hizi hata kujibu comment za wachangiaji inahitaji moyo sana!
Wewe kwa uzoefu wako hapa ulipaswa angalau ujitofautishe na kundi la instagram lililovamia JF lakini umeshindwa!
Samahani kama nimekukwaza!
Bernard Kamillius Membe waziri wa zamani wa Mambo ya nchi za Nje na uhusiano wa kimataifa, anazidi kukoleza mbio za kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2020 ndani ya chama cha Mapinduzi CCM. Anaripoti Yusufu Katimba.
Taarifa za hivi karibuni zinasema Membe ambaye alikuwa waziri kwa miaka minane ya utawala wa Jakaya Kikwete, ameapa kujitosa katika kinyang'anyiro cha kumpinga rais wa sasa John Pombe Magufuli.
"Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala tuombe Mungu niwe mzima. Nitajitosa na nitashinda." Amenukuliwa mwanasiasa huyo akiwaeleza baadhi ya wafuasi wake wa karibu ndani ya chama hicho.
Amesema, "Katika hili siwezi kurudi nyuma na hayupo anayeweza kunishawishi kurudi nyuma. Nitagombea, nitajitosa katika kinyang'anyiro hicho kwa kuwa nina kila sababu ya kufanya hivyo."
Kupatikana kwa taarifa kuwa Membe amepanga kujitosa katika mbio za urais 2020, kutaweza kumaliza mining'ono kuwa kwa muda mrefu kiongozi huyo amekuwa akiendesha mikakati yake kimya kimya ya kumkabili Magufuli ifikapo 2020.
![]()
Membe kuwa Rais!! Hapana kwa kweli. Heri ya Magufuli wetu. Tumwombee Magu,aache hofu ajiamini;awe na hekima na busara,aache kiburi.
Kwahiyo maamuzi ya vikao vyote vya chama tayari yanajulikana, kumbe CCM ni predictable.Sawa...kujitosa kwake ni sawa kabisa...ila jina lake litaishia kwenye kamati ya maadili...Kamati Kuu itabariki uamuzi wa kamati hiyo na kuamua jina moja tu nalo ni la JPM liende kwenye NEC...Nayo NEC itakubaliana na maamuzi ya Kamati KUU na kuamua kulipeleka kjina moja tu kwenye Mkutano Mkuu..huo ndio utamaduni wa CCM...
Heri ya nani wee???!!!!?? Watu wanakufa kwa stress.Membe kuwa Rais!! Hapana kwa kweli. Heri ya Magufuli wetu. Tumwombee Magu,aache hofu ajiamini;awe na hekima na busara,aache kiburi.
Umeandika poa na kila kitu lakini sioni mantiki ya yeye kusema hivyo halafu Mwanahalisi ndiyo liwe lenye stori husika.Kuna la ajabu hapo mpaka usiamini, huoni juzi kakiri kuwa sauti iliyodukuliwa ni ya kwake? Kama ameweza kukiri yale atashindwa kuzungumza hayo? Ukweli ni kuwa kuna wanaccm wengi hawaridhishwi na namna Magufuli anavyoongoza chama chao na nchi kwa pamoja kwani kajigeuza kuwa mkubwa kuliko chama na nchi. Sasa huyo Membe anachofanya ni kumuonyesha kwamba yeye sio mkubwa kuliko chama au nchi, hivyo yuko tayari kupambana naye ili kumuonyesha hana madaraka zaidi ya hayo anayopaswa kuwa nayo.
Mimi ninaamini Membe hawezi kuwa rais mzuri, lakini huyu wa sasa sio mzuri pia. Na pia tulishatoka kwenye kuongozwa kwa vitisho na kusujudia viongozi. Sasa hivi tunataka kiongozi anayeheshimu wananchi sio anayeogopwa na wananchi kisa anapandikiza hofu. Kama ni maendeleo tungeweza kuyapata hata chini ya wakoloni, lakini uhuru wetu ulikuwa na maana kuliko maendeleo ya wakoloni.
Kupitia katiba ipi?huu ni uhaini
Atafukuzwa kwa kosa gani.Na atafukuzwa tu hakuna namna hata akisema anagombea Urais hawezi kunusurika na kufukuzwa. Atafukuzwa yeye na wenzake wote kama vipi akaanzishe Chama chake ama aungane na vyama vingine
Lile debe tupu tu, nadhani CCM asilia wamejipanga kimkakatiMusiba yuko wapi aanze kutukana!?
Labda urais wa YANGAAmesema, "Katika hili siwezi kurudi nyuma na hayupo anayeweza kunishawishi kurudi nyuma. Nitagombea, nitajitosa katika kinyang'anyiro hicho kwa kuwa nina kila sababu ya kufanya hivyo."
Ombwe lililopo magogoni ni dhahiri lahitaji kuzibwa. Kinyago tulichokichonga tukiogope vipi? Akalime nyanya chato na kwa vile uwanja wa ndege kajijengea kama maandalizi awe mjasilia mali tu.Nchi hii si sehemu ya Gitarama!Ninachokiona ni Membe kupewa sifa ambazo hana. Hata hivyo sishangai kwa sababu wapinzani wa Rais Magufuli wana ombwe la mtu ambaye atapambana naye katika kiti cha Urais.
Kinachofanyika kwa sasa ni kumshabikia mtu yeyote anayesema au kuonekana atapambana na Rais Magufuli hata kama hana sifa ili tu kujaza ombwe.
Ahhhh wapi , fisiem wajinga sana! Hapa wanataka kutuaminisha wagombea Urais 2020 ni kati ya Jiwe Vs Membe , mwisho wa siku Membe anajitoa Jiwe anapita bila kupingwa.Bernard Kamillius Membe waziri wa zamani wa Mambo ya nchi za Nje na uhusiano wa kimataifa, anazidi kukoleza mbio za kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2020 ndani ya chama cha Mapinduzi CCM. Anaripoti Yusufu Katimba.
Taarifa za hivi karibuni zinasema Membe ambaye alikuwa waziri kwa miaka minane ya utawala wa Jakaya Kikwete, ameapa kujitosa katika kinyang'anyiro cha kumpinga rais wa sasa John Pombe Magufuli.
"Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala tuombe Mungu niwe mzima. Nitajitosa na nitashinda." Amenukuliwa mwanasiasa huyo akiwaeleza baadhi ya wafuasi wake wa karibu ndani ya chama hicho.
Amesema, "Katika hili siwezi kurudi nyuma na hayupo anayeweza kunishawishi kurudi nyuma. Nitagombea, nitajitosa katika kinyang'anyiro hicho kwa kuwa nina kila sababu ya kufanya hivyo."
Kupatikana kwa taarifa kuwa Membe amepanga kujitosa katika mbio za urais 2020, kutaweza kumaliza mining'ono kuwa kwa muda mrefu kiongozi huyo amekuwa akiendesha mikakati yake kimya kimya ya kumkabili Magufuli ifikapo 2020.
![]()
Na atafukuzwa tu hakuna namna hata akisema anagombea Urais hawezi kunusurika na kufukuzwa. Atafukuzwa yeye na wenzake wote kama vipi akaanzishe Chama chake ama aungane na vyama vingine
Inategemea wanakiongelea chama kwa mazuri au mabaya.Hahahaha yaani hakuna anayeongelea kina Mbowe, yaani ni CCM tu. 2020 twende na Magufuli ndiyo mpango mzima!
November 2020 baada ya uchaguzi utuletee feedback please.