Uchaguzi 2020 Membe: Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala, nitajitosa na nitashinda

Uchaguzi 2020 Membe: Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala, nitajitosa na nitashinda

Bahati nzuri na Katiba ya Chama hicho ikaruhusu, nongwa inatoka wapi sasa!
 
Bahati nzuri na Katiba ya Chama hicho ikaruhusu, nongwa inatoka wapi sasa! Watu pekee wanaopiga kelele kuita wenzao sio wazalendo ni kina musiba ambao wanasumbuliwa na mfupa walionao mdomoni.
 
Membe kuwa Rais!! Hapana kwa kweli. Heri ya Magufuli wetu. Tumwombee Magu,aache hofu ajiamini;awe na hekima na busara,aache kiburi.
Mungufuli ni jiwe na jiwe haliwezi kuwa mkate mimi nitaomba awe mwehu aanze kulopoka maovu yote aliyotenda.
 
Membe
Kuna la ajabu hapo mpaka usiamini, huoni juzi kakiri kuwa sauti iliyodukuliwa ni ya kwake? Kama ameweza kukiri yale atashindwa kuzungumza hayo? Ukweli ni kuwa kuna wanaccm wengi hawaridhishwi na namna Magufuli anavyoongoza chama chao na nchi kwa pamoja kwani kajigeuza kuwa mkubwa kuliko chama na nchi. Sasa huyo Membe anachofanya ni kumuonyesha kwamba yeye sio mkubwa kuliko chama au nchi, hivyo yuko tayari kupambana naye ili kumuonyesha hana madaraka zaidi ya hayo anayopaswa kuwa nayo.

Mimi ninaamini Membe hawezi kuwa rais mzuri, lakini huyu wa sasa sio mzuri pia. Na pia tulishatoka kwenye kuongozwa kwa vitisho na kusujudia viongozi. Sasa hivi tunataka kiongozi anayeheshimu wananchi sio anayeogopwa na wananchi kisa anapandikiza hofu. Kama ni maendeleo tungeweza kuyapata hata chini ya wakoloni, lakini uhuru wetu ulikuwa na maana kuliko maendeleo ya wakoloni.
Tulia mkuu 2020 utamuona Membe akimpigia Magufuli kampeni.
 
Tatizo kampeni za Africa zinaitaji pesa nyingi na Huyu ameshaliona hilo.

Kwa mtazamo wengi, B.M anatafuta sababu za kufukuzwa CCM au jina lake kukatwa kwenye mchakato aende Kugombea kupitia ACT.

Kuna ukaribu sana wa kiongozi wa ACT na wale ambao mawasiliano yao yaliyodukuliwa. Na siku za karibuni kumekuwa na kauli kutoka ACT za kuunganisha nguvu uchaguzi ujao.

Tatizo litakuja ACT kupata wadhamini kuchangia kampeni zao.
Hawa wameshavutwa
R.A - ameshasogezwa karibu
M.D - Huyu zilikuwa hazipandi na Mkuu wetu toka enzi za sakata la kusafirisha boti.Nani rafiki wa February. Lakini Mkuu ameona hakuna namna zaidi kumvuta karibu na juzi walionekana kwenye ufunguzi flani pamoja.

Usishangae yule aliyekuwa Yanga, Y.M. Naye anaanza kuvutwa na kufanywa rafiki.
Na mtu kama yule tajiri mkubwa wa africa matatizo yake kutatuliwa na kupewa kipaumbele kwenye mambo yake!

Tatizo ni yule wa risasi za miguuni ambaye bado yupo kwenye matibabu nje ya nchi. Akirudi anaweza kuaribu ndoto ya B.M!
 
Kaka una akili kubwa Sana. Binafsi nimekuelewa vema
Kuna la ajabu hapo mpaka usiamini, huoni juzi kakiri kuwa sauti iliyodukuliwa ni ya kwake? Kama ameweza kukiri yale atashindwa kuzungumza hayo? Ukweli ni kuwa kuna wanaccm wengi hawaridhishwi na namna Magufuli anavyoongoza chama chao na nchi kwa pamoja kwani kajigeuza kuwa mkubwa kuliko chama na nchi. Sasa huyo Membe anachofanya ni kumuonyesha kwamba yeye sio mkubwa kuliko chama au nchi, hivyo yuko tayari kupambana naye ili kumuonyesha hana madaraka zaidi ya hayo anayopaswa kuwa nayo.

Mimi ninaamini Membe hawezi kuwa rais mzuri, lakini huyu wa sasa sio mzuri pia. Na pia tulishatoka kwenye kuongozwa kwa vitisho na kusujudia viongozi. Sasa hivi tunataka kiongozi anayeheshimu wananchi sio anayeogopwa na wananchi kisa anapandikiza hofu. Kama ni maendeleo tungeweza kuyapata hata chini ya wakoloni, lakini uhuru wetu ulikuwa na maana kuliko maendeleo ya wakoloni.
 
Ninachokiona ni Membe kupewa sifa ambazo hana. Hata hivyo sishangai kwa sababu wapinzani wa Rais Magufuli wana ombwe la mtu ambaye atapambana naye katika kiti cha Urais.

Kinachofanyika kwa sasa ni kumshabikia mtu yeyote anayesema au kuonekana atapambana na Rais Magufuli hata kama hana sifa ili tu kujaza ombwe.
Kwani Magufuli ana sifa ????????
 
Kwanza anatakiwa kuchukuliwa hatua na Chama chake baadae ile sauti yake iliyodukuliwa kusambaa. Hii ya kugombea anasema ili wakimfukuza apate agenda ya kisiasa eti baada ya kuonesha nia ya kugombea urais 2020 ndo amefukuzwa chamani.

Membe anatakiwa kufukuzwa fasta CCM ili akastaafie siasa akiwa opposition.
Inavyoonekana hata EL alitarajiwa kustaafia opposition lakini ile mialiko kutoka jumba jeupe imemrudisha alikotoka...
Maji huwa hayasahau baridi...
 
Labda kwa kutumia chadema .. bado tuna imani na magufuli
 
Membe kuwa Rais!! Hapana kwa kweli. Heri ya Magufuli wetu. Tumwombee Magu,aache hofu ajiamini;awe na hekima na busara,aache kiburi.
Hawezi kuacha kibri. Atajuta kujaribu kuua upinzani. Hakujua maneno ya baba wa taifa kuwa upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM?
 
kwahiyo mimi nikisema nagombea jimbo la mtama 2020 kushindana na mbunge wa sasa ni uhaini huo?
Huo ni uhaini dhidi ya mbunge halali wa jimbo hilo anayeishi na kulitawala jimbo mpaka atakaporuhusu mtu mwingine agombee.
 
Back
Top Bottom