Uchaguzi 2020 Membe: Mimi nilitafuta wadhamini kimya kimya kukwepa mtego wa kuvunja kanuni na kuanza kampeni mapema

Uchaguzi 2020 Membe: Mimi nilitafuta wadhamini kimya kimya kukwepa mtego wa kuvunja kanuni na kuanza kampeni mapema

Kwa hiyo Chadema waliotafua wadhamini hadharani wameteleza.?

Kwa hii kauli haoni kama anawasaidia CCM na Tume ya Uchaguzi kufanya fitina.

Upepo wa Lissu unamtesa Sana huyu Membe kuliko nguvu ya CCM.

CCM inapenda watu waoga waoga kama Membe ili ipate kuwaburuza.

Halafu yeye Membe alivyoenda Zanzibar Yale maandamano na zile ahadi jukwaani alikuwa anafanya nini.

Inawezekana Membe ndio mchawi wa Lissu kuliko hata CCM wenyewe.
Huyo ni pandikizi
 
Kwani nyie mnaelewaga basi!

Mpaka mpigwe kidogo kwenye vichwa hivyo ndio mnaelewa.

Hivi unafikiri Membe na Magufuli hawakuwa na hela za kuzungukia mikoani kutafuta wadhamini?
2015 magufuli alivyotangazwa alizunguka. Nchi nzima safari hii kitu gani kimemzuia. 2015 lowassa alizunguka nchi nzima 2010 Dr Slaa alizunguka nchi nnzima. Acheni uoga nyie ccm. Na vibaraka wenu act
 
Itoshe kusema CHADEMA isimame kivyake.
Ni bora CHADEMA isimamie show yenyewe kuliko kua na muungano uchwara na hao vibaraka wa CCM akina Membe.

Tundu Lissu anatosha kusimamia show peke yake na CCM waka surrender .
 
Kama waliozitunga wanazijua kuliko wengine,mbona hawaji mahakamani kuzifanyia hukumu,?kwa taarifa tu, Lissu kakosea kanuni,na ataenguliwa,Sheria zinasomewa ndugu.
Tume ya uchaguzi imetoa kanuni za uchaguzi 2020 hakuna katazo la kampeni za mapema. Kasome
 
Membe mpuuzi anaongea kitu gani? Chadema muogopeni Membe na Zito kuliko Ccm hao ni mapandikizi hakuna wapinzani hapo!
 
Kwani Membe amemtaja mtu yoyote? Amesema yeye amekwepa mtego wa kuanza kampeni mapema bila ya kumtaja mtu yoyote. Kama kuna mtego wa kuanza kampeni mapema basi unawahusu Magufuli,Rungwe na Lissu.
 
Atofautishe kampeni na mikutano,,ambayo hadi mheshimiwa rais aliiruhusu mapema mwanzoni mwa mwezi huu,
Kampeni inaanza kwa kutamkwa rasmi,tumeanza kampeni na pia kuomba kura
 
Mchawi Wa Upinzani ni mpinzani mwenyewe!..Naanza kuiona Vita ya panzi ambayo kwa hakika itamfaidisha zaidi kunguru! Naanza kuamini ule uzushi kuwa Membe ni pandikizi!

Membe sio mpinzani boss, Bali ndio mmiliki wa ACT, na hiyo ACT ilianzishwa ili kuivuruga cdm, na sasa hilo linaanza kuwa wazi peupe.
 
Vurugu gani? Kwani kuna aliyeletewa vurugu?
Au mnataka vurugu?

Tume ya uchaguzi kwa maelekezo ya Magufuli na ccm ndio wanatumika kuaandaa machafuko. Inakuwaje nchi yenye wananchi karibia 60m wapiga kura wawe 29m+? Ina maana nusu ya watanzania wako miaka 18 na kuendelea? Kama idadi ya wapiga kura ni ya uongo, matokeo watatamgazaje ya ukweli? Kama sio kuandaa mazingira ya machafuko ni nini?
 
Mimi nitabaki kusimamia ukweli tu kuwa CDM lissu kawashika Akili na kujikuta mnakurupuka kwa kuwaaminisha kuwa yeye anaijua Sheria wakati haiju. Sasa subirieni kuvuna mlichokipanda nyumbu nyie.
 
Back
Top Bottom