TANZIA Member deo paul55 wa JamiiForums afariki dunia

TANZIA Member deo paul55 wa JamiiForums afariki dunia

Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahala pema peponi
 
Huyu ni moja ya memba tuliekua nae humu kwa muda mrefu. Ni moja ya watu walionifanya niijue JF miaka ya 2013 huko ingawa yeye alichelewa kidogo kujiunga. Na kwa Mara ya mwisho kuonekana humu ni 28/11/2020

Anaitwa Deogratius Paul Maige (30) mkazi wa Madibira Mbarali Mbeya, amefariki usiku wa kuamkia tar 08/12/2020 katika hospital ya Irembula kwa matatizo ya tumbo.

Kwa miaka mingi alikua nasumbuliwa na miguu kufa ganzi kitu kilichofanya ashinde home tu akichat kwenye mitandao ya kijamii. Baadae alipona miguu na ingawa hakuwa full recovered.

Tar 3/12/2020 alipelekwa sanitarium moja baada ya kuona mwili unakosa nguvu, huko aliambiwa anakisukari akapewa dawa lakini hali ikawa mbaya akakimbizwa Ilembula. Baada ya vipimo ikabainika utumbo umejifunga na anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa haraka. Wakati wanaanza mchakato yakatokea ya kutokea .

Atazikwa Leo Tarehe 09/12/2020 katika makaburi ya kanisa Catholic Mahango - Madibira.


R. I. P deo paul555

Facebook alikua anatumia Deogratius Paulo Zachalia.

Apumzike kwa amani


Tutakukumbuka daima kwamchango wako namaono yako.

Amen[emoji120]
 
Utumbo kujifunga/Intestinal obstruction.

Hili tatizo limekuwa kubwa sana mtaani ila halipewi attention kubwa sana na wadau kama mabusha,matende,minyoo etc.

Ukilipata hilo tatizo kuchomoka labda hospital zinazoeleweka,wengi wanafia vyumba vya upasuaji.

Nilimpoteza mwanafamilia pia 2002 kwa tatizo hili.
 
Rest in peace, Mungu akuepushe na adhabu ya kaburi.. ameeni

"Ee mwenyezi Mungu naomba unipunguzie uchungu wa mauti na ninaomba kifo chema siku zangu zitakapo timia"😭😭
 
R.i.p kijana mwenzangu.



Hivi hizi info za watu mnazipataje akati tunatumia fake IDs?, Nawaza siku nami nikifa zitashushwa nondo zangu humu hatari.
Mie Binafsi natamani watu kadhaa wanijue hivi sasa na ID yangu fake ili siku yangu ikifika anayenijua na yeye yu hai bado atoe taarifa zangu halisi
 
Niliyeandika hapa na wewe unayesoma, sote njia yetu ni moja, Naipa familia yake pole sana. Jamiiforums: uongozi na members wote nawapa pole sana! Apumzike kwa amani.

🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom