Huyu ni moja ya memba tuliekua nae humu kwa muda mrefu. Ni moja ya watu walionifanya niijue JF miaka ya 2013 huko ingawa yeye alichelewa kidogo kujiunga. Na kwa Mara ya mwisho kuonekana humu ni 28/11/2020
Anaitwa Deogratius Paul Maige (30) mkazi wa Madibira Mbarali Mbeya, amefariki usiku wa kuamkia tar 08/12/2020 katika hospital ya Irembula kwa matatizo ya tumbo.
Kwa miaka mingi alikua nasumbuliwa na miguu kufa ganzi kitu kilichofanya ashinde home tu akichat kwenye mitandao ya kijamii. Baadae alipona miguu na ingawa hakuwa full recovered.
Tar 3/12/2020 alipelekwa sanitarium moja baada ya kuona mwili unakosa nguvu, huko aliambiwa anakisukari akapewa dawa lakini hali ikawa mbaya akakimbizwa Ilembula. Baada ya vipimo ikabainika utumbo umejifunga na anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa haraka. Wakati wanaanza mchakato yakatokea ya kutokea .
Atazikwa Leo Tarehe 09/12/2020 katika makaburi ya kanisa Catholic Mahango - Madibira.
R. I. P
deo paul555
Facebook alikua anatumia Deogratius Paulo Zachalia.