TANZIA Member deo paul55 wa JamiiForums afariki dunia

TANZIA Member deo paul55 wa JamiiForums afariki dunia

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na awape subira wafiwa katika kipindi hiki kigumu kwao 🙏🏽
kinachonishangaza ni namna hawa watu wanavyojuana huku wanatumia ID za gizani !
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Huyu ni moja ya memba tuliekua nae humu kwa muda mrefu. Ni moja ya watu walionifanya niijue JF miaka ya 2013 huko ingawa yeye alichelewa kidogo kujiunga. Na kwa Mara ya mwisho kuonekana humu ni 28/11/2020

Anaitwa Deogratius Paul (30) mkazi wa Madibira Mbarali Mbeya, amefariki usiku wa kuamkia tar 08/12/2020 katika hospital ya Irembula kwa matatizo ya tumbo.

Kwa miaka mingi alikua nasumbuliwa na miguu kufa ganzi kitu kilichofanya ashinde home tu akichat kwenye mitandao ya kijamii. Baadae alipona miguu na ingawa hakuwa full recovered.

Tar 3/12/2020 alipelekwa sanitarium moja baada ya kuona mwili unakosa nguvu, huko aliambiwa anakisukari akapewa dawa lakini hali ikawa mbaya akakimbizwa Ilembula. Baada ya vipimo ikabainika utumbo umejifunga na anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa haraka. Wakati wanaanza mchakato yakatokea ya kutokea . Alifariki usiku wa saa saba na nusu usiku wa tar 8/22/2020

Amezikwa Leo Tarehe 09/12/2020 katika makaburi ya kanisa Catholic Mahango - Madibira.


R. I. P deo paul555

Baadhi ya michango ya wadau




May his Soul Rest in Eternal Peace[emoji120][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Back
Top Bottom