Members wa JF baadhi wanafiki sana, wanajifanyaga wako sayari nyingine

Members wa JF baadhi wanafiki sana, wanajifanyaga wako sayari nyingine

Nzuri sana, marafiki zangu wameanza kutumia zamaniiii wakawa wananishawishi nijiunge, nikawagomea.

Sasa kuna ile kutumiana post/link kama hauna app ina usumbufu kuaccess, eventually nikafungua account, weee mambo ni motooo 😅
Tusichojua wengi hii mitandao ni kama sokoni. Kuna kila kitu ni wewe tu kichagua unataka nini
 
Kinachoniudhi kwenye hii mitandao ni hicho, hivi kuna ulazima wa kunihusianisha na watu walioko kwenye contacts? Nikitaka akaunti ambayo haitagusiana na watu wangu nafanyaje?
Ngoja wataalamu watakupa muongozo.

Lakini nadhani kule kwenye setting kuna ile sehemu ya kudisable access na contacts zako, lakini sioni ikisaidia, utaletewa tu watu wako kama suggestion. Hii ndio moja ya weakness za alogarithm.

Kuna mtu aliniambia anataka kutengeneza program ya kuzuia ufanyaji kazi wa alogarithm namna hii, siwezi muuliza zaidi maana now hatuongei. (nimekueleza ki-layman) I hope wataalamu watafafanua tectonically.
 
Kuna watu wasiotaka mabadiliko kabisa. Wakati watsapp inaanza hapa TZ kuna watu walikuwa wanaona ni uhuni. Hata matumizi ya computer na printers baadhi ya ofisi hasa za serikali ilichukua muda sana. Wale masecretary waliendelea kukomaa na typewriters. Mtu anayesema hatumii facebook, insta wala tiktok huenda sio mfanyabiashara au hana purpose yoyote maishani.
 
Ni kweli Kuna mtu ambaye Hana purpose yoyote Duniani kweli?. Inauma sana hii, inawezekana mtu akachelewa kujua au akawa anatekeleza purpose bila kujua ila kutokuwa na purpose yoyote Daaah..
 
Mimi nilikua naletewa habari za wasagaji na mashoga nikawa naignore hizo pages mpaka nikachoka.
Nina miezi sijagusa Tiktok
Ile baada ya muda fulani unaanza kuletewa contents unazotaka, hizo zilizogoma labla zilikupenda zenyewe 😂
 
Ngoja wataalamu watakupa muongozo.

Lakini nadhani kule kwenye setting kuna ile sehemu ya kudisable access na contacts zako, lakini sioni ikisaidia, utaletewa tu watu wako kama suggestion. Hii ndio moja ya weakness za alogarithm.

Kuna mtu aliniambia anataka kutengeneza program ya kuzuia ufanyaji kazi wa alogarithm namna hii, siwezi muuliza zaidi maana now hatuongei. (nimekueleza ki-layman) I hope wataalamu watafafanua tectonically.
Sawa Asante
 
Kwa mtazamo wangu, JF ni moja ya mtandao ambayo kwa kiasi kikubwa tunaitumia kupitisha muda na kutoa mawazo kuliko kupata jambo jipya la maana. Mada nyingi zinajirudia, stori ni zilezile na mijadala mingi huishia kwenye mabishano yasiyo na tija.

Ukiangalia kwa makini, kuna muda mwingi unaishia kusoma hoja zilezile kwa watu wale wale, kuhusu mambo yale yale. Ndiyo maana mtu anaweza kutumia masaa mengi hapa bila kupata maarifa mapya, fursa mpya au kitu cha maana anachoweza kwenda kukitumia kwenye maisha yake.

Sina maana kwamba JF haina faida kabisa. Kuna mada nzuri na taarifa muhimu zinapatikana, lakini kwa ujumla wake, mtu asipokuwa makini anaweza kuifanya iwe sehemu ya kupotezea muda tu. Mimi binafsi naiona zaidi kama sehemu ya kupunguza stress na kupitisha muda, siyo sehemu ambayo nitategemea kupata mabadiliko makubwa kwenye maisha yangu.
 
ID nyingi humu ni Wala ugimbi ,hoe hae na makapuku wa kiwango cha lami mkuu..hua nasoma maandiko Yao nacheka sana..yaan JF iwe na watu wenye akili kuliko Facebook??kwa lipi hasa?
Jishikilie wewe.

Sisi humu ni ma-great thinkers, levels za kina plato nakadhalika.

Facebook ni ya mazwazwa akina ndege John etc.

Cc: Mbaga Jr secretarybird
 
Control algorithm yako tu Dot 3 za kulia kwako chini kama ukifungua video au chochote... Kama Interested au Not interested utajua wewe unaselect ipi.

Kama takataka za ushoga zinakufuata kila ulipo kifupi huyo ndio wewe.
 
Wanajifanya hawajui kinachoendelea Instagram kuhusu trends za tiktok wanajifanya hawaitumii ni ya watoto mara wengine wanasema ni ya ma shoga...wakati kiuhalisia tikTok Shop ni moja ya majukwaa makubwa ya ununuzi mtandaoni Asia yote.

Ukimpa stori ya Facebook mtu wa JF anakwambia nilifunga miaka 10 iliyopita, situmii kabisa. Halafu unajiuliza, huyu mtu anajuaje kila kitu kinachotrend kwa sababu ukiangalia mijadala ya humu ndani asilimia kubwa ni mambo yaliyotoka TikTok, Instagram au Facebook.

Hakuna ubaya kutokutumia mitandao fulani. Lakini tusijifanye tunaishi sayari nyingine wakati habari zetu nyingi zinatoka huko huko, me hayo maisha ya kinafiki ndo siyapendi.
Unahakikishaje mtu anajua kitu wakati wewe si huyo mtu?

Halafu kama anajua au hajui, kwa nini hili ni muhimu kwako?

Unaumia mtu akisema hajui mambo ya Tik Tok?

Akisema hajui si umuache tu, kwa nini hili ni jambo la muhimu kwako mpaka ulianzishie uzi?
 
Hata mimi nilidhani hivyo lakini Tiktok ni nzuri kwa biashara.
Watu kibao wanaamini hivi kwamba ni mtandao wa kibiashara lakini hawajawahi uza chochote na wala hawana hiyo biashara, huko kumejaa Malaya, mashoga na mahohe have hata kusoma hayajui.

Yenyewe ni Ku scrow to ma video na maudio na mapicha picha
 
Back
Top Bottom