Meneja: Uwanja wa ndege Chato unahudumia abiria 250 kwa mwezi

Hujui biashara ya ndege wewe tuliza mshono. Mimi juzi nilienda Mtwara Bombadia tulikuwa abiria 15 tu kwenye ndege lakini bado ATCL wanaendelea kwenda huko.
Si ndio maana shirika linajiendesha Kwa hasara!Ndege kutoka Dar kwenda Mwanza,ikipitia Chato ni kuchoma mafuta bure!
 
Suala hapo ni uwanja kutokuwa na tija Kwa Sasa!
 
Uwanja kujengwa Chato bado ni mali ya serikali na fedha zilizotumika ni za serikali, itakua jambo la ajabu kama serikali haifanyi juhudi zozote kuona uwanja ule unatumika.
 
Abiria 8 kwa siku hata dereva bajaji atakataa kufanya biashara hiyo. Ni hamnazo tu ndio anaweza fanya hiyo biashara na kuja hapa kujaza seva za jf
 
Hivi wale waliotaka kuanikia mazao waliishia wapi...[emoji3]
 
Mtu wa Geita hawezi kwenda Chato,ataenda Mwanza!
Mkuu kutoka Geita kwenda Mwanza ni kilometa 137 wakati kutoka Geita kwenda Chato ni kilometa 70. Kwa mtu anayetaka kusafiri kwa ndege kutoka Geita kwenda Mwanza, Arusha na Dar es salaam, ni rahisi kwake kwenda kupandia Chato na zaidi kwa taarifa ndege hiyo hiyo inayoondokea Chato ni lazima itue Mwanza kwanza.

Mara yangu ya mwisho kutumia njia hiyo ni tarehe 06.01.2022 na hesabu zangu za haraka pale Chato tu, tulipanda watu 26 na ndege ilijaa viti vyote. Kiwanja cha Chato kimeleta nafuu ya usafiri kwa mikoa ya Kigoma, hasa wilaya za Kibondo na Kakonko. Mkoa wa Kagera, wilaya za Biharamlo na Ngara,Mkoa wa Geita na hapa miji inayochipukia kama Katoro, Bwanga, Ushirombo, Runzewe na Nyakanazi wanatumia sana kiwanja kile.
 
Zinazotua zitakuwa ni ndege za gamboshi zinazowapeleka wazee shift kulinda kaburi la mwanachama wao kama walivyoahidi kumulinda kwa gharama yoyote.
 
250/30 =8.33
Sasa wastani wa abiria nane Kwa siku ni matumizi mabaya ya rasilimali watu na miundombinu hiyo ya uwanja na ndege!
Uwanja hauna tija hapo Chato!
Hujui hesabu
Umeambiwa routes 3 kwa wiki.
 
Mkuu ndege ikitoka Mwanza na watu 76,wakatua Chato na akapanda mmoja basi uwanja unarecord umehudumia watu 76!
Mkuu, Hesabu ya abiria wanaoshuka au kupandia Chato haijumuishi abiria wanaoshuka au kupandia Mwanza. Abiria wa Mwanza hawashuki Chato kuhesabiwa idadi yao na wala abiria wanaopandia Mwanza hawahesabiwi pamoja na wale waliopandia Chato.

Tangu mwaka jana nimekuwa nikisafiri kupitia uwanja wa Chato, nimefanya safari nne na zote nimejiridhisha kuwa Chato itakuja kuwa moja ya route tegemeo ya Air Tanzania.
 
Naam. Hata hao watoa huduma watashindwa kupata faida ya kuendesha biashara zao.
250/30 =8.33
Sasa wastani wa abiria nane Kwa siku ni matumizi mabaya ya rasilimali watu na miundombinu hiyo ya uwanja na ndege!
Uwanja hauna tija hapo Chato!
 
Mwaka jana mwezi wa tano nikiwa uwanja wa ndege Chato, nilipiga picha za kumbukumbu na nia yangu hasa nilitaka kuonyesha nyomi iliyokuwepo siku hiyo kwa abiria waliopandia Chato kwenda Dar es salaam. Kilichoniduwaza kuna mdada mmoja pale yuko kwenye kitengo cha ukaguzi, alinifuata na kunitaka nifute picha zote nilizopiga kwa kuwa hawaruhusu.

Nilifuta picha zote na kila nikipita hapo sina mpango tena wa kupiga picha pale kwa kuwa nimekoma!. Kila ninaposoma taarifa za uwanja wa ndege wa Chato, nagundua upotoshaji na taarifa nyingi zisizo sahihi ambazo zingeweza kukanushwa na abiria wanaoutumia uwanja ule mara kwa mara kwa kuonyesha picha zenye uhalisia. Mamlaka ya viwanja vya ndege, na hasa mamlaka inayosimamia uwanja wa Chato mnapaswa kutetea hoja zenu maana biashara ni matangazo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…