Meneja: Uwanja wa ndege Chato unahudumia abiria 250 kwa mwezi

Meneja: Uwanja wa ndege Chato unahudumia abiria 250 kwa mwezi

Kamati ya roho mbaya hamna "credibility" yoyote ile ya kitakwimu, zaidi ya kuja na takwimu za kupikwa ili muweze kusubiri "karma" yenu juu ya matendo yenu maovu.
 
250/30 =8.33
Sasa wastani wa abiria nane Kwa siku ni matumizi mabaya ya rasilimali watu na miundombinu hiyo ya uwanja na ndege!
Uwanja hauna tija hapo Chato!
Arusha yanaelekea mabasi zaidi ya 10 kwa siku lakini uwanja wa ndege haujajengwa.

Chattle hakuna hata basi moja la abiria linalo3lekea huko, lakini wanajenga uwanja wa ndege.

Mtaumbuka tu. Mungu hapendi uongo na utapeli
 
Meneja wa uwanja wa ndege wa Chato amesema uwanja huo umefikia 95% ya ujenzi wake na kwamba uwanja huo umekuwa msaada mkubwa sana kwa wakazi wa kanda ya ziwa na nchi jirani.
Meneja amesema mpaka sasa kwa wasitani wana hudumia abiria 250 kwa mwezi na ndege za shirika la ATCL zinatua uwanjani hapo mara 3 kwa wiki. Pia shirika la TANAPA wanatumia mara kwa mara uwanja huo kwa shughuli zao za uhifadhi.

My take.
Huu ni uthibitisho tosha kuwa kila alichofanya Magufuli alifanya kwa masilahi ya taifa hili, na ujumbe huu uwafikie wote wenye roho za korosho na wapinga maendeleo wote ikiwemo timu gaidi.

250 Kwa Mwezi ni Average ya watu nane Kwa siku halafu unasifia
Kama hizi sio akili za Maiti itakuwa nini jamani
 
Mara 3 kwa wiki kupitia ATCL
Mkuu (mfano) wenye makampuni ya mabasi wanapotoa mabasi mapya huwa wanayatoa kipindi ambacho hhakuna wateja/abilia wengi kama ilivyo mwezi wa kumi na mbili.

Na kwa kipindi hicho chombo usafiri na abilia mpaka 11 huku wengi wa hao wakiwa wa njiani, na uchoma mafuta na tyres kurika kwa hata miezi 5 na huwa wanaamini bandaye msimu na abilia wakitambua huduma zake watakuja na kutumia gari zake.

Unadhani ile safari ya India ndege ilijaza abilia wote 200na kenda?
Mkuu pambania regase😄
 
Mkuu, Hesabu ya abiria wanaoshuka au kupandia Chato haijumuishi abiria wanaoshuka au kupandia Mwanza. Abiria wa Mwanza hawashuki Chato kuhesabiwa idadi yao na wala abiria wanaopandia Mwanza hawahesabiwi pamoja na wale waliopandia Chato.

Tangu mwaka jana nimekuwa nikisafiri kupitia uwanja wa Chato, nimefanya safari nne na zote nimejiridhisha kuwa Chato itakuja kuwa moja ya route tegemeo ya Air Tanzania.
Wewe ni mkazi wa Chato?Ndege inapotua Chato na kuondoka lazima iingie kwenye record kuwa imepaa kutoka Chato na abiria wangapi!
Nipe ushahidi wa tiketi maana ni online booking,Naona umeleta story tu ya kujitungia!Weka ticket Moja tu,ficha details!
 
Hujui hesabu
Umeambiwa routes 3 kwa wiki.
Wewe naye kilaza tu,Sasa hapo Mimi nimetoa wastani wa siku!Unashindwa Nini kuzidisha Kwa 7/3 upate wastani wa wiki?Ulitaka hata wastani Kwa saa utapata!
 
Mkuu, Hesabu ya abiria wanaoshuka au kupandia Chato haijumuishi abiria wanaoshuka au kupandia Mwanza. Abiria wa Mwanza hawashuki Chato kuhesabiwa idadi yao na wala abiria wanaopandia Mwanza hawahesabiwi pamoja na wale waliopandia Chato.

Tangu mwaka jana nimekuwa nikisafiri kupitia uwanja wa Chato, nimefanya safari nne na zote nimejiridhisha kuwa Chato itakuja kuwa moja ya route tegemeo ya Air Tanzania.
Kwanini watu wanaumia wakisikia habari kama hizo kuhusu Chato?
 
Abiria 250 kwa mwezi sawa na abiria 8 kwa siku...

Ndege inapiga trip tatu kwa mwezi... Wasatani wa abiria 83 kwa kila trip...

Bado hali sio mbaya sana... Ngoja tuone mbele ya safari... Huenda ukaleta tija vile uwanja sio kama maembe kwamba utakufa...

Japo JpM alikurupuka sana kuujenga
 
Mkuu kutoka Geita kwenda Mwanza ni kilometa 137 wakati kutoka Geita kwenda Chato ni kilometa 70. Kwa mtu anayetaka kusafiri kwa ndege kutoka Geita kwenda Mwanza, Arusha na Dar es salaam, ni rahisi kwake kwenda kupandia Chato na zaidi kwa taarifa ndege hiyo hiyo inayoondokea Chato ni lazima itue Mwanza kwanza.

Mara yangu ya mwisho kutumia njia hiyo ni tarehe 06.01.2022 na hesabu zangu za haraka pale Chato tu, tulipanda watu 26 na ndege ilijaa viti vyote. Kiwanja cha Chato kimeleta nafuu ya usafiri kwa mikoa ya Kigoma, hasa wilaya za Kibondo na Kakonko. Mkoa wa Kagera, wilaya za Biharamlo na Ngara,Mkoa wa Geita na hapa miji inayochipukia kama Katoro, Bwanga, Ushirombo, Runzewe na Nyakanazi wanatumia sana kiwanja kile.
Umeandika uongo,road distance kati ya Geita na Chato ni 115km!wakati Mwanza to Geita ni 124 km!
Eti imeleta unafuu Kwa kigoma,una akili kweli?Unajua umbali wa kibondo mpaka Chato ni almost 240 km!
 
Chato haiwezi kukosa abiria ukizingatia Geita kuna makampuni mengi ya madini na wafanyabiashara wakubwa wapo wengi tu.
Sasa kwanin uwanja Huo usingejengwa Geita?
 
250 x TZS 450,000.00= 90,000,000+2,250,000=TZS 92,250,000.00/ mwezi

Kwa mwaka, karibu 1 bilioni.Siyo haba.
Uwanja umejengwa kwa Bilioni 38. Kwa hesabu zako itachukua miaka 38 kurudisha gharama za ujenzi wa uwanja.miaka 38 ni Selikari 4. Sasa fikiria hela ni ya mkopo wa miaka 5 yaani unalipa deni huku huna faida unayoingiza.


Hiyo billion 1 kwa mwaka ondoa operating cost za ndege, uwanja ili ujue unazalisha faida au hasara.
 
Kia
Arusha yanaelekea mabasi zaidi ya 10 kwa siku lakini uwanja wa ndege haujajengwa.

Chattle hakuna hata basi moja la abiria linalo3lekea huko, lakini wanajenga uwanja wa ndege.

Mtaumbuka tu. Mungu hapendi uongo na utapeli
H haitoshi?! Au Arusha hupajui?!
 
Back
Top Bottom