Meneja: Uwanja wa ndege Chato unahudumia abiria 250 kwa mwezi

Meneja wa uwanja wa ndege wa Chato amesema uwanja huo umefikia 95% ya ujenzi wake na kwamba uwanja huo umekuwa msaada mkubwa sana kwa wakazi wa kanda ya ziwa na nchi jirani.
Meneja amesema mpaka sasa kwa wasitani wana hudumia abiria 250 kwa mwezi na ndege za shirika la ATCL zinatua uwanjani hapo mara 3 kwa wiki. Pia shirika la TANAPA wanatumia mara kwa mara uwanja huo kwa shughuli zao za uhifadhi.

My take.
Huu ni uthibitisho tosha kuwa kila alichofanya Magufuli alifanya kwa masilahi ya taifa hili, na ujumbe huu uwafikie wote wenye roho za korosho na wapinga maendeleo wote ikiwemo timu gaidi.

Jinga sana ww. 250 kwa mwezi ndio unaringa? Hio ni LOSS KUBWA SANA KWA HILI TAIFA.. Ni sawa na kujenga hotel kubwa ya room 1000, halafu ni room moja tu mtu anakaa kwa siku. Nyingine 999 hazina watu kabisa
 
Uwanja umejengwa kwa Bilioni 38. Kwa hesabu zako itachukua miaka 38 kurudisha gharama za ujenzi wa uwanja.miaka 38 ni Selikari 4. Sasa fikiria hela ni ya mkopo wa miaka 5 yaani unalipa deni huku huna faida unayoingiza.

Hiyo billion 1 kwa mwaka ondoa operating cost za ndege, uwanja ili ujue unazalisha faida au hasara.
Yaani mmeishapanga kuwa kwa miaka yote hiyo 38 watanzania hatutazaliana na kuongezeka. Kwa takwimu za hivi karibuni population growth rate yetu ni kama 2.5%.

Pia kuna factors nyingine za kulazimisha discounted payback period ya mradi wa uwanja huo pamoja na shughuli zinazochichewa na uwanja huo ishuke mpaka iwe chini ya miaka 5. Mkuu, nadhani wewe ni mchumi utakuwa unajua ninaxhokieleza hapa.

Karibu.
 
Hoja ni kwamba hauna tija Kwa Sasa na ulijengwa huko bila uhitaji!
Kupanga ni kuchagua,kwani huo uwanja ungejengwa pale ambapo kutakuwa na demand,tatizo lingekuwa wapi?
Kuna sehemu ambazo zinahitaji uwanja wa ndege Kwa Sasa lakini hakuna,angalia miji kama Kahama,geita kukosa uwanja halafu unaenda kujenga Chato!
Kahama kuna uwanja, na pia Geita kuna uwanja! Labda ungesema vijengwe viwanja vikibwa
 
Ni wanafamilia wa Magu, Kalemani, na Dotto, hao ndio hupanda ndege hiyo, ni uwanja wa familia ya JPM, Rais wa hovyo kabisa kuwahi kuongoza nchi hii, hovyo kabisa
Moja kati ya post za kipuuzi ni hii. Kweli unadhani pamoja na tawala zote za uraisi ndo Marehemu Magufuli alikua wa hovyo kabisa huku unasahau leo hii unatumia miundombinu mingi aliyoimalizia na aliyoianzisha na bado alijitahidi kwa nafasi yake. Hamna ambaye atakua safi ktk utawala ila alijitahidi kufumbua watanzania akili kufahamu mamlaka kamili aliyonayo raisi na utendaji wake kwamba inawezekana ila watawala wanaamua kujinufaisha wenyewe na sio Taifa mkuu. Jitafakari
 
Mkuu (mfano) wenye makampuni ya mabasi wanapotoa mabasi mapya huwa wanayatoa kipindi ambacho hhakuna wateja/abilia wengi kama ilivyo mwezi wa kumi na mbili.

Na kwa kipindi hicho chombo usafiri na abilia mpaka 11 huku wengi wa hao wakiwa wa njiani, na uchoma mafuta na tyres kurika kwa hata miezi 5 na huwa wanaamini bandaye msimu na abilia wakitambua huduma zake watakuja na kutumia gari zake.

Unadhani ile safari ya India ndege ilijaza abilia wote 200na kenda?
Mfano sahihi kabisa
 
Alikuwa Rais wa hovyo kabisa, hovyo sana
 
250/30 =8.33
Sasa wastani wa abiria nane Kwa siku ni matumizi mabaya ya rasilimali watu na miundombinu hiyo ya uwanja na ndege!
Uwanja hauna tija hapo Chato!
Mkuu hiyo 250/30 umeitolea wapi? Wakati ushaambiwa wastani wa flight ni 3 kwa wiki? Kwahivyo inamaana kwa mwezi flight 12 tu
 
Hauko chato wewe kichwa panzi! Hautafungwa jidanganye hizo sehemu kuna watu watafutaji sana mkuu!
Siwezi kaa chato hakuna hela hakuna chochote cha maana.
Nimefanya kazi Geita na chato nimefika mara nyingi halmashauri yao. Ule umbali huwezi kutoka katoro ukawahi ndege chato..

Na usitujaze ujinga hapa wasukuma wapande ndege wanaenda wapi?

Uwanja wa Chato ni liability. Wasipogeuza Chato kuwa makao makuu ya mkoa huo uwanja na miradi mingine itakufa.

Kama manager kakiri wateja 250 inamaana ni watu 8 per day..hivi biashara ghani inafanyika kwa style hiyo?
 
250/30 =8.33
Sasa wastani wa abiria nane Kwa siku ni matumizi mabaya ya rasilimali watu na miundombinu hiyo ya uwanja na ndege!
Uwanja hauna tija hapo Chato!
kwa wiki anatua mara 3x4=12
 
Uwanja huo umejengwa kwa bei gani? vs hao abilia 250 kwa mwezi.
 
250/30 =8.33
Sasa wastani wa abiria nane Kwa siku ni matumizi mabaya ya rasilimali watu na miundombinu hiyo ya uwanja na ndege!
Uwanja hauna tija hapo Chato!
Mkuu una matatizo makubwa ya mathematics. Umeambiwa ndege huja mara 3 kwa wiki. Jaribu tena kwa kutumia ndondoo nilizokupa.
 
sijaelewa, uwanja unapokea abiria 250 (mia mbili hamsini) au laki mbili na nusu? yaani mwezi mzima watu 250? kwa uwanja uliojengwa kwa bilioni zaidi ya 40? jamani jamani tujifunzege basi.
 
Mkuu (mfano) wenye makampuni ya mabasi wanapotoa mabasi mapya huwa wanayatoa kipindi ambacho hhakuna wateja/abilia wengi kama ilivyo mwezi wa kumi na mbili.

Na kwa kipindi hicho chombo usafiri na abilia mpaka 11 huku wengi wa hao wakiwa wa njiani, na uchoma mafuta na tyres kurika kwa hata miezi 5 na huwa wanaamini bandaye msimu na abilia wakitambua huduma zake watakuja na kutumia gari zake.

Unadhani ile safari ya India ndege ilijaza abilia wote 200na kenda?
Amekupotosha, hajui hesabu Mkuu. Mwambie arudie kama anauwezo huo wa mahesabu ili tathmini uifanye kwa takwimu sahihi
 
Meneja wa uwanja wa ndege wa Chato amesema uwanja huo umefikia 95% ya ujenzi wake na kwamba uwanja huo umekuwa msaada mkubwa sana kwa wakazi wa kanda ya ziwa na nchi jirani.
Meneja amesema mpaka sasa kwa wasitani wana hudumia abiria 250 kwa mwezi na ndege za shirika la ATCL zinatua uwanjani hapo mara 3 kwa wiki. Pia shirika la TANAPA wanatumia mara kwa mara uwanja huo kwa shughuli zao za uhifadhi.

My take.
Huu ni uthibitisho tosha kuwa kila alichofanya Magufuli alifanya kwa masilahi ya taifa hili, na ujumbe huu uwafikie wote wenye roho za korosho na wapinga maendeleo wote ikiwemo timu gaidi.

Jambo jema hapo bei Kwa mtu mmoja ikoje??
 
sijaelewa, uwanja unapokea abiria 250 (mia mbili hamsini) au laki mbili na nusu? yaani mwezi mzima watu 250? kwa uwanja uliojengwa kwa bilioni zaidi ya 40? jamani jamani tujifunzege basi.
Leta takwimu za viwanja vya level ya Chato dunia ili tuweze kujadili kwa ufasaha
 
250/30 =8.33
Sasa wastani wa abiria nane Kwa siku ni matumizi mabaya ya rasilimali watu na miundombinu hiyo ya uwanja na ndege!
Uwanja hauna tija hapo Chato!
Unajua safari Kwa wiki ziko ngapi??
 
Mkuu una matatizo makubwa ya mathematics. Umeambiwa ndege huja mara 3 kwa wiki. Jaribu tena kwa kutumia ndondoo nilizokupa.
Sasa hapo kwenye hiyo 8.33 ni wastani wa siku,ulitaka kujua wastani Kwa kila safari basi unachukua 8.33×7/3,mbona simple tu!
Nikutoe tongotongo,hata kama mshahara wako unalipwa Kwa mwezi,ila unaweza kutafuta wastani wa mshahara wako Kwa wiki,siku,saa,dakika hata sekunde!Hizo ni mean estimations tu!
 
Back
Top Bottom