Meneja: Uwanja wa ndege Chato unahudumia abiria 250 kwa mwezi

Meneja: Uwanja wa ndege Chato unahudumia abiria 250 kwa mwezi

Sio kwamba hao abiri ni wa Chato,mfano ndege ikitoka dar inaenda Mwanza,ikitua Chato na abiria 70,walashuka watatu,basi uwanja unarecord umehudumia abiria 70 japo hao wengine 67 wanaenda Mwanza!
Hakuna route inayoanzia Chato au kuishia Chato!
Unadhania.Toa ukweli wa data halisi.
 
Angalia huyu nae eti anajiona ana akili. Acha kukurupuka, hesabu yangu inahusu aliesema ndege inakuja mara moja kwa wiki.
Kama ni mara moja kwa wiki, ingekuwa abiria 30. Abiria 60 ulipata kwa hesabu gani?
 
Chato ni kijiji chenye uwanja wa ndege.Mwenye akili ndogo peke yake ndiye anayeelewa kilichofanyika pale.Ile pesa iliyotumika pale bora ingeboresha maisha ya wanakijiji hata kwenye huduma ya maji ambao hadi sasa bado kuna maeneo mengi wanafwata maji ziwani kwa ndoo na baiskeli uku hali za maisha kwa wanainchi waliowengi zikiwa niza shida.Ukitembea kuanzia bwanga hadi mganza ukaambiwa hao wanakijiji wanamiliki uwanja wa ndege mkubwa utasikitika sana.Na hata kama kulikua na uhitaji haukupaswa uwe uwekezaji mkubwa vile.Yale ni matumizi mabaya ya cheo tuache kuremba rema bila sababu.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Naunga mkono hoja, Wachina ndio wanapenda bond za hivi, tuchukuwe pesa za wachina tuwaachie uwanja huo useless kabisa.
Huo uwanja sio useless kwao. Si wanaweka airbase kwa ajili ya East & Central Africa power projection
 
Tukimaliza tuambiane na wa mtwara unapitisha abiria kiasi gani, au wa mpanda kwa Pinda nao unapitishia abiria wangapi kwa mwezi then tufanye ulinganishi.
 
ukisoma hii thread plus wachangiaji , unagundua bara la afrika haliendelei kwa kuweka chuki mbele , ule uwanja wa chato ni sawa na viwanja vingine vya wilaya mbali mbali hapa Tz ila watu wamekosa hoja za kumkosoa marehemu basi hii ndo inabakia kuwa hoja ila in reality , hakuna route za kila siku hapo chato pia shirika la ndege sio wajingq kias hicho kuruhusu ndege kubeba watu sita kila siku throughout the year , Wabongo tunaendekeza siasa chuki na tutavuna tunachokitafuta one day
Namkubar sana mzee Jpm kwa nia na kazi nyingi nzuri alizofanya kwa Tanzania hii.

Lakini kwa ujenzi wa huu uwanja Chato na hata ujenzi unaoendelea pale Nduli Iringa ni investiment za hasara sana.

Hata kama kwa wiki inaruka ndege mara 2 ukichukua hizo nauli ugawe kwa expenses zote utaona shirik linaingiza loss kubwa san
 
Wewe ni taahira! Katoro Chato kilometer 45 na katoro mwanza kilometer 165 uwezo unafatilia! Katoro niko ndani ya wilaya ya chato wewe inakuja kutuambia kutoka katoro kwenda mwanza ni karibu kuliko kutoka katoro kwenda chato!
Kilometa 45 za kinyesi labda.acha kudanganya watu ili tu ujifanye unajua kutetea legacy.Una google taarifa zako kwa mihemko alafu unatuletea hapa.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Ninasikitika kwasababu Watanzania hamjui hukumu za haki isipokuwa chuki.
Kwa mtu anayetumia usafiri wa anga Tanzania huwezi kuwabeza Wasukuma.
Ukiwa JNI waiting lounge 30% wasukuma hujaa.
90% ya wasafiri wa route za Mwanza ni wasukuma.
99% ya route za Tanzania route za kanda ya ziwa ina abiria wengi.
Acheni chuki Msukuma na kanda ya ziwa sio wanyonge.
Tunaongelea uhalisia mambo ya chuki unasema wewe au uduni unaleta wewe.haya ni maisha ya watanzania wote ila kwenye ukweli yatupasa tuseme.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Tunaongelea uhalisia mambo ya chuki unasema wewe au uduni unaleta wewe.haya ni maisha ya watanzania wote ila kwenye ukweli yatupasa tuseme.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Chato haiwezi kukosa abiria ukizingatia Geita kuna makampuni mengi ya madini na wafanyabiashara wakubwa wapo wengi tu.
 
Usikariri maisha! Ushawahi kuuliza wakati JNIA au Kilimanjaro airport inaanza walianzaje? Nyinyi akili zenu zinawaza leo utafikiri Tanzania haitakuwepo baada ya miaka 50!
Huna sababu yakulazimiasha mambo ambayo yangefanyika miaka 30 ijayo ukalazimisha kuyafanya leo wakati kuna mambo ya msingi ambayo ni mahitaji muhimu ya watu wako ya kila siku.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Huu ndo uwanja wa kimataifa wanaosema magufuli alijenga kwao!!?? Hii nchi ina watu wa ajabu sana.
 
Huo ni uwanja wa ndege,usilete story za mabasi!
Kuna maeneo ambayo Yana mahitaji ya uwanja wa ndege,mji kama Kahama ambao umechanganya sana kibiashara!Sasa unapoenda kuweka uwanja sehemu ambayo Bado Haina demand ya uwanja,unaonekana mwendawazimu!
Yaani unaacha maeneo potential unaenda kuzika Hela sehemu isiyo na mwamko!
Jambo likishatokea nini kifanyike?
Pesa imeshazikwa pale tayari so what next, tusianze kutupiana lawama hapa wanaJF utadhani sisi/mimi ndiye nilijenga ahahahaaaa tuelezane ukweli hapa mkuu, as kama mkeo kajifungua nyani au si damu yako utafanyaje?.
 
250 x TZS 450,000.00= 90,000,000+2,250,000=TZS 92,250,000.00/ mwezi

Kwa mwaka, karibu 1 bilioni.Siyo haba.
 
Ni wanafamilia wa Magu, Kalemani, na Dotto, hao ndio hupanda ndege hiyo, ni uwanja wa familia ya JPM, Rais wa hovyo kabisa kuwahi kuongoza nchi hii, hovyo kabisa
Tema mate chini.

#MaendeleoHayanaChama
 
Jambo likishatokea nini kifanyike?
Pesa imeshazikwa pale tayari so what next, tusianze kutupiana lawama hapa wanaJF utadhani sisi/mimi ndiye nilijenga ahahahaaaa tuelezane ukweli hapa mkuu, as kama mkeo kajifungua nyani au si damu yako utafanyaje?.
Tulipiga kelele sana wakati huo!Tunaongea hapa Ili tabia kama hiyo isijirudie!
 
Back
Top Bottom