Meneja wa TRA Kibondo akamatwa na meno ya tembo

Meneja wa TRA Kibondo akamatwa na meno ya tembo

Jeshi la Polisi Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma linamshikilia Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Wilayani humo Irving Mutegeki kwa tuhuma za kukutwa na meno ya Tembo.

Mutegeki Bagasheki amekamatwa na nyara hizo za Serikali Wilaya ya Kibondo Julai 2, 2024 akiwa kwenye gari binafsi majira ya usiku na anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Meneja huyo wa TRA anadaiwa amekuwa akifanya biashara ya meno ya Tembo kutoka Wilaya ya Kibondo na Kakonko kwenda mikoa mbalimbali nchini na nje ya nchi ikiwemo Burundi.
ameshindwa kuelewana na hao waliomkamata hadi anadhalilishwa hivi
amezingua
 
Jeshi la Polisi Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma linamshikilia Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Wilayani humo Irving Mutegeki kwa tuhuma za kukutwa na meno ya Tembo.

Mutegeki Bagasheki amekamatwa na nyara hizo za Serikali Wilaya ya Kibondo Julai 2, 2024 akiwa kwenye gari binafsi majira ya usiku na anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Meneja huyo wa TRA anadaiwa amekuwa akifanya biashara ya meno ya Tembo kutoka Wilaya ya Kibondo na Kakonko kwenda mikoa mbalimbali nchini na nje ya nchi ikiwemo Burundi.
Wizi wote wanaoufanya TRA haukumtosha?

Hayo manamba yote ya nini? Huyu ni jambazi kabisa, inaonesha ana mengi sana ya kujibu.
 
Hizo plate numbers pia😅 usikute walikuwa wanatfuta kitu kingine kbs.. ila walivyoyaona hayo manamba mengi ikabidi waingie deep..

Imenikumbusha siku moja nimetoka shamba/site nikasahau SIME kwenye gari, zikapita kama siku 3 nikaw niko Posta, hiyo siku sina hili wala lile gari ikawa imezungukwa na polisi kama vile mm ni Jambazi (Enzi za kuzuia Tinted kali) basi nikawaacha wafanye search..

Aisee wakakutana na Sime ikabidi wanipige pingu, wakaendelea kufumua mpk chini ya kapeti.. engine compartment yote chungulia mpk na tochi hawakukuta kitu kingine..

Ikabid wanihoji pale nikawaelezea ABC wakamiachia ila kwa mbinde sana..

Sasa imagine ndio umebeba labda bange hata grams mbili tu za kuvutia beach alafu msala unatokea kama hivyo wao watakutangaza kama MSAFIRISHAJI WA MADAWA YA KULEVYA.
Hii biashara za mihogo ina mambo mengi,ukiletewa mezani
Mipesa yake inatamanisha sana
Ni biashara unayotakiwa kuwa na mtandao mpana
Longtime sana,ndy nakutana na malkia wa pembe za ndovu hotelini kwake pale beijing opp na shoppers plaza
Pale si kulikuwa na wageni wengi kutoka China wanafikia,kumbe yule mama alikuwa anaona sana pilika zangu nkiingia pale kuwafTa wageni wangu wachina....ananisoma tu....
Sasa kuna siku yule mama akaniita akasema nna maongezi na wewe,tukapanga siku ya meeting pale ....
Siku naonana naye sasa akaanza kuniambia ebwana ehh yule mama alikuwa anajuwa kila kitu nachofanya na wale wachina 😄
Yule mama wa kichina naye,baada ya kuona pilika zangu na ufaster wangu kwa wale wageni wa kichina akavutiwa na mm sasa,kukawa na ukaribu
Yule mama alikuwa anajuwa dili bana Ana michakato kibaooo
Hawa sjui wakubwa marpc polisi anaongea wakat wowote
Sasa kuna siku hyo aliinita akaniambia kwake watakuja wageni kutoka China na nia yao waende kongo wakanunue dhahabu na wanakuja na mshiko mkubwa,sasa yeye anasema wakifika anataka kuwapiga helaa
😄 nakumbuka issue ilisikilizwaa lakini mwisho wa siku wale wageni kutoka China hawajaja kwake walionganisha juu kwa juu 😄
Yule mama alilaani sana akasema hawa walisoma nyakati
Sasa tukawa una ukaribu fulani akiwa na issue tunaongea,nakumbuka wakat balloon gari zinatoka alinunua alikaa nayo wiki tu akaibiwa,polisi wana haha kumpigia masimu wamsaidie kuitafuta mama anasemaa achaneni nayoo tu
😄
Sasa kuna siku nmekaa naye ndy akawa ananielezea kuhusu biashara ya pombe za ndovu na kama alitaka kuniingiza,nkasema hapana hii issue syo badaye huwa inabuma,sema kama mtu wa tamaa na hujuwi kucaLculate
Risk ....unapoteaaa

Ova
 
Si wengine wanasema Tanzania ni ngumu kutajirika kupitia mshahara halali?
Hakuna bilionea aliyeajiriwa. Matajiri wote wamejiajiri na huko kwenye kujiajiri ndiko kwenye magumashi. By the way huyu jamaa itakuwa wamechomana na wenzake baada ya kudhulumiana. Sidhani kama ndio kwanza anaanza hio biashara!
 
Lakini isije ikawa huyo jamaa amebambikiwa hayo meno ya tembo kutokana na Visa vyao binafsi kati yake na hao Askari Polisi, kwa sababu Polisi wa Tanzania hawaaminiki hata kidogo. Tusimhukumu huyo Meneja wa TRA kabla ya kumsikiliza kwanza.

Polisi Wana Kesi nyingi zimejaa kwenye "stoo" zao, ukipishana nao Kiswahili tu Basi watakupatia Kesi nzito Sana itayokufaa, kama vile "Kesi ya kichwa."

Polisi hawaaminiki kabisaaaaaaa!!

Hahaha umenikumbusha kipindi cha RFA ,Ndugu Jonathan Meshack Jambazi mtoto alipewa "KESI YA KICHWA" na maaskari .....Polisi walimbambikizia KESI YA MAUAJI wakati kesi yake ilikuwa ya ujambazi wa kutumia silaha.
 
Huko Kibondo na meno ya tembo wamenikumbusha kisa cha zamani sana cha Sharifu wa Mabamba.

Huyu Sharifu wa Mabamba kama si mjomba wake Dr. Leakey, mchambuzi maarufu wa mpira Tanzania basi atakuwa ni baba'ke mdogo.

Huyo jamaa alikuwa kinara wa kusafirisha pembe za ndovu huko Kibondo miaka ya 70s, akaingia 18 za Nyerere lakini alikuwa ni bingwa, akaipanguwa mitego ya Nyerere na akapotelea Burundi, akwa anaishi kifahamri Bujumbura na akafunguwa shirika moja kubwa la magari Burundi, inaaminika alikuwa akishirikiana biashara zake na Kiongozi wa Burundi wa siku hizo, Micombero.
Ni kaka wa mchambuzi. Alirudi Mabamba, now ni mwanachama mtiifu wa chama tawala. Ana tenda za barabara na kukodisha mbasi ya kubeba wakimbizi.
 
Ni kaka wa mchambuzi. Alirudi Mabamba, now ni mwanachama mtiifu wa chama tawala. Ana tenda za barabara na kukodisha mbasi ya kubeba wakimbizi.
Inawezekana, una maana alifilisika? Maana alikuwa tajiri mkubwa Burundi. Siku hizo Bakhresa bado anauza viatu mtaa wa Uhuru.

imi nafahamu kaka wa mchambuzi ni yule Captain wa ndege aliyeshikwa na Dhahabu, enzi za Mrema alipokuwa waziri wa mambo ya ndani.
 
Nacheka maana nnavyoijua hii biashara kufanya hutakiwi kukurupuka jamaa anavyoonekana aliingia kwa kukurupuka,utafikiri anapeleka ndizi sokoni [emoji1]
Meneja wa tra wa mkoa aibuuu sana,jamaa anaonekana alikuwa mtu wa rushwa na magendo sasa kaamua kuingia kwenye biashara ya wenyewe wanaita ya mihogo(pembe za ndovu)
[emoji1]

Ova
Wenyewe wanasema! "If you don't no the rules, don't play the game "
 
Inawezekana, una maana alifilisika? Maana alikuwa tajiri mkubwa Burundi. Siku hizo Bakhresa bado anauza viatu mtaa wa Uhuru.

imi nafahamu kaka wa mchambuzi ni yule Captain wa ndege aliyeshikwa na Dhahabu, enzi za Mrema alipokuwa waziri wa mambo ya ndani.

Wewe Bibi andika MAKALA za historia kama Mzee Mohamed Said ,una vitu vingi vya kihistoria vijana wa 2000 wajifunze.
 
Jeshi la Polisi Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma linamshikilia Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Wilayani humo Irving Mutegeki kwa tuhuma za kukutwa na meno ya Tembo.

Mutegeki Bagasheki amekamatwa na nyara hizo za Serikali Wilaya ya Kibondo Julai 2, 2024 akiwa kwenye gari binafsi majira ya usiku na anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Meneja huyo wa TRA anadaiwa amekuwa akifanya biashara ya meno ya Tembo kutoka Wilaya ya Kibondo na Kakonko kwenda mikoa mbalimbali nchini na nje ya nchi ikiwemo Burundi.
Hiki ni kielelezo cha wazi jinsi baadhi ya watumishi wa umma walivyo. Wengi ni wapigaji. Wapigaji wa mali ya umma na rasilimali zetu. Na wanalindwa na mfumo, kwamba ni watumishi wa umma. Inaonekana hata wakiiba ni kitu cha kawaida au ni kidogo.
 
Back
Top Bottom