Mtukutu wa Nyaigela
JF-Expert Member
- Sep 4, 2018
- 8,013
- 14,263
yaani hajafanya poa kabisaElimu nzuri
Mshahara mzuri
Tamaa mbele
Miaka 30 jela
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
yaani hajafanya poa kabisaElimu nzuri
Mshahara mzuri
Tamaa mbele
Miaka 30 jela
ameshindwa kuelewana na hao waliomkamata hadi anadhalilishwa hivi
Jeshi la Polisi Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma linamshikilia Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Wilayani humo Irving Mutegeki kwa tuhuma za kukutwa na meno ya Tembo.
Mutegeki Bagasheki amekamatwa na nyara hizo za Serikali Wilaya ya Kibondo Julai 2, 2024 akiwa kwenye gari binafsi majira ya usiku na anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Meneja huyo wa TRA anadaiwa amekuwa akifanya biashara ya meno ya Tembo kutoka Wilaya ya Kibondo na Kakonko kwenda mikoa mbalimbali nchini na nje ya nchi ikiwemo Burundi.
Atakua Ali leta zile za "UNAJUA MIMI NI NANI"ameshindwa kuelewana na hao waliomkamata hadi anadhalilishwa hivi
amezingua
inawezekana, au lilikuwa ni swala linajulikana muda mrefu kwamba anafanyaga hizo mambo wakamletea wakuda kutoka mbaliAtakua Ali leta zile za "UNAJUA MIMI NI NANI"
Majuto ni Mjukuu ndugu yangu, pole kwake mpambanaji hakujua siku wala saa ya kukamatwa na vithibitisho vya madili aliyokuwa anafanyaHapo anatamni siku irudi nyuma ila wapi ndio kimeshanukaa..!
Wizi wote wanaoufanya TRA haukumtosha?
Jeshi la Polisi Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma linamshikilia Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Wilayani humo Irving Mutegeki kwa tuhuma za kukutwa na meno ya Tembo.
Mutegeki Bagasheki amekamatwa na nyara hizo za Serikali Wilaya ya Kibondo Julai 2, 2024 akiwa kwenye gari binafsi majira ya usiku na anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Meneja huyo wa TRA anadaiwa amekuwa akifanya biashara ya meno ya Tembo kutoka Wilaya ya Kibondo na Kakonko kwenda mikoa mbalimbali nchini na nje ya nchi ikiwemo Burundi.
Haamini kaotewa leo 😀Si unajuwa zile wanakuambia mzee gari lako halipigwi mkono
We barabarani unafagiaaa tu 😄
Ova
Hii biashara za mihogo ina mambo mengi,ukiletewa mezaniHizo plate numbers pia😅 usikute walikuwa wanatfuta kitu kingine kbs.. ila walivyoyaona hayo manamba mengi ikabidi waingie deep..
Imenikumbusha siku moja nimetoka shamba/site nikasahau SIME kwenye gari, zikapita kama siku 3 nikaw niko Posta, hiyo siku sina hili wala lile gari ikawa imezungukwa na polisi kama vile mm ni Jambazi (Enzi za kuzuia Tinted kali) basi nikawaacha wafanye search..
Aisee wakakutana na Sime ikabidi wanipige pingu, wakaendelea kufumua mpk chini ya kapeti.. engine compartment yote chungulia mpk na tochi hawakukuta kitu kingine..
Ikabid wanihoji pale nikawaelezea ABC wakamiachia ila kwa mbinde sana..
Sasa imagine ndio umebeba labda bange hata grams mbili tu za kuvutia beach alafu msala unatokea kama hivyo wao watakutangaza kama MSAFIRISHAJI WA MADAWA YA KULEVYA.
Hakuna bilionea aliyeajiriwa. Matajiri wote wamejiajiri na huko kwenye kujiajiri ndiko kwenye magumashi. By the way huyu jamaa itakuwa wamechomana na wenzake baada ya kudhulumiana. Sidhani kama ndio kwanza anaanza hio biashara!Si wengine wanasema Tanzania ni ngumu kutajirika kupitia mshahara halali?
The bigger the risk, the higher the returnManager kazingua sana sio wa kufanya hizo kazi mbona zipo biashara safi mpaka kakimbilia kwenye deal ngumu za kuchomana hizo na pesa zake hazieleweki...
Lakini isije ikawa huyo jamaa amebambikiwa hayo meno ya tembo kutokana na Visa vyao binafsi kati yake na hao Askari Polisi, kwa sababu Polisi wa Tanzania hawaaminiki hata kidogo. Tusimhukumu huyo Meneja wa TRA kabla ya kumsikiliza kwanza.
Polisi Wana Kesi nyingi zimejaa kwenye "stoo" zao, ukipishana nao Kiswahili tu Basi watakupatia Kesi nzito Sana itayokufaa, kama vile "Kesi ya kichwa."
Polisi hawaaminiki kabisaaaaaaa!!
Ni kaka wa mchambuzi. Alirudi Mabamba, now ni mwanachama mtiifu wa chama tawala. Ana tenda za barabara na kukodisha mbasi ya kubeba wakimbizi.Huko Kibondo na meno ya tembo wamenikumbusha kisa cha zamani sana cha Sharifu wa Mabamba.
Huyu Sharifu wa Mabamba kama si mjomba wake Dr. Leakey, mchambuzi maarufu wa mpira Tanzania basi atakuwa ni baba'ke mdogo.
Huyo jamaa alikuwa kinara wa kusafirisha pembe za ndovu huko Kibondo miaka ya 70s, akaingia 18 za Nyerere lakini alikuwa ni bingwa, akaipanguwa mitego ya Nyerere na akapotelea Burundi, akwa anaishi kifahamri Bujumbura na akafunguwa shirika moja kubwa la magari Burundi, inaaminika alikuwa akishirikiana biashara zake na Kiongozi wa Burundi wa siku hizo, Micombero.
Inawezekana, una maana alifilisika? Maana alikuwa tajiri mkubwa Burundi. Siku hizo Bakhresa bado anauza viatu mtaa wa Uhuru.Ni kaka wa mchambuzi. Alirudi Mabamba, now ni mwanachama mtiifu wa chama tawala. Ana tenda za barabara na kukodisha mbasi ya kubeba wakimbizi.
Wenyewe wanasema! "If you don't no the rules, don't play the game "Nacheka maana nnavyoijua hii biashara kufanya hutakiwi kukurupuka jamaa anavyoonekana aliingia kwa kukurupuka,utafikiri anapeleka ndizi sokoni [emoji1]
Meneja wa tra wa mkoa aibuuu sana,jamaa anaonekana alikuwa mtu wa rushwa na magendo sasa kaamua kuingia kwenye biashara ya wenyewe wanaita ya mihogo(pembe za ndovu)
[emoji1]
Ova
Kabisa,hizi biashara walifanya wazee wa zamani na walikuwa na mtandao mrefu sanaWenyewe wanasema! "If you don't no the rules, don't play the game "
Inawezekana, una maana alifilisika? Maana alikuwa tajiri mkubwa Burundi. Siku hizo Bakhresa bado anauza viatu mtaa wa Uhuru.
imi nafahamu kaka wa mchambuzi ni yule Captain wa ndege aliyeshikwa na Dhahabu, enzi za Mrema alipokuwa waziri wa mambo ya ndani.
Tuwasifie pia na watumishi wa umma (polisi) waliomkamata.Pesa ya walipakodi Iko mashakani,Hawa ndio aina ya Watumishi wa Umma waliojaa maofisini.
Hiki ni kielelezo cha wazi jinsi baadhi ya watumishi wa umma walivyo. Wengi ni wapigaji. Wapigaji wa mali ya umma na rasilimali zetu. Na wanalindwa na mfumo, kwamba ni watumishi wa umma. Inaonekana hata wakiiba ni kitu cha kawaida au ni kidogo.