t blj
JF-Expert Member
- Dec 2, 2011
- 7,035
- 16,705
Manual tena??Kwakweli ni Gari lile wataalamu wameweka akili na maarifa yao hapo, ulikute manual aisee. Umadhubuti ni wahali ya juu sana kwa hizo gari.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Manual tena??Kwakweli ni Gari lile wataalamu wameweka akili na maarifa yao hapo, ulikute manual aisee. Umadhubuti ni wahali ya juu sana kwa hizo gari.
Roman catholic walikuwa na hizi benz toka miaka mingi ya nyuma,La Kanisa? Umefaidi sana aisee! Mimi sijawahi hata kuligusa kwa mkono sembuse kulipanda!
Lina upekee gani?
Kuna ya kukodi ili alau na sisi tukajionee wenyewe?Kwakweli ni Gari lile wataalamu wameweka akili na maarifa yao hapo, ulikute manual aisee. Umadhubuti ni wahali ya juu sana kwa hizo gari.
Jipya kabisa (zero kilometre) ni kwenye milioni 800 hadi 900.BEI ?.
Upo nchi gani mkuu? Sisi huku tuliko ni Mchana!Wacha niendelee kulala ili niote vizuri
mafuta utaniambia milion 50 yakushitulia tu.1😂Jipya kabisa (zero kilometre) ni kwenye milioni 800 hadi 900.
Mitumba ni kwenye milioni mia tano, mia sita, n.k. kutegemeana na hali ya gari!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]mafuta utaniambia milion 50 yakushitulia tu.1[emoji23]
Haiwezi kuwa hivyo mkuu!mafuta utaniambia milion 50 yakushitulia tu.1😂
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]mafuta utaniambia milion 50 yakushitulia tu.1[emoji23]
Mm nimeisoma hiyo milion 500 km sijui kusoma vizuri hatari😀😀mafuta utaniambia milion 50 yakushitulia tu.1😂
Kati ya G Wagon na S Class ipi zaidi?Nimeendesha Benz tofauti tofauti na sijawahi kujutia hata siku moja
Kwanza Wajerumani wana umakini sana katika kufanya mambo yao na ndio maana vitu vyao ni bei juu
Hata ujenzi na kila kitu
Kama unataka nyumba waliyoipaki wanakuletea na kuijenga kwako kama mnavyoona Sanlg wanavyofunga 😄
Hizi G Wagon hata Pope aliagiza mwaka 1980 tena aliundiwa yeye na madoido kibao
Kwanza iko juu kuliko gari zingine ina 7G tronic gearbox, na permanent wheel drive
Kuna jamaa mmoja Ganther Haltorf aliendesha G Wagon nchi 215, na maili 559,234 na haikuharibika hata siku moja
Heshima kwa Benz hata kama la zamani
G Wagon lipo kwenye orodha
G ni habari nyingine mkuuKatibya G Wagon na S Class ipi zaidi?
Kuna mtu alishawahi kusema mara yake ya kwanza kuendesha S Class alijihisi yeye si dereva. Ni tofauti kabisa na magari aliyokuwa ameshayaendesha kipindi hicho.
Gelandewagen ni ndinga matata vibaya mnoo!! Inakanyaga kokote tofauti na Sedan class ambazo ni luxury.Katibya G Wagon na S Class ipi zaidi?
Kuna mtu alishawahi kusema mara yake ya kwanza kuendesha S Class alijihisi yeye si dereva. Ni tofauti kabisa na magari aliyokuwa ameshayaendesha kipindi hicho.
🙏🙏🙏G ni habari nyingine mkuu
S class ni luxury saloon
Kazini walinipa S Class V6 ilikuwa ya manager mmoja akaniachia mimi miaka ya nyuma
Kweli lilikuwa ni gari ukikaa ndani unajua umekaa kwenye gari kwa ubora, comfortability na hata barabarani limetulia
Kwa Benz haikutupi boss
Mimi ni mhenga na miaka ya 80 nikiwa kwenye nchi moja tajiri nilinunua Benz 450sel 6.9 V8
Mkuu hii mashine hata uje na gari gani enzi hizo nikiwa kijana hunikamati
Nilikuwa nawaambia wenye GT, 280z , na hata Camaro Z na Mustang watangulie na mimi nakuja nyuma
Nawapita kama wamesimama
Turudi kwenye mada sasa G Wagon nasubiri kustaafu 😄
Ila S Class kwa G usifananishe ni magari mawili tofauti kabisa