Mercedes Benz G Wagon lina upekee gani?

Mercedes Benz G Wagon lina upekee gani?

_20240711_190519.JPG
 
G ni habari nyingine mkuu
S class ni luxury saloon
Kazini walinipa S Class V6 ilikuwa ya manager mmoja akaniachia mimi miaka ya nyuma
Kweli lilikuwa ni gari ukikaa ndani unajua umekaa kwenye gari kwa ubora, comfortability na hata barabarani limetulia

Kwa Benz haikutupi boss
Mimi ni mhenga na miaka ya 80 nikiwa kwenye nchi moja tajiri nilinunua Benz 450sel 6.9 V8
Mkuu hii mashine hata uje na gari gani enzi hizo nikiwa kijana hunikamati
Nilikuwa nawaambia wenye GT, 280z , na hata Camaro Z na Mustang watangulie na mimi nakuja nyuma
Nawapita kama wamesimama

Turudi kwenye mada sasa G Wagon nasubiri kustaafu 😄
Ila S Class kwa G usifananishe ni magari mawili tofauti kabisa
kaka shikamoo, miaka ya 80 tayari ulikuwa na ndinga.
 
kaka shikamoo, miaka ya 80 tayari ulikuwa na ndinga.
Marahaba
Hakika kabisa, nilikimbia ujamaa nikiwa mdogo 😄
1978 nikakuta wenzetu wamebarikiwa na kila kitu kwq ajili ya wese
TV nikakuta wanazo zamani na ndinga za America yaani American Muscles kama GMC wanachungia mbuzi na ngamia

Nikajipiga ndinga mshahara wa Tatu tu GT
Na baadae nikanogewa ikawa kubadili tu

Mafuta ni kama bure huko yaani jamaa wamefaidika na mafuta yao kwa kutaka wawekewe kila kitu Kama wazungu

Sisi madini yetu tunauza kama kokoto tu maana watoto bado wanakaa chini bila madawati
Wao wakwao niliwakuta wanacheza Atari games kama Ps sasa
 
G ni habari nyingine mkuu
S class ni luxury saloon
Kazini walinipa S Class V6 ilikuwa ya manager mmoja akaniachia mimi miaka ya nyuma
Kweli lilikuwa ni gari ukikaa ndani unajua umekaa kwenye gari kwa ubora, comfortability na hata barabarani limetulia

Kwa Benz haikutupi boss
Mimi ni mhenga na miaka ya 80 nikiwa kwenye nchi moja tajiri nilinunua Benz 450sel 6.9 V8
Mkuu hii mashine hata uje na gari gani enzi hizo nikiwa kijana hunikamati
Nilikuwa nawaambia wenye GT, 280z , na hata Camaro Z na Mustang watangulie na mimi nakuja nyuma
Nawapita kama wamesimama

Turudi kwenye mada sasa G Wagon nasubiri kustaafu 😄
Ila S Class kwa G usifananishe ni magari mawili tofauti kabisa
Unasemaje kuhusu bentley flying spur?
 
Hii inatesa sana madereva wa matajiri,makampuni na serikali,hata akibarikiwa la kwake la milion 25 anaona ni kama mkokoteni😁😁😁.

Ni sawa unatumia iphone 15 au s24 ofisini halafu ukirudi ghetto unatulia ktk tecno pop 1,waaaaaaaah mpaka mzuka unakata🤣🤣
It's just a poor mindset kwa sababu tunafahamu watu wanafanya kazi benki daily kuhesabu mamilioni ya pesa ambazo si mali yake,anarudi home hata laki yake mwenyewe hana. Ukitaka kujua hizi mindset zetu zilivyo za kiboya fanya kazi na mzungu. Yeye salary zaidi ya 10milion lakini yuko simple na simu simple tuu, sasa geuka kwa mmatumbi salary hata milioni haifiki lakini mashauzi sasa daaah...
 
Unasemaje kuhusu bentley flying spur?
Ni gari kubwa sana hilo
Ila kwa mimi sijalipenda hivyo
Kwa £32,000 kama 100m unaweza ukalipata la 2014 sio mbaya ingawa kuna ya ghali zaidi kwa mwaka huo
Huku naona wadosi wanashindana kuwa nayo
Hapo hujalipa ushuru kwa bongo mara 2

Kama la 2024 ni 870m ya bongo bila ushuru
Jipya litakuwa ghali sana
Kuna rafiki yangu analo jeusi sport V8
 
870 mill bila ushuru, ukiongeza ushuru billion na poing zake.. zile chuma kubwa sana, ila naona zilo na luxury kubwa sana.. walikuwa wanafanya comarison na S680 naona S alikalishwa chini.. V8 sport naona lipo la V12 au W16 kama sijakosea
 
Back
Top Bottom