Mercedes Benz G Wagon lina upekee gani?

Mercedes Benz G Wagon lina upekee gani?

Sadiq Khan anaingizaje £4m? Kwa shughuli zake binafsi?
Hapana mkuu ni makusanyo ya serikali kwa Congestion charge ambapo kila gari likiingia london mjini kuanzia saa 1 asubuhi unalipa £15 na £12.50 kwa ajili ya Ultra Low Emissions kwa kila gari
Hapo ULEZ tu karibia gari 60,000 hazikidhi kiwango cha usafi yaani wachafua hewa wanalimwa haswa na usipolipa faini yake ni £180 kama laki 5 na 40 ya home

Bado msongamano wa jiji nao lazima ulipe kama 45,000 ya bongo

Mkuu sorry hizo sio zake bali amebuni na ameongeza mipaka sasa sehemu nyingi wameiga kama Manchester, Birmingham, Leeds, Bristol nk
 
Hapana mkuu ni makusanyo ya serikali kwa Congestion charge ambapo kila gari likiingia london mjini kuanzia saa 1 asubuhi unalipa £15 na £12.50 kwa ajili ya Ultra Low Emissions kwa kila gari
Hapo ULEZ tu karibia gari 60,000 hazikidhi kiwango cha usafi yaani wachafua hewa wanalimwa haswa na usipolipa faini yake ni £180 kama laki 5 na 40 ya home

Bado msongamano wa jiji nao lazima ulipe kama 45,000 ya bongo

Mkuu sorry hizo sio zake bali amebuni na ameongeza mipaka sasa sehemu nyingi wameiga kama Manchester, Birmingham, Leeds, Bristol nk
Shukran mkuu!
Anaweza kukubali kuja kutuendeshea TRA alau kwa miaka mitano tu?
 
Kuna wazungu wanapenda adventures mkuu
Yaani mtu anaamua kuvunja rekodi yake tu
Na mimi ngoja siku moja nikate Afrika yote ila ntaandaa kitita cha kuhonga mipakani 😄
Wewe una passport kubwa mkuu, kwa nini uhonge?

Mimi nataka nifanye ya Mwanza - Dar kwa baiskeli. Mwanzoni nilitaka kufanya kwa miguu lakini baada ya kutafakari nimeona itakuwa "too much". Bora baiskeli.
 

Attachments

  • images (2).jpeg
    images (2).jpeg
    35.6 KB · Views: 5
Mercedes-Benz G-Class, maarufu kama G-Wagon, ni gari la kipekee kwa sababu kadhaa ambazo zinachangia kuifanya iuzwe kwa bei ya juu. Kwanza, historia yake ya muda mrefu na asili yake ya kijeshi inaiweka katika daraja la kipekee. Iliyotambulishwa kwanza mwaka 1979, G-Wagon ilitengenezwa kwa ajili ya matumizi ya kijeshi na imeendelea kuboresha miundo yake bila kupoteza muundo wake wa awali.

Muundo wa G-Wagon ni wa kipekee, ukiwa na umbo la kisanduku ambalo limebaki kuwa nembo ya gari hilo. Ni gari linalojulikana kwa uimara wake na uwezo wake wa kuvuka maeneo magumu na magumu zaidi, ikiwa na mfumo wa kudumu wa magurudumu manne unaoweza kushughulikia mazingira mbalimbali.

Ubora wa vifaa vinavyotumika kutengeneza G-Wagon ni wa hali ya juu sana. Gari hili linajulikana kwa kuwa na vifaa vya ndani vilivyo bora, kama vile ngozi, mbao za thamani, na teknolojia za kisasa. Pia, linajumuisha teknolojia za kisasa za usalama na urahisi wa matumizi, kama vile mifumo ya kuzuia kuteleza, kamera za nyuma, na mfumo wa burudani wa hali ya juu.

G-Wagon pia ina injini zenye nguvu kubwa, ikiwa na chaguo za injini za V8 na V12 ambazo zinatoa nguvu na kasi kubwa, pamoja na utendaji bora wa barabarani na nje ya barabara.

Utoaji mdogo wa gari hili pia huchangia bei yake kuwa juu. Kutokana na kwamba G-Wagon ni gari la kifahari na la kipekee, uzalishaji wake ni mdogo, na kufanya kuwa adimu. Hii huongeza thamani yake katika soko.

Kwa kuzingatia yote haya, Mercedes-Benz G-Wagon inauzwa bei ya juu kwa sababu ya historia yake, uimara na ubora wake, vifaa vya hali ya juu, teknolojia za kisasa, na sifa zake za kipekee. Gari hili ni zaidi ya chombo cha usafiri; ni ishara ya hali ya juu na hadhi, na hii inaonyeshwa wazi katika bei yake.

AI
 
Shukran mkuu!
Anaweza kukubali kuja kutuendeshea TRA alau kwa miaka mitano tu?
Nashangaa sijui kazi ya Mayor wa jiji ni nini huko

Labda wamuajiri Sunak awe Advisor kwenye uchumi wenu
Kama Kagame alivyomuajiri Tony Blair mwaka 2008 tena unpaid ila siamini

Mkuu Kariakoo tu ikiwekwa cameras kama za london na kuhakikisha kila usafiri unaoingia unalipia mbona TRA wasingesumbua wafanyabiashara wadogo
Ukosefu wa ubunifu ndio unasababisha wakamate mpaka Malaya

Waniajiri hata mimi ningewaweka sawa na baada ya miaka mitatu hata ajali zingepungua kwa 60%
 
Ila hio gari ukiitizama ground clearence na muonekano unapata jibu imetengenezwa kikazi zaidi sio show off..
Inasemekana hata engines zake ni handcrafted, wanatumia mikono kuzitengeneza, ina maana umakini mkubwa umetumika.

Gari in airbags 10, horsepower zaidi ya 570 si mchezo.
 
Asante mkuu, ila ni kawaida tu
Sio ujanja bali ulipoandikiwa ndio utaishi na kufia pia
Kikombe cha kahawa kawaida ni kama 10,000 Starbucks
Ila mshahara kwa mbeba box ni 10m kwa mwezi
Kwa hiyo ni sawa tu
Mbeba box anakula 10m😄

Halafu bado kuna wananzengo wanaowalinganisha masikini wa Ulaya na wa Kolomije!
 
Back
Top Bottom