Merry Christmas from Mohamed Salah. Je, anapima upepo? Waislam wamshangaa!

Merry Christmas from Mohamed Salah. Je, anapima upepo? Waislam wamshangaa!

Ni hiyari kwa waislam kukataa kutoshiriki Xmass kama ambavyo mkristo hatoshiriki Idd na sherehe zingine za kiislam.
Mambo mengine yabaki kuheshimiana na kutolazimishana.
Ila naomba kuuliza wataalam: vp ukaletewa ubwabwa wa asiye wa imani yako kwenye sherehe yake tuubwie au tuuakatae? Anijibu muislam na mkristo kila mmoja kwa upande wake.
 
Unakuta mtu sadaka hatoi kuzini anazini ila Mo Salah kupost Merry Christmas anaumia
Katika Uislamu madhambi yanatofautiana ,Kusherekea na kutambua hiyo sikukuu ni sawa na kukubali Mungu ana mwana na leo Mungu amezaliwa kitu ambacho ni dhambi kubwa sana.Hata wakifa hao watu leo huyo mwenye kusapoti itikadi hizo ana wakati mgumu sana kuliko uliowataja vilevile mtu kufanya dhambi haimaanishi usikemee .
 
Jamaa ame_tweet hii picha sasa hizo comments kutoka kwa jamii ya kiislam wamegoma kumuelewa jamaa wakidhani anataka kuokoka!.

View attachment 2457499
Wapo wa Arab wakristo,kuanzia Iraq,Turkey,Saudia mpaka Palestine,
Jana,Aljazeera,ilionyesha wa Arab wakisherehekea Christmas,bethelem,Gaza,
Sasa Rudi huku kwetu kwa mburukenge waislam weusi,wanaojiona ni Waarab zaidi kuliko Waarab wenyewe,ukiwa Zenj,hawataki kabisa kuona mkristo anakula bata la christmass
 
Katika Uislamu madhambi yanatofautiana ,Kusherekea na kutambua hiyo sikukuu ni sawa na kukubali Mungu ana mwana na leo Mungu amezaliwa kitu ambacho ni dhambi kubwa sana.Hata wakifa hao watu leo huyo mwenye kusapoti itikadi hizo ana wakati mgumu sana kuliko uliowataja vilevile mtu kufanya dhambi haimaanishi usikemee .
Mkuu ila mambo ya imani ni binafsi mtu na Muumba wake Mo Salah amepost karibu mara ya nne sasa lakini hajali na Quran anasoma Mungu ndiye atakayemuhukumu nadhani huwa anarudi kwao Misri unadhani atakuwa haambiwi na ana ndugu ambao ni waislam ,jitazame wewe na Mungu wako umesimama vipi katika imani usimuangalie mtu mwingine hata awe maarufu kiasi gani .
 
Muislamu yoyote anae sherekea hiyo siku jua tu ajitambui na ni jahilliya asie jua misingi ya Dini yake.

kutojitambua ni kuungana na wakristo wengine walio hollyday nawewe unalala,kama ni mwalimu huendi shuleni kufundisha.

nenda shuleni hivyo hivyo hata ukachore chore tu ubao.

chini ya dini mnakuwa kama mambuzi.
 
Christmass asili yake ni sikukuu ya kipagani, haimo kwenye bible na wala Yesu hajawahi kuisherehekea.

Mashabiki wako sahihi kumrudisha katika njia sahihi.

Kwenye uislamu ukipotea njia unakumbushwa, na hapo Mo Salaa anakumbushwa!

anakumbushwa na watu ambao hajui wametenda yepi yasiyoonekana.

hoja hapa ameungana na wakristo wote kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa kristo,inaambatana na siku ipi hilo ni swala jingine.

hata hiyo eid huna uhakika 100% kama ni siku halisi aliyozaliwa mtume wako.
 
Kwanza sio waislam tu ambao hawataki kusikia kitu kinacho itwa krismas hata baadhi ya wakristo wenzenu wana ipinga mfano ni wasabato na waothodoxs.

Kwa mjibu wa uislamu hakuna kitu kinacho itwa krismas ila kwa sababu jamii yetu ni jamii mchanganyiko wa dini hasa uislamu na ukristo ni vyema kufumbia macho baadhi ya mambo ili maisha yaende ,ila ukifuata maandiko ya dini hii sikukuu muislam haruhusiwi kuihusudu kwa namna yeyote ile.

orthodox na sda wamekaa chini wameatamia mayai yao.

wewe kanzu juu juu unapambana na salah ambaye hapangiwi cha kufanya!!!!
 
Moja ya Sababu uisilamu upo vile vile haujabadilishwa mpaka leo ni hio, Jamaa yupo wrong na waisilamu wengine wana haki ya kumuambia kama amekosea

haubadiliki achana na story hizo.

tokea enzi za punda mpaka leo unadhani vingapi vebadilika??imeandikwa wapi mtumie speaker za umeme kuitia watu msikitini???

miaka 50 ijayo utaingia msikitini na viatu sababu ni visafi,sio kwa sababu umeagizwa uvue muda wote.
 
Hao waislam unao taka wakupende na kukuheshimu je ww unawapenda na kuwaheshimu?

wakristo wanawapenda sana waislam ila asante zinarudigi kwa namna mbaya sana.

unyanyapaa,kejeli na makasiriko.

shida ni usataarabi tu,kuna dini inafanya watu waishi kama kuku.
 
wenyewe ukiwa Zenj hawataki kabisa kuona mkristo anakula bata la christmass
Bata linaliwa mkuu (sikupata picha ya forodhani jana) ila nyomi ilikuwepo, hata Rais mwenyewe anaitambua na katoa ulinzi mahala tofauti ili kushereheka kwa amani.

Screenshot_2022_1226_185310.jpg
 
Mkuu ila mambo ya imani ni binafsi mtu na Muumba wake Mo Salah amepost karibu mara ya nne sasa lakini hajali na Quran anasoma Mungu ndiye atakayemuhukumu nadhani huwa anarudi kwao Misri unadhani atakuwa haambiwi na ana ndugu ambao ni waislam ,jitazame wewe na Mungu wako umesimama vipi katika imani usimuangalie mtu mwingine hata awe maarufu kiasi gani .
Umma huu umesifiwa kuwa Umma bora kutokana na watu kukatazana maasi na kuamrishana mema ,na kwenye dini ya Uislamu lazima kila mtu aonywe bila kujali mambo mengine vilevile katika kuonywa mtu vilevile watu wengine wakapata fursa ya kutambua kuwa jambo fulani ni kosa .

Katika Qu'ran
Mkuu ila mambo ya imani ni binafsi mtu na Muumba wake Mo Salah amepost karibu mara ya nne sasa lakini hajali na Quran anasoma Mungu ndiye atakayemuhukumu nadhani huwa anarudi kwao Misri unadhani atakuwa haambiwi na ana ndugu ambao ni waislam ,jitazame wewe na Mungu wako umesimama vipi katika imani usimuangalie mtu mwingine hata awe maarufu kiasi gani .
Umma huu umepewa hadhi ya kuwa Umma bora moja Kati ya sababu ni watu kukatazana maasi na kuamrishana mema , hivyo ni lazima uovu usemwe ili mtu abadilike au wengine wapate mazingatio kutokana na hayo.

Na jambo hilo la kukatazana maovu na madhambi limesisitiziwa mno katika Qu'ran na Sunna
ETzSrA5UUAE9Z-A(1).jpg
 
Sasa kama sio mwenyewe kinacho kuuma ni nini? Wewe endelea na birth day ya Yesu, sie tuna Issa nessiah bin Maryam, sioni haja ya kutukana labda ni chuki zako binfsi dhidi ya Dini tukufu ya haki na ya Allah
Safi kabisa. Ninyi mna Isa bin Mariam.

Sasa tusiwasikie tena mkimuegemeza huyo Isa kwa Yesu.

Mwacheni isa wenu ajitegemee mwenyewe. Kitendo cha kumwegemeza kwa Yesu wa Biblia kinamfanya huyo isa aonekane dhaifu sana asiyeweza kusimama mwenyewe.

Mbona wakristo hawana time kabisa na huyo Isa wenu?
 
Back
Top Bottom