Mesut Ozil ametangaza rasmi kustaafu mpira wa miguu

Mesut Ozil ametangaza rasmi kustaafu mpira wa miguu

fyddell

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2011
Posts
12,026
Reaction score
22,549
Mesut Ozil, mchezaji wa zamani wa Arsenal, Real Madrid na kiungo wa timu ya taifa ya Ujerumani ametangaza rasmi kustaafu mpira wa miguu akiwa na umri wa miaka 34.

Akiandika katika page yake ya Instagram akisema "Ilikuwa ni dhahiri na sasa ni wazi kuwa muda wa kuacha mpira katika hatua kubwa umefika".

Mechi yake ya mwisho ilikuwa ni February 2 alipofanyiwa mabadiriko baada ya timu yake Basaksehir kufungwa 1-0 katika ligi ya Uturuki. Ilikuwa ni mara yake ya pili kuanza kipindi cha kwanza katika mechi mbili alizozichezea klabu yake hiyo tangia aliposaini akitokea Fenerbahce msimu uliopita.

Sky Sports

images (3).jpeg
images (4).jpeg

images (5).jpeg
 
Nitakumbuka kiungo wangu ukiichezea Arsenal katika kiwango chako cha hali ya juu, ukaondoka kuelekea Fenerbahce huku mashabiki wa Arsenal bado wakikuhitaji lakini kocha hakukuona ukifit katika mipango yake.
 
Back
Top Bottom