Ozil akiwa Real Madrid alikuwa na Ronaldo, Di Maria na Benzema wachezaji ambao daima walikuwa mbele yake. Matamanio ya wachezaji hao watatu kupata matokeo mazuri ni ono la kila shabiki wa mpira na hakika walifunga kutokana na ubora wa kiungo Ozil. Kwa upande wa Arsenal na falsafa za Arsene Wenger za kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa Ozil akiwa mbele ya Mikel Arteta na Aaron Ramsey alikuwa akionekana wa kawaida kwasababu akiwa nyuma, upande wa kushoto Saint Cazorla na kulia Walcott mbele kabisa Geroud hakuona mtu ambaye yuko tayari hata kuvunjika miguu ili aingie kwenye box. So naweza kuconclude kuwa Ozil wa Real Madrid alikuwa bora zaidi ya Ozil wa Arsenal.