Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Walikuwa wapi siku zote kuanza ujenzi hadi wasubiri kipindi cha kampeni tena Maji ya shingo???Are you insane? Barabara ilishafanyiwa upembuzi yakinifu. Alafu rais anasema ataijenga ni rushwa? Kuwashauri watu wa Bunda wasikosee kuchagua ni kuwatisha.
Mwaka huu kuna mgombea mzuri na anayetosha Kama Tundu Lissu?Hakuna msimu chadema wamekosa mgombea uraisi kama awamuu hiiii.
Maana ukiangalia mgombea walie mpisha, kwenye kujenga hoja na kuleta heshima ya mgombea uraisi, kiukweli anapwaya saana. Tungu lisu mda wote wa kampeni anautumia kama mwanaharakatii. Sasa hiii imesha mgarimu, vinginevyo abadili namna ya kuendesha kampeniii. Au viongozi wenzake wamshauliiii.
Swali ni je Kwa nini afanye kipindi hichi cha kampeni???Ujenzi umeanza mkuu? Mtendaji mkuu Tanroads ameambiwa atangaze tenda. Alafu kila jambo na wakati wake.
Unajua kanuni na maadili ya uchaguzi???Yeye bado anawatumikia watanzania kwani, wewe hujui?
Ujenzi umeanza mkuu? Mtendaji mkuu Tanroads ameambiwa atangaze tenda. Alafu kila jambo na wakati wake.
Ovani kweli wanatapa-tapa hadi wameenda kumkokota Mama Maria Nyerere aje kuwaombea kura lakini akawadhalilisha jukwaani.
Naona mkuu CHADEMA imekunata akilini. Kutaja kuwa CHADEMA inakwapua hela ya Serikali badala ya CCM, inadhihirisha hoja hiyo. Pili n kwamba CCM bila msaada wa tume ya uchaguzi na vyombo vya dola na habari ni wepesi sana. Kama CCM inapendwa na wananchi kwa nini itumie tume kuengua wagombea wa upinzani na kutisha vyombo vya habari visitangaze kampeni za wapinzani? "The entire media through CCM influence is biased against the opposition. Shame on CCM!"Uchaguzi wa mwaka huu ulionyesha mapema kabisa kuwa CCM itashinda kwa urahisi sana. Hii ni kwa sababu kazi nzuri iliyofanyika ndani ya miaka minne ilikuwa ni kete tosha kwa CCM kutusua bila matatizo
Zimebaki siku 49 watanzania waende kupiga kura ili kuchagua wabunge, madiwani na rais wa JMT kakini mpaka siku ya leo inafika tayari Chadema wameshaonyesha kushindwa. Na hii ni kwa sababu wamenza kulialia kama watoto wadogo.
Kitendo cha mgombea urais wa CHADEMA kuanza kutoa sababu ambazo hazina msingi,hizi ni Dalili kuwa sasa jahazi linazama. Mfano kulialia kwa waandishi wa habari kuwa sasa hana pesa na inalazimu kutembeza bakuli hii ni dalili kuwa hali ni mbaya. Lakini kwa nini hakufanya tahimini kuwa Chama chake hakina fedha hivyo akakaa kando na kuacha kuingia kwenye mtanange ambao ni gharama kubwa kuuendesha? Lissu hakufanya tathimini kuwa kuna michango ya wabunge iliyokuwa itumike kwenye uchaguzi ilikwapuliwa na wamiliki wa Chadema? Maana hii ni aibu kutembeza bakuli wakati wananchi tuna hali ngumu.
Kusema kuwa CHADEMA wanachota pesa za serikali pia ni dalili kuwa huyu jamaa amekosa hoja za msingi. Hivi hajui kuwa Ccm wana asset ambazo zinawaingizia pesa lukuki ambazo wakizikusanya kwa miaka mitano zinaweza kuendesha kampeni kwa ufanisi mkubwa? Kutoa sababu eti Hayati Benjamin Mkapa alisema kuna watu walimdanganya na kukwapua pesa za Epa sio justification kuwa Ccm inachota pesa serikalini. Maana CCM ya mwaka 2005 sio hii ya leo.
Kuleta hoja eti CCM imepitisha mgombea ubunge wa Njombe ambae alikuwa na mashitaka ya ufisadi. Kwa hiyo Ccm haipambani na ufisadi huku nako ni kukosa hoja zenye mashiko na zisizo na msaada kwa CHADEMA . Mimi nafikili kama chama makini wangetuambia namna gani watamshinda huyu mgombea ubunge aliyekuwa na makosa ya ufisadi ili wachukue jimbo la Njombe kuliko kuanza kulalama juu ya kuteuliwa kwake kugombea. Pia ifahamike huyu mgombea baada ya kubainika amefanya makosa ya kusaidia Acaccia wasilipe kodi alikamatwa nakufunguliwa mashitaka na kisha kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria. Na hukumu yake haijamuondolea sifa ya kuwa mgombea ubunge. Kwa hiyo ni wazi kuwa serikali ya CCM ilichukua hatua stahiki, kusema kwamba haipambani na ufisadi ni uongo na kukosa hoja.
Kujibu hoja ya kuwa anatumiwa na mabeberu kizembe hivyo pia imeonyesha ni wazi kuwa anapata misaada toka kwa mabeberu. Maana huwezi kusema kuwa kisa Usaid au JICA wakitoa misaada tayari tumepata msaada toka kwa mabeberu. Maana dhana nzima ya ubeberu huwa inakamilika pale misada ya taifa lenye uwezo linapotoa msaada ambao una lengo la kuinyonya nchi yetu kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni. Hili hajajibu vuzuri maana anakiri kuwa impliedly kuwa anapata misaada. Je hiyo misaada anaipata kwa mashariti gani huyu ndugu Lissu? Ili aje alinde faragha za watu wanaovunja sheria za nchi!
Kusingizia media za Tanzania hazifanyi coverage ya mikutano yake ni aibu na hii ndio imeonyesha sasa ameishiwa nguvu. Amesahau kilichotokea pale Zakheim? Lakini pamoja na hayo mimi naona vyombo vya habari karibu vyote vinaripoti mikutano yake.
Kusema rais anatumia madaraka yake kujipatia kura. Hili nalo linachanganya. Kwani Tundu Lissu hajui kuwa ukomo wa rais wa JMT ni mpaka aapishwe mwingine? Maana pale Nyehunge rais Magufuli alikuwa anatumia kofia yake ya urais kutekeleza majukumu yake,na kwa katiba ya JMT lipo wazi. Ila dalili zinaonyesha sasa maji yamefika shingoni na baada ya siku kumi itakuwa aibu kwa Chadema.
Laana kubwa.
Kwa kujifariji mnawezaa. Yaani anatia huruma, alidhani kwa zile kiki alizozifanya halafu akatimkia ugaibuni, alidhani akirudi atapindua meza fasta kwa kutumia kiki ya miujizaaa, sasa zote zimebumaaa.Mwaka huu kuna mgombea mzuri na anayetosha Kama Tundu Lissu???