Uchaguzi 2020 Mfa maji haachi kutapatapa! CHADEMA maji shingoni

Uchaguzi 2020 Mfa maji haachi kutapatapa! CHADEMA maji shingoni

😂😂😂😂 acha kuchekesha wewe kilaza wa Lumumba!! Yaaani Tundu Lissu atafute kiki???
Sasa chadomo bila kiki kuna hojaa palee.
Lisu wenu zaidi ya kupayukapayuka, na kiuanaharakati, kuna mtu pale. Kiki zake zote zimebumaaa
 
Ni kweli kabisa wanatapa-tapa sana hadi wameenda kumkokota Mama Maria Nyerere aje kuwaombea kura lakini akawadhalilisha jukwaani.
Walimuomba na kifimbo cha baba wa taifa , akawanyima wakataka kukichukua kwa nguvu , ulimsikia Makongoro nimeacha kifimbo nipo na mama , walishindwa kukichukua.
 
Hakuna msimu chadema wamekosa mgombea uraisi kama awamuu hiiii.

Maana ukiangalia mgombea walie mpisha, kwenye kujenga hoja na kuleta heshima ya mgombea uraisi, kiukweli anapwaya saana. Tungu lisu mda wote wa kampeni anautumia kama mwanaharakatii. Sasa hiii imesha mgarimu, vinginevyo abadili namna ya kuendesha kampeniii. Au viongozi wenzake wamshauliiii.
Wakubwa wenu vichwa vimevimba kwa mchaka mchaka wa Lissu wewe unaropoka tu hapo,au hujaona push ups zimeanza tena.
 
Ni kweli kabisa wanatapa-tapa sana hadi wameenda kumkokota Mama Maria Nyerere aje kuwaombea kura lakini akawadhalilisha jukwaani.
Alifikiri uraisi ni kula myama choma na bia akiwa ana hudumiwa na mzungu huko uberigiji?
Mmemdanganya kwenye mitandao nae akavimba kichwa sasa joto linamuwakia.
Kama ameshindwa kumuuliza Mbowe wapi pesa za wabunge zipo, basi wacha akione cha moto.
 
Uchaguzi wa mwaka huu ulionyesha mapema kabisa kuwa CCM itashinda kwa urahisi sana. Hii ni kwa sababu kazi nzuri iliyofanyika ndani ya miaka minne ilikuwa ni kete tosha kwa CCM kutusua bila matatizo
Kamwe usimchukulie poa adui yako. Usifanye kosa hilo kabisa
 
Alifikiri uraisi ni kula myama choma na bia akiwa nhudumiwa na mzungu huko uberigili?
Mmemdanganya kwenye mitandao nae akavimba kichwa sasa joto linamuwakia.
Kama ameshindwa kumuuliza Mbowe wapi pesa za wabunge zipo, basi wacha akione cha moto.
mataga hapa tayari umeshapanic 🤣 🤣 🤣
 
Lis
Wakubwa wenu vichwa vimevimba kwa mchaka mchaka wa Lissu wewe unaropoka tu hapo,au hujaona push ups zimeanza tena.
Lisu anamchamchaka gani, ambao unaweza kuisumbua ccm? Hivi lisu inje ya kupayuka na kushudia kiki za miujiza na kuwatoza watu sadaka za lazima na kuwataka wanatanzania wampe uraisi kama kifuta machozi, anasera zipiii?? Au unataka tuanike kiki zenu zote hapa??
 
Dah uvccm humu hoja hakuna..yaani ni empty kichwani hawana critical reasoning mihemko na mahaba niue ya chama yamewajaa kichwani... Mpaka Muite maji mmma.[emoji16][emoji16][emoji16][emoji18]
 
Uchaguzi wa mwaka huu ulionyesha mapema kabisa kuwa CCM itashinda kwa urahisi sana. Hii ni kwa sababu kazi nzuri iliyofanyika ndani ya miaka minne ilikuwa ni kete tosha kwa CCM kutusua bila matatizo

Zimebaki siku 49 watanzania waende kupiga kura ili kuchagua wabunge, madiwani na rais wa JMT kakini mpaka siku ya leo inafika tayari Chadema wameshaonyesha kushindwa. Na hii ni kwa sababu wamenza kulialia kama watoto wadogo.

Kitendo cha mgombea urais wa CHADEMA kuanza kutoa sababu ambazo hazina msingi,hizi ni Dalili kuwa sasa jahazi linazama. Mfano kulialia kwa waandishi wa habari kuwa sasa hana pesa na inalazimu kutembeza bakuli hii ni dalili kuwa hali ni mbaya. Lakini kwa nini hakufanya tahimini kuwa Chama chake hakina fedha hivyo akakaa kando na kuacha kuingia kwenye mtanange ambao ni gharama kubwa kuuendesha? Lissu hakufanya tathimini kuwa kuna michango ya wabunge iliyokuwa itumike kwenye uchaguzi ilikwapuliwa na wamiliki wa Chadema? Maana hii ni aibu kutembeza bakuli wakati wananchi tuna hali ngumu.

Kusema kuwa CHADEMA wanachota pesa za serikali pia ni dalili kuwa huyu jamaa amekosa hoja za msingi. Hivi hajui kuwa Ccm wana asset ambazo zinawaingizia pesa lukuki ambazo wakizikusanya kwa miaka mitano zinaweza kuendesha kampeni kwa ufanisi mkubwa? Kutoa sababu eti Hayati Benjamin Mkapa alisema kuna watu walimdanganya na kukwapua pesa za Epa sio justification kuwa Ccm inachota pesa serikalini. Maana CCM ya mwaka 2005 sio hii ya leo.

Kuleta hoja eti CCM imepitisha mgombea ubunge wa Njombe ambae alikuwa na mashitaka ya ufisadi. Kwa hiyo Ccm haipambani na ufisadi huku nako ni kukosa hoja zenye mashiko na zisizo na msaada kwa CHADEMA . Mimi nafikili kama chama makini wangetuambia namna gani watamshinda huyu mgombea ubunge aliyekuwa na makosa ya ufisadi ili wachukue jimbo la Njombe kuliko kuanza kulalama juu ya kuteuliwa kwake kugombea. Pia ifahamike huyu mgombea baada ya kubainika amefanya makosa ya kusaidia Acaccia wasilipe kodi alikamatwa nakufunguliwa mashitaka na kisha kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria. Na hukumu yake haijamuondolea sifa ya kuwa mgombea ubunge. Kwa hiyo ni wazi kuwa serikali ya CCM ilichukua hatua stahiki, kusema kwamba haipambani na ufisadi ni uongo na kukosa hoja.

Kujibu hoja ya kuwa anatumiwa na mabeberu kizembe hivyo pia imeonyesha ni wazi kuwa anapata misaada toka kwa mabeberu. Maana huwezi kusema kuwa kisa Usaid au JICA wakitoa misaada tayari tumepata msaada toka kwa mabeberu. Maana dhana nzima ya ubeberu huwa inakamilika pale misada ya taifa lenye uwezo linapotoa msaada ambao una lengo la kuinyonya nchi yetu kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni. Hili hajajibu vuzuri maana anakiri kuwa impliedly kuwa anapata misaada. Je hiyo misaada anaipata kwa mashariti gani huyu ndugu Lissu? Ili aje alinde faragha za watu wanaovunja sheria za nchi!

Kusingizia media za Tanzania hazifanyi coverage ya mikutano yake ni aibu na hii ndio imeonyesha sasa ameishiwa nguvu. Amesahau kilichotokea pale Zakheim? Lakini pamoja na hayo mimi naona vyombo vya habari karibu vyote vinaripoti mikutano yake.

Kusema rais anatumia madaraka yake kujipatia kura. Hili nalo linachanganya. Kwani Tundu Lissu hajui kuwa ukomo wa rais wa JMT ni mpaka aapishwe mwingine? Maana pale Nyehunge rais Magufuli alikuwa anatumia kofia yake ya urais kutekeleza majukumu yake,na kwa katiba ya JMT lipo wazi. Ila dalili zinaonyesha sasa maji yamefika shingoni na baada ya siku kumi itakuwa aibu kwa Chadema.
Chadema ilishajifia baada ya ccm kugeuzwa kuwa Magufuli.
 
Kitendo cha tume kuengua wagombea wa upinzani inaonyesha ccm hali mbaya
 
Huu uchaguzi una uhaba mkubwa wa mabango na bendera za kampeni hata za mwaka 1995 nyingi. Nadhani ni mambo ya funds. Just thinking aloud.
Mabango yote ya upinzani TRA wameambiwa walipie kodi, ya ccm bure
 
Back
Top Bottom