Uchaguzi 2020 Mfa maji haachi kutapatapa! CHADEMA maji shingoni

Ndugu zangu,

Sisi waswahili huwa tuna msemo ''ukiona kenge anatoa damu masikioni ujue anakufa''..hali ipo hivi, yawapasa muelewe. Hakuna mtu anayeweza kusema ''nimeshindwa'' au ''tumeshindwa'' hasa ikiwa alishajigamba na kujimwambafai kuwa anashinda saa mbili asubuhi.

Kauli za ''kiutu uzima'' ni kama ''hatuna pesa za kampeni'', ''mguu wangu haukunjuki'' ''habaru zangu hazirushwi'',''mshindani wangu anahela sana''.

Kwa wale tunaojua hesabu za ''cross multiplications'' tunasema ''ikiwa Tundu kafanya mikutano 10 ndani ya siku 10 basi ndani ya siku 60 anatafanya mikutano 60''

Ukweli ni kuwa angalau ya watanzania asilimia 70 wanaishi vijijini sasa kama kishagundua kuwa hawezi kukutana na kushawishi wanachi walio wengi wampigie kura, ni dhahiri kishaanguka.

Wakati umefika ambao Robert Amsterdam amejichokea na kutokomea bila kuandika ''vijibarua vyake uchwara''.

Uraisi sio Urahisi.
 
Huu uchaguzi una uhaba mkubwa wa mabango na bendera za kampeni hata za mwaka 1995 nyingi. Nadhani ni mambo ya funds. Just thinking aloud.
 
Naona kilaza wa Lumumba umekuja kujidhalilisha humu!

Kwanza nani kakwambia mgombea wa Chadema kalalamika hawana hela? Aliulizwa swali juu ya bajeti na akaelezea kuwa wanategemea michango, shida iko wapi?

Kwani ni uongo kuwa mmempitisha mgombea ambae mlidai ni fisadi na anashirikiana na mabeberu kugombea Ubunge njombe????? Hapa hamna lolote lile la kujisafisha.

Kuhusu raisi kutoa kufanya utekelezaji kipindi cha kampeni hivi hujui kuwa kuna maadili ya uchaguzi??? Hujui kuwa kuna kitu kinaitwa rushwa kwenye uchaguzi!? Mtu kuwa raisi haiondoi ukweli kuwa na yeye ni mgombea ivyo lazima aheshimu miiko na taratibu a uchaguzi!

Ni dhahili kuwa sasa CCM mmeshindwa kuja na majibu ya hoja za Lissu hivyo mmeamua kufanya upotoshaji ila ukweli ni kuwa watanzania tumemuelewa sana Lissu.
 
Are you insane? Barabara ilishafanyiwa upembuzi yakinifu. Alafu rais anasema ataijenga ni rushwa? Kuwashauri watu wa Bunda wasikosee kuchagua ni kuwatisha.
Walikuwa wapi siku zote kuanza ujenzi hadi wasubiri kipindi cha kampeni tena Maji ya shingo???
 
Mwaka huu kuna mgombea mzuri na anayetosha Kama Tundu Lissu?
 
Walikuwa wapi siku zote kuanza ujenzi hadi wasubiri kipindi cha kampeni tena Maji ya shingo???
Ujenzi umeanza mkuu? Mtendaji mkuu Tanroads ameambiwa atangaze tenda. Alafu kila jambo na wakati wake.
 
Chama chochote kushinda uchaguzi sio tu inategemea uongozi wake umefanya vitu vingapi! bali ni lazima kwenda mbali zaidi kujiuliza hivyo vitu vimefanyika kwa njia zipi na wakati gani alafu visingefanyika je,chama kingine kingefanya kwa njia gani na ubora gani kulinganisha na lasirimali watu na vitu vilivyopo.

Kwaufupi nilazima tutambue sera mbadala na namna gani ya kufanya vitu na manufaa yake kwa watu na kwa wakati kuliko kujivuna kufanya tu ,wakati labda kuna wengine wanaweza kufanya zaidi ya hapo bila kuumiza wananchi wake.
 
Naona mkuu CHADEMA imekunata akilini. Kutaja kuwa CHADEMA inakwapua hela ya Serikali badala ya CCM, inadhihirisha hoja hiyo. Pili n kwamba CCM bila msaada wa tume ya uchaguzi na vyombo vya dola na habari ni wepesi sana. Kama CCM inapendwa na wananchi kwa nini itumie tume kuengua wagombea wa upinzani na kutisha vyombo vya habari visitangaze kampeni za wapinzani? "The entire media through CCM influence is biased against the opposition. Shame on CCM!"
 
Mwaka huu kuna mgombea mzuri na anayetosha Kama Tundu Lissu???
Kwa kujifariji mnawezaa. Yaani anatia huruma, alidhani kwa zile kiki alizozifanya halafu akatimkia ugaibuni, alidhani akirudi atapindua meza fasta kwa kutumia kiki ya miujizaaa, sasa zote zimebumaaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…