Dabil
JF-Expert Member
- Sep 30, 2021
- 6,823
- 15,293
Kitendo alichofanyiwa mshambuliaji wa Yanga Princess na timu ya Taifa ya Tanzania U17 (Seregenti Girls) Clara Luvanga na maafisa wa Cameroon cha kumkagua njisia yake sio kitu cha kiugwana bali ni udhalilishaji, Unyanyasaji na Ubaguzi wa hali ya juu.
-Some time mpira wa Afrika una mambo ya ajabu ajabu sana yaani wale maafisa mpaka wanataka kulazimisha kumkagua mtu uwanjani hivi hii ni haki kweli? Nigeria ina wachezaji wengi wenye maumbo ya kiume kwa nini wao hawajakaguliwa jinsia zao.
-Pongezi nyingi ziende kwa maafisa wa Tanzania ambao waliambatana na timu pamoja na bechi la ufundi la Serengeti Girls kwa kumjenga kisaikolojia Clara pamoja na udhalilishaji aliofanyiwa akawafunga magoli matatu pekee yake kwenye ushindi wa magoli 4-1.
Walikosea ,wangekuwa na mashaka naye baada ya mechi wangeandika malalamiko CAF. Ila nina mashaka mashindano yanavyoendelea timu zingine zitalalamika ,Viongozi wa timu na maafisa wanatakiwa wawe na msimamo mkali asidhalilishwe.